Angalizo: Wafuasi wa CHADEMA msigeuze changisha changisha yenu kuwatapeli watu

Angalizo: Wafuasi wa CHADEMA msigeuze changisha changisha yenu kuwatapeli watu

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Huu utaratibu wa kuwachangisha watu kwa sababu mbalimbali unamapungufu mengi sana tunaomba serikali iingilie Kati kuna ufisadi mkubwa sana Wananchi wanafanyiwa kupitia hii michango ambayo wafuasi wa chadema wamekuwa wakichangisha watu kila uchao na ukijaribu kuhoji kidogo tu juu ya mapato na matumizi wanaporomosha matusi.

Tunaomba serikali izuie huu utaratibu wa kuchangisha watu ambao una cover nchi nzima badala yake uchangishaji uratibiwe na viongozi wa serikali za mitaa ambapo mchangiwa anatoka ili kuwafuta hawa watu wanaochangisha watu kiholela.

Pia iwe marufuku kwa Chama Cha siasa kutangaza kwenye vyomba vya habari michango ya aina yyte ile kwa Wananchi badala yake michango ichangishwe Kama harambee na wafuasi wao wanapokutana kwenye vikao vyao

👉🏿Mapungufu ya wachangishaji Ni Kama yafuatayo;

1. Michango haina deadline.

2. Elimu haitolewi yakutosha kwa wachangiaji

3. Hawatoi mrejesho na mchanganuo wa matumizi

4. Michango inagubikwa na usiri mkubwa kiasi kwamba hata mpokeaji hawezi toka hadharani kutaja kiasi alichopewa.

5. Ni michango inayogubikwa na tamaa ya kujilimbikizia Mali ndo maana tunaona Kuna vyama vinapokea ruzuku lakini bado kila siku viongozi wao wanaanzisha majina mbalimbali ya michango.

6. Hakuna uwazi wa mapato na matumizi mf. Join the chain.

NB; Mimi binafsi sipendezwi watu wanapotumia shida za watu Kama mradi wa kujiingizia kipato hii hali inafanya vijana kuwa dumavu wa maendeleo na kutegemea michango ya watu kuibia watu, Kama wanafanya hivo Kama nilivyoeleza waache Mara moja.
 
CCM ndio matapeli wakubwa na mbaya zaidi wanauza nchi kama vile utapeli hautoshi.

Hakuna Matapeli kwenye hii nchi kama CCM,
 
CCM ndio matapeli wakubwa na mbaya zaidi wanauza nchi kama vile utapeli hautoshi.

Hakuna Matapeli kwenye hii nchi kama CCM,
Kuwepo na utaratibu wa kutaifisha hz donation za kitapeli
 
Umechangishwa nini au kipi hasa kinakuwasha?.
 
mazoea hujenga tabia....

kuomba omba kuchangiwa ndio hulka, na ndio sura ya CHADEMA kwasasa..

na hakuna namna unaweza kuwatoa kwenye mazingira hayo...

kwasa msimamo, sera, uelekeo na malengo yake ni kuomba omba chochote kitu ndani na nje ya nchi ili wapate chakula, hakuna nia au dhamira nyingine waliyonayo hata tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 🐒
 
Kabisa wamefanya mradi wa kujipatia kipato
 
Back
Top Bottom