Angola: Watu 22 wafariki na wengine 1124 wakamatwa kufuatia maandamano dhidi ya Serikali

Angola: Watu 22 wafariki na wengine 1124 wakamatwa kufuatia maandamano dhidi ya Serikali

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Takribani watu 22 wamefariki dunia katika maandamano yenye vurugu nchini Angola kufuatia ongezeko kubwa la bei ya mafuta, mamlaka zilisema Jumatano. Idadi hii ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na vifo vinne vilivyoripotiwa siku iliyotangulia.

Taarifa ya Ikulu ya Rais ilibainisha kuwa maandamano hayo yamesababisha vifo 22, majeruhi 197 na kukamatwa kwa watu 1,214. Aidha, maduka 66 na magari 25 yaliharibiwa huku maghala na maduka makubwa yakiporwa.

Maandamano hayo yalianza Jumatatu baada ya vyama vya madereva wa daladala kuanzisha mgomo wa siku tatu kupinga uamuzi wa serikali wa kuongeza bei ya dizeli kwa theluthi moja. Hatua hiyo inalenga kupunguza gharama kubwa za ruzuku na kuimarisha hali ya fedha za umma.

Hata hivyo, maandamano hayo yalisambaa haraka kutoka mji mkuu wa Luanda hadi mikoa mingine, yakigeuka kuwa vurugu zilizoambatana na mapambano makali kati ya waandamanaji na vyombo vya usalama pamoja na uporaji wa mali.

====================================

At least 22 people have been killed in violent protests across Angola following a sharp fuel price hike, authorities said Wednesday, marking a dramatic escalation from the previous day’s death toll of four. The unrest, triggered by the government’s decision to slash diesel subsidies, has led to widespread clashes, looting, and mass arrests, with tensions spreading from the capital, Luanda, to other provinces.

The protests began Monday after minibus taxi unions launched a three-day strike in response to the government’s move to raise diesel prices by one-third—a measure aimed at curbing costly subsidies and stabilizing public finances.

The demonstrations quickly turned violent, with reports of looting, vandalism, and deadly confrontations between protesters and police.

President João Lourenço’s cabinet held an emergency meeting Wednesday to assess the security crisis and coordinate law enforcement’s response.


Source: African News
 
Wakenya wengine waonekana pande za Kusini,mnaandamana vipi huku mnavunja maduka ya watu?Mnaharibu mali za watu?Hao ni wezi kama wezi wangine na hukumu yao ni kuwarestisha in peace tu wakawasalimie Babu zao.
 
Back
Top Bottom