Anglikana kutozika wasiohudhuria Ibada na Jumuiya

Anglikana kutozika wasiohudhuria Ibada na Jumuiya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam limeweka msimamo kuhusu utoaji huduma za kiroho kwa waumini wake, ambapo kuanzia sasa watakaohudumiwa ni wale wanaoshiriki ibada za jumuiya na kanisani.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Februari 11, 2023 wakati wa kikao cha Achidikonary ya Kibaha kilichofanyika mjini Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Huduma hizo ni pamoja na mazishi, ndoa kipaimara, ubatizo na hata maombi mbalimbali yanayoendana na imani ya dhehebu hilo.

Baba Askofu ameshasisitiza kuhusu hilo hivyo kuanzia sasa sisi wachungaji hatutahusika kutoa huduma hizo kwa waumini ambao watakiuka kanuni hizo," amesema Rogers Mshuza.

Mshuza ambaye ni Mchungaji kutoka Kanisa la Anglikana, Sofu Kibaha mkoani Pwani amesema kuwa hivi sasa baadhi ya waumini wamekuwa wakiyumba, leo yuko huku kesho yuko kule jambo ambalo linaweza kuleta mvutano hata kwa viongozi wa madhehebu mengine.

Kwa upande wake Kasisi kiongozi Kanisa Anglikana Kibaha, Exavia Mpambichile amesema kuwa utaratibu huo utasimamiwa na viongozi wa jumuiya kwani ndio wanaowatambua waumini wao.

"Sisi tutakuwa tunapokea taarifa kutoka kwa viongozi wa jumuiya ndio watakuwa wanatuletea ukweli pindi muumini anapofika kutaka kupata huduma yoyote ya kiroho kama ayasema hamtambui basi hatutahusika kwa lolote," amesema.

Amesema kuwa mipango iliyopo kwa sasa mbali na waumimi kusali pia wanaweka mikakati ya kuwepo miradi ya kiuchumi Ili kuwasaidia waumini.

Kwa upande wake, Hilaly Sagawala ameuomba uongozi wa Achidikonary hiyo kuwekeza elimu ya masuala ya kiuchumi kwa waumini wa Kanisa hilo ili waweze kutumia rasilimali mbalimbali kujikwamua kiuchumi.

My Take
Huu ni ukiristo gani. Wakirsto tumeanza kuhukumiana hapa hapa duniani? Hongereni Waislamu kwenye hili,mnamzika marehemu ataenda kujuana na Mungu wake huko akhera.
 
Kuzika sio jambo la kiroho , Yesu alisema muamini aliyelisikia neno lake hatokufa.Kiroho hakuna Huduma ya kuzikana maana mkristo hafi.
Hahahaha yesu mwenyewe alizikwa kulingana na mafundisho ya kikristo afu wewe hutaki watu wazikane maana mkristo hafi

Kimazingira kibailojia kuzika ni usafi we hujui kuwa maiti huwa mwenye kutoa harufu?

Sasa tuwafanye vipi maiti maana twawaona wakifa wakristo wakifa kila Leo au hao wanakuwa wakristo jina hawana imani sio?

Achana nahizo fikra mkuu uzuria kwenye misiba ya jamaa, ndugu, rafiki na jirani zako kadiri uwezavyo afu mambo mengine usimsingizie Yesu
 
Wakikataa kuzika wengine hujitokeza kuzika, kule Moshi nimehudhuria misiba ya ajabu ajabu marehemu kukataliwa kuzikwa na dhehebu lake kwa sababu hizi hizi. Wakati mwingine hutokea fujo na vurugu kwa kutaka kutoa kipigo kwa kiongozi wa dini anayekataa kufanya ibada ya mazishi.

Kuna wengine watamzika muumini wao mwenye makosa kama haya huku wakiyasema waziwazi makosa yake bila kumfichia aibu marehemu.

Waislam wakiona marehemu asuswa kuzikwa kwa taratibu za dini yake humzika wenyewe kiislam japo hawamfanyii mambo yote ya kiislam kwani hata wao wana kasumba ya kususiasusia baadhi ya taratibu za mazishi kwa muumini wao ambaye naye si mhudhuriaji sana wa vikao vyao.

Anyway, dini ni imani tu wazike kwa taratibu zao au wasizike maiti itazikwa tu na Mungu ataipokea na kuhukumu kwa haki
 
Anglican wamechelewa sana.

Huu mchezo RC wameanza muda mrefu sana.
 
Imetokea sintofahamu baada ya wachungaji wa kanisa la Anglican kutangaza kutowapa huduma ya kuzika, ndoa waumini wasiohudhuria Ibada kanisani/ jumuia

Je, hii ipo sawa?
 
Imetokea sintofahamu baada ya wachungaji wa kanisa la Anglican kutangaza kutowapa huduma ya kuzika,ndoa waumini wasiohudhuria Ibada kanisani/jumuia

Je hii ipo sawa?
Kukataa kusoma Biblia tena ilivyoandikwa kwa lugha yako Mama yaani kiswahili ni kukubali Kudanganywa [emoji1787][emoji1787][emoji1787] when you die, your soul tend to leave the body, taken somewhere else waiting for the judgement day!

Vipi kuhusu wanaofia majini au kuliwa na wanyama?

1676208054309.jpg
 
Africa tumemalizwa na hizi dini na zinatutia woga bila sababu
 
Yesu alishasema.

"acha wafu wazike wafu wao".

Kulilia kuzikwa na walio hai Ni uzwazwa
 
Back
Top Bottom