PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anjelah Kairuki, ameahidi kutatua kero ya maji inayowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, ikiwemo Mpiji Magohe, Msigani na Mbezi Msumi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Mbezi, eneo la Mpiji Magohe jijini Dar es Salaam, Kairuki amesema kuwa upanuzi wa mtandao wa maji safi katika maeneo hayo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa kero ya maji.