Anguko la Bashe ni ruzuku ya Mbolea

Anguko la Bashe ni ruzuku ya Mbolea

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Wabunge wanaendelea kujadili ripoti ya CAG Bungeni wabunge wengi wmeonekana kulalamikia ubabaishaji mkubwa uliopo kwenye mfumo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea huku wengi wakidai utaratibu huo unawanufaisha matajiri huku wakulima wakiendelea kulia.

Mbunge Condescha Sichalwe na Vita Kawawa wamelalamikia wakulima wengi kutofikiwa na mbolea ya ruzuku huku Serikali ikiwa imeshatoa Bilioni 150 kwa ajili ya kugawa mbolea ya Ruzuku.

Hali ikoje kwa wakulima kuhusu mbolea ambayo inaonekana ndio machinjio ya Waziri Bashe na hata alipotoa taarifa yake bungeni kwa Mbunge Vita, Spika Tulia akaikataa na kutaka wakulima wafikiwe na mbolea kama malengo ya Serikali
 
Nchi ya ajabu sana hii. Hakuna chochote kinachofaulu. Nimeamini, Tanzania yahitaji dikteta mzalendo kama Magufuli kwa muda wa miaka hamsini ijayo, kabla tabia kubadilika. Vinginevyo, hatutoboi.
 
Wakiwa wanaongea unaweza dhani watu wa maana kweli, kumbe ovyo kweli.

Hizo mbolea zitawafikia wakulima saa ngapi wakati majizi wanajipimia tu za kwenda kuuza kwingine.

Hawa ni watu wanaoropoka tu lakini hawana mikakati ya porojo zao.
 
Wakulima hawafikiwi kwa kuwa waagizaji wako mijini .Agrodelear hawapata nafasi ya kuuza mbolea hizo .na kamtaji kadogo sisi tununue cash.pamoja nae ruzuku ya serikali itakalipwa na serikali tuwalipie.tubaki tukidai kwao.haifai kwanini wao wasisubirie kudai serikalini.
 
Mkuuu umesema kweli mie ni muhanga wa biashara hyo naogopa hata kuifanya naogopa kuweka pesa yangu
 
Niliwahi kukueleza bashe kuwa hili la mbolea Kuna utaratibu walikosea kuuweka
 
Ila kwenye issue ya vibali ya mazao yanayo kwenda nje ya nchi ni pekee ndio anayepambana.
Namfikiria angekuwa waziri wa viwanda na biashara,anajua takwimu muhimu kwa nchi zinapatikana vipi.sasa mbolea mkulima anasubiria shambani kitu ambacho hata Nqyerere alishindwa.
 
Anguko kuu ni kuagiza chakula nje ya nchi baada ya Serikali kutoweka mipango sahihi kuhusu swala la chakula .
 
Mbolea inatesa watu, inatesa watu, inatesa sanaaaaa. Foleni ni kubwa na watu wanapotezewa mudaaa..
 
Wabunge wanaendelea kujadili ripoti ya CAG Bungeni wabunge wengi wmeonekana kulalamikia ubabaishaji mkubwa uliopo kwenye mfumo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea huku wengi wakidai utaratibu huo unawanufaisha matajiri huku wakulima wakiendelea kulia.

Mbunge Condescha Sichalwe na Vita Kawawa wamelalamikia wakulima wengi kutofikiwa na mbolea ya ruzuku huku Serikali ikiwa imeshatoa Bilioni 150 kwa ajili ya kugawa mbolea ya Ruzuku.

Hali ikoje kwa wakulima kuhusu mbolea ambayo inaonekana ndio machinjio ya Waziri Bashe na hata alipotoa taarifa yake bungeni kwa Mbunge Vita, Spika Tulia akaikataa na kutaka wakulima wafikiwe na mbolea kama malengo ya Serikali
Bashe alikuwa na mpango mzuri, lakini alichosahau ni kitu kimoja cha msingi sana na viongozi wetu wanategemea sana mipango ya makaratasi kuliko uhalisia

Hii Tanzania ni nchi kubwa sana kijografia, fedha za ruzuku ni vigumu kutoka kwa wakati kwasababu ya michakato ya taratibu za kiserikali na penye hela lazima wajanja watataka kupenya tu.

Haya na mengineyo yanaweka ugumu sana kuwafikia wakulima wote kwa wakati hasa ukizingatia kilimo kinaenda na msimu

Mkulima akichelewa msimu wa kilimo kwasababu ya kusubiri mbolea lawama zote zitarudi kwako tu. Hiki ndicho kilichomfelisha
 
Wabunge wanaendelea kujadili ripoti ya CAG Bungeni wabunge wengi wmeonekana kulalamikia ubabaishaji mkubwa uliopo kwenye mfumo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea huku wengi wakidai utaratibu huo unawanufaisha matajiri huku wakulima wakiendelea kulia.

Mbunge Condescha Sichalwe na Vita Kawawa wamelalamikia wakulima wengi kutofikiwa na mbolea ya ruzuku huku Serikali ikiwa imeshatoa Bilioni 150 kwa ajili ya kugawa mbolea ya Ruzuku.

Hali ikoje kwa wakulima kuhusu mbolea ambayo inaonekana ndio machinjio ya Waziri Bashe na hata alipotoa taarifa yake bungeni kwa Mbunge Vita, Spika Tulia akaikataa na kutaka wakulima wafikiwe na mbolea kama malengo ya Serikali
Hili kwa kweli ndio kaburi lake kisiasa
 
Bashe hajawahi kufaulu kwa lolote. Amezidisha uongo na masifa.
Kilimo cha vijana kujiajiri kiko wapi? Mbolea ya ruzuku iko wapi. Chakula kimepanda bei kwa ujinga wake. Ana wapelekea Wasomali wenzake wasife njaa kwa kuwatesa Watanzania. Bado ana tukejeli.
 
Back
Top Bottom