#COVID19 Angekubali Chanjo na kuchukua tahadhari mapema, mpaka leo huenda tungekuwa naye

#COVID19 Angekubali Chanjo na kuchukua tahadhari mapema, mpaka leo huenda tungekuwa naye

Wewe uwezo wako wa kupambunua mambo umekufikisha kwenye hitimisho lipi?
Bado sijachanja. Sijafikia bado hitimisho kuhusu chanjo na samia na jpm wana mtazamo tofauti kuhusu covid
 
Wiki iliyopita, tumezika wazee mashuhuli wawili hapa mtaani kwetu. Walikua wamepata Chanjo ya UVIKO-19, lakini walifariki kwa dalili za Ugonjwa huo.
Funzo: Mungu ndiye anayejua nani atakufa kwa sababu ya nini na lini.
Tumshukuru Mungu kwa yote.
 
Bado sijachanja. Sijafikia bado hitimisho kuhusu chanjo na samia na jpm wana mtazamo tofauti kuhusu covid
Utofauti wa mitazamo yao imeleta impact gani.

Kumbe hujachanja? Sasa una utofauti gani na Magu.?
 
Wakulaumiwa ni yule aliyekuwa Katibu mkuu Afya na daktari wake binafsi kwa kuacha kumwambia ukweli
Ulikuwa upumbavu mkubwa kumuacha mtu mwenye tatizo la moyo ajichanganye na wahanga wa covid 19 hata baada ya Kijazi na walio karibu naye kufariki kwa kinacho aminika ni Uviko
 
Tupate funzo kupitia hili, Sio kwamba unapokua mkubwa kifedha/kimadaraka ni unaona kila mtu unamzidi akili, hapana Mungu alituumba akatupa akili akatubariki akatufanya tuishi kwa kutegemeana ili kutatua mambo mbali mbali ya duniani.

Mungu akawabariki wataalamu mbalimbali, watabibu, waalimu, wahasibu, wanajeshi, wanasayansi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, wanamichezo nk.

Hawa wote tunaishi kwa kutegemeana ili maisha yasonge, mimi muhasibu nikiugua nitaenda kwa mtabibu, mwanajeshi akitaka kula ataenda kwa mkulima, mwanasiasa akitaka haki ataenda kwa wanasheria wamsaidie, mwalimu akipata tatizo la kiusalama ataenda polisi, polisi akitaka elimu atarudi kwa mwalimu, hivyohivyo kwa wote.

Inapotokea wewe umewadharau wenzio na kuona unaakili kuliko wote ndugu yangu unajidanganya.

Matabibu wamekwambia ukiwa na ugonjwa sugu tafadhari zingatia miongozo kwa usahihi maana upo kwenye risk kubwa, wewe kwa kiburi chako ukaona unacheo kikubwa na kuwadharau wengine ukijiona umewazidi akili matokeo yake utayaona.

Wewe mmoja huwezi kuwa mkemia, ukawa mtabibu, ukawa mwalimu, ukawa mchungaji, ukawa mfamasia, ukawa mwanasaikolojia tafadhali heshimu kada za wengine.

Ndugu yangu kufa kupo lakini na kufa kijinga kupo,
bibilia inasema usiwe mjinga kupita kiasi ukafa kabla ya siku zako

Mhubiri 7:17
Usiwe mwovu kupita kiasi;
Wala usiwe mpumbavu;
Kwani ufe kabla ya wakati wako?


Kwa maana hiyo ni kwamba sio kila mtu anaekufa basi ni wakati wake, wengine hufa kabla ya wakati kwa upumbavu.

Pengine ungeheshimu taaluma za watu ukachukua tahadhari mpaka leo tungekua pamoja tukiijenga Tanzania Mama,

Dharau na kibuli havijawai kumuacha mtu salama tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu

View attachment 1924317
Lipo jambo la kujifunza, Mungu ni Mkuu wa wakuu wote full stop.
 
Back
Top Bottom