Ndugu, wadau, nilitoa uzi hapo juu ili kupata ufafanuzi wa kichumi zaidi, lakini bahati mbaya naona watalaamu wapo kimya tu..
Anyway, kwa kutumia knowledge yangu ya ARU pale Darusalaam main campus katika moja ya kozi niliyo kuwa nachukua, economics pia nilisoma
Mjadala ulikuwa wazi,
By reference kwa Jamaa JPM (marehemu), dhahabu ilipanda kupindukia zaidi kiasi kwamba hata sisi wafanya biashara wa chini kqbisa tulifanikiwa kupata fedha ambazo hakuna biashara nyingine una weza kuilingqnisha nq dhahabu ya Tz.
Ikumbukwe kuwa Tz ni moja ya nchi mzalishaji mkubwa wa dhahabu duniani ikiwa na caratage ya daraja la juu sana, yaani (24k, 23k, 22k, na rarely 21k), hivyo Tz ni moja ya supplier mkubwa wa dhahabu duniani ikitanguliwa na nchi za DRC, South Africa kwa bara la Africa.
Sasa tukirejea enzi za utawala wa Magufuli kulitokea mgogoro uliosanuliwa na Mwamba mmoja anaitwa TAL, baada ya late presidaa Magufuli kuingilia kati harakati za madini na wawekezaji wa Madini (BARICK, GGM n.k) ambapo TAL aligeuka kuwa wakili wa hawa mabepari kutetea maslahi yao kisheria kama nguli wa Sheria Tz.
Mgogoro huu uliitwa usafirishaji wa makinikia ambapo ilibainika haukuwa mchanga mtupu bali na madini ndani yake.
TAL alidai na kuiambia serikali ya Magufuli endapo itaingilia mikataba walio ifunga ba kusaini kwa mikataba ya madini duniani, serikali ingeweza kushtakiwa MIGA kwa kuvunja mkataba kinyume cha makubaliano.
Magufuli alikaza kamba kana kwamba hakujali kabisa madhara yoyote ambayo yangeweza kutokea endapo angefeli mkakati wake kuizuia dhahabu isiendelee kuchukuliwa na mabepari haya.
Tulishuhudia sote dege la binafsi (private jet) la boss wa BARRICK bwana Tomson likitua pale JNIA kumfata mwamba wayamalize( dah! Alikuwa mwamba kweli na chuma wa misimamo kama talbani hivi)
Ikumbukwe kuwa kipindi hicho chote cha mgogoro, migodi kama ya BULYANHULU kahama, North Mara musoma ilisimama ualishaji hivyo kuathiri upatikanaji wa dhahabu ya Tz kwenye soko la Mabepari.
Kukosekana kwa dhahabu hii soko la dunia kuliifanya bei kupanda sana kwa sababu ilikuwa adimu tena sokoni, matajiri wakawa wanaipandilia bei ili angalau waipate hata magendo tu, maana haikuwa nyingi sojoni
Hivyo wachumi waka sema kuwa
Ikiwa upatikanaji wa bidhaa ukiwa mdogo mara nyingi uhitaji wa bidhaa hiyo kwa watu huwa mkubwa, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei yake sokoni yaani ( THE LOW THE SUPPLY~THE HIGH THE DEMAND=THE HIGH THE PRICE) vile vile, ikiwa upatikanaji wa bidhaa ni mkubwa mara nyingi uhitaji wa bidhaa hiyo huwa mdogo, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa bei yake (THE HIGH THE SUPPLY THE LOW THE DEMAND=THE LOW THE PRICE)
Sasa kwa wale tunao ishi katika maeneo ya uwekezaji wa dhahabu yaani Bulyanhulu na North Mara kwa mfano, tunaweza kuwa mashuhuda kuwa, kipindi cha Mwamba, ndege za kubeba mizigo ya dhahabu kutoka ubeparini zilipungua sana kupelekea hata viwanja vyao vya kutua kuota majani kutokana na kutokutumika kwa mda mrefu bila ndege kutua viwanjani humo,
Baada ya mwamba kufariki na usukani kupokelewa na MGAWA ASALI,, viwanja hivi vilifufuliwa kwa kasi sana ikiwa ni pamoja na kufyekwa majani na ukarabati mwingine wa kimiundo mbinu ili kurahisisha utuaji wa ndege hizi kubeba matofali ya dhahabu kutoka Tz nchi ya WAGAWA ASALI.
Binafsi nakaa kakola ambako BARICK amewekeza, ndege nadhani inatua mara mbili ama mara tatu kwa wiki ikipakia matofali ya dhahabu kwenda ulaya na nabaki nakodoa tu macho juu huku ikienda kweli dah!
Hivyo upatikanaji wa dhahabu ya Tz kwenye soko la dunia ni nyingi sana kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha Hayati Magufuli, na kuporomoka kwa bei tusishangae sana.
Nawasilisha...
By Epafra Clement, Jobless choka mbaya sana kutoka mitaa ya Bulyanhulu kakola