Maendeleo Kwanza1
Member
- Apr 4, 2020
- 16
- 7
ASKOFU wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Dk Stanley Hotay amesema Watanzania wana kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumpata Rais Dk John Magufuli aliyeruhusu ibada ziendelee wakati wa tishio la ugonjwa wa corona.
Aidha, amewataka waandishi wa habari nchini kutekeleza majukumu yao kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kuandika habari chanya za madhehebu ya dini nchini. Askofu Hotay alisema hayo jana jijini hapa wakati akiongoza ibada ya mazishi ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Eliya Mbonea (45).
Alisema homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid- 19) ni ugonjwa hatari usio na chanjo wala tiba, lakini anaamini utapita lakini wananchi wanatakiwa kumtumaini Mungu kwa kuwa ni hatari. Kuhusu Mbonea, Askofu Hotay alisema alikuwa mcheshi msikivu na aliyependa kumtumikia Mungu katika maisha yake yote. “Marehemu alikuwa muumini aliyependa kutumikia kanisa na wakati mwingine alijitoa kuwa dereva wangu ikiwa ni sehemu yake ya kumtumikia Mungu,” alieleza askofu huyo.
Akisoma wasifu wa Mbonea, kaka wa marehemu, Fanuel Hume alisema alizaliwa mwaka 1975 na alisoma Shule ya Msingi Kahama na baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Korongwe iliyopo Kahama, kabla ya kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times cha jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Zelothe Stephen alitoa pole kwa familia ya Mbonea na watu wote walioguswa na msiba huo. Marehemu alizikwa jana alasiri katika makaburi ya Njiro jijini hapa