Anguko la Diamond ni sawa na "Mr nice"

Diamond aanguke kama mr nice kwa lipi mkuu
 
Bora umeongea wewe hii KOKORO hata sijaielewa yaani naona staili ya Wasafi ni ile ile tu, ukiangalia Mugachere, Kokoro........

Ngoja tuwaachie wenye Team zao bhana
 
Mkuu kweli nitasubiri sana maana KWENYE UDHIA PENYEZA RUPIA na kuhusu hilo wcb wako vizuri kwa hiyo sitoshangaa kuona hii nyimbo inaachwa tu iendelee kuonekana kwenye jamii lkn ukweli utabaki palepale kwamba haipaswi kuonyeshwa kwa tv za bongo
 
Kitu kimoja ambacho watu hawajaelewa kuhusu diamond ni kwamba jamaa anajua kuucheza mchezo...kucheza na akili za watu..naomba mtoa mada usubir miezi kadhaa utaleta feedback hapa...
 
hakuna ajuae kesho mkuu wala hakuna anaemuombea diamond anguko nampenda diamond sana mimi binafsi ila trend yake haipo sawa kama zamani au wewe unasemaje?
Nikiangalia mtazamo wako kwa diamond nadhani una lean kuto mpenda( may be ulimpenda zamani its ok)

Mimi namkubali, na nakubali akosolewe kwa nia njema, nyimbo ya Ne-yo ndio ilinistua ilikiwa chini ya matarajio yangu, ila kwengine naona ako sawa, akipotoka ntasema.
 
Ila hii video mmmh mmmh mmmh, nahisi itapigwa chini, sasa sijui nani aliitoa idea ya wale madada kuweka viplasta vya x kwenye chuchu, ila hii nyimbo nilitarajia makubwa kutoka kwao ila naipa 7/10 ila video hiiiiiiiii.................... Tusubiri tuone itakuwaje, ila nimemuona fundi mitambo kufanya yake, ktk hii video kama kule mombasa 😛😛😛. Nakuhusu diamond platnumz kushuka sitegemei, sitarajii kama hatashuka kwa Muda huu, kwani huu ni muda wake, ww endelea kupiga ramli, choma ubani lkn ni wakati wake, maneno haya toka 2014 mpaka hivi leo yashazunguzwa sana lkn bado namba moja, najua muda wake wakushuka utafika ila sio sasa na usitegemee atatetereka kiuchumi, muundo na mfumo wakikampuni aliojijengea diamond platnumz ndio utakaomuingizia ela mpaka anakufa kama alivyo AY.
 
Mkuu umeandika assumption tu.. Au ndoto ya mchana..
Am not team Diamond.. Wala c shabiki wa Diamond but I respect akili yake ya biashara kimuziki..
Ukikosoa Siku nyingine njoo na fact.. Na statistics pamoja na mifano ya kutosha..
Nyimbo mbaya.. Hujataja hata moja...
Wasikilizaji wa audio vs watazamaji wa video.. Tupe numbers.. Ama takwimu.. Ukishindwa hata makadirio..
And last.. Uckarir mambo.
 
Lazma tukubali diamond ni mwanamziki mzuri lkn kuna haya ya kufanyia kazi kwenye hizi nyimbo mbili ya neyo na mavoko.
1. Uandishi apunguze kurudiarudia maneno na idea mfano wimbo wa neyo na ule kwenye video yuko na Avril. Zote idea nataka nikuoe nikupeleke nyumbani.
2. Beat na melody ziko kinaigeria sana anakosa identity sababu style za wanaigeria wako wengi sana.
3. Producer anagonga beat zinafanana sana at least awe nao zaidi ya wawili kutofautisha ladha.
4. Staha za video. Sidhani km hawakufikilia basata watawamind. Kuwaweka wadada kwenye mabeseni maziwa nje nikuwazalilisha wanawake na ninje ya utaratibu wetu.

Sio lazma ashindwe hatumuombei lkn akubali critcizm zenye kujenga.
Kuhusu kushuka kimuzik hakuna mtu aliyeishi milele au kuhit milele unawasahau kina defao, kina pepekale kina kofii kina Michael Jackson kila mtu anazama zake hizi nizama za Diamond lkn azingetie ushauri.
All in all Nyimbo hizi hazina kipya hata hazifikii kina INDe,
Lkn Najua Clouds wapo na hizi nyimbo zitakuwa kubwa regadless na uzuri au ubaya wake.
 
Tatizo ni lugha tu wadau.....
Ngoma zote, za mond sehemu anazotumia lugha nje ya kiswahili inaonekana mashairi kapuyanga.
Vionjo kubadilika cjui kama tekno,ngoma haina ladha ya ki-tz, hiyo ni ''marketing target'' wanawaza mangoma yatakayohit abroad ili wakapige show za bei mbaya.
TRUST ME MYFRIEND AND TIME WILL TELL US THIS SONG WILL GIVE RICH MAVOKO MORE INTERNATIONAL STANDARDS
 
Wimbo wa rich mavoko ni mzuri ila diamond ndo amefanya uwe wa kawaida!. Ameimba kwa mazoea na hakuna kupya alichofanya kwenye huo Wimbo! . Kwa lugha nyepesi Rich Mavoko amemfunika boss wake.bora rich angefanya mwenyewe.
Diamond na alikiba style zao hazibadiliki ivyo wanakuwa wabazoeleka masikioni hata wakitoa Wimbo huusikii km mpya.mfn Wimbo wa alikiba na ommy dimpos ni Wimbo Mzur ila style ya alikiba Ile ile.jike shupa Wimbo Mzur ila style Ile ile. ..soon utakuta hawa alikiba na diamond ndo wanabebwa na collabo.
Wimbo wa mwisho mzuri alikiba kutoa ni ule naghalamia na Christian Bella,Wimbo wa mwisho diamond kutoa mzuri ni let me sing na AKA wa S.a
 
Kateleza kidogo blaza ila sehem ya mfano wako haukufanyi Akili nyingi
 
Hizi wahenga wanaita dua za kuku kamwe haziwezi mpata mwewe...na watu wanasahau kadri mnavyo muombea mabaya ndivyo Sir God anavyozidi kum'bariki...Muda wake wa kushuka utafika ila sio sasa,na maneno mnayo muombea yanamfanya akomae zaidi kwenye game...km kweli mnataka ashuke ni bora mkae kimya ajisahau ashuke mwenyewe,mnachokifanya ss ni sawa na kumshtua shtua mtu anaetaka kulala...atakaza jicho balaaa na mwisho wa siku utalala ww unae mwamsha..ila all in all hii Ngoma ya rich mavoko itampeleka rich kimataifa wakapige dolari..na nnadhani target yao ni huko sio vituo vya runinga vya kibongo...
 
Huko kimataifa amefika ukingoni kwakuwa ameanza kuwacopy hao wa kimataifa.
Ukimcopy mtu utaweza kushindana naye kwenye soko moja?
 
Kila nyimbo ya diamond ikitokaga..utabiri huu unakuepogo..subiri tu utaona..time will tell
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…