Anguko la Syria litafungua njia kwa anguko la tawala za Kishia Mashariki ya Kati

Anguko la Syria litafungua njia kwa anguko la tawala za Kishia Mashariki ya Kati

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Homs tayari imeanguka mikononi mwa waasi

Damascus ipo matatani

Wakurd jana nao wameteka mji wa mashariki mwa Syria na kuzuia jeshi la Iraq na Iran kutoa msaada wa silaha na kijeshi kwa Assad

Homs
Wanamgambo wa Hayat Tahrir al-Sham (HTS) muda huu wapo Homs, wakishika maeneo muhimu ya mji. Wamefungua mamia ya wafungwa wote waliofungwa na serikali ya Assad ambayo imetawala Syria kwa miaka 54. Kwanza ni maajabu makubwa sana kwa kinachotokea Syria. Yaani ndani ya wiki mbili tu jeshi la Syria limeshindwa mbele ya waasi hata wasio na ndege, helkopta, vifaru nk. Wakiwa na landcruzer, Alphard, na virukuu na pikipiki wamefanikiwa kuteka karibu zana zote za Syria alizopewa/kununua kutoka Urusi na Iran. Hivyo Assad anapigwa na silaha zake mwenyewe huku wanajeshi wake wengi wameweka silaha chini na kuvaa kiraia na wengine 2000 wamekimbilia Iraq. Swali nani anawapa waasi intelijensia? maana hawabahatishi.

Damascus
Sasa HTS wapo kwenye lango la kusini la mji wa Damascus kwa 20km. Wameshatwaa miji iliyo kando kando yake huku wakiungwa mkono na maandamano ya raia ambao wanaondoa mabango ya picha na sanamu za Bashar na baba yake. Kweli Assad kaçhokwa. Mkuu wa majeshi wa Syria amekanusha kuingia kwa waasi katika mji huo na akidai watashindwa vibaya mno. Lakini nchi za Kiarabu kama Jordan, Misri, Qatar nk badala ya kumwokoa zimemuambia Assad aondoke Syria kwabusalama wake na kuzuia Syria isiharibike zaidi. Kwa kweli huku ni kushindwa kukubwa kwa Assad.

Wakurd
Juzi Wakurdi wa Syria wanaoungwa mkono na Marekani wameuteka mji wa mashariki mwa Syria wa Deir Ezzor, duru mbili za usalama zimeiambia Reuters. "Vikosi vya Syria na washirika wao wanaoungwa mkono na Iran walijiondoa kabisa katika maeneo wanayodhibiti katika jimbo la Deir Ezzor na vikosi vya Wakurdi vinasonga mbele kuelekea maeneo yao," anasema Rami Abdel Rahman, anayeongoza Shirika la Kuchunguza Haki za Kibinadamu la Syria.

Mkoa wa deir Ezzor umegawanyika kati ya vikosi vya Wakurdi vilivyoko mashariki mwa Euphrates na vikosi vya serikali ya Syria vinavyoungwa mkono na Iran na washirika wake upande wa magharibi. Kando ya Deir Ezzor, gazeti la habari la Suadi Alhadath linaripoti kwamba waasi wa Syria pia wamechukua udhibiti wa Albukamal kwenye mpaka wa Syria na Iraq, na hivyo kukata vyema njia ya ardhini ya usambazaji wa zana na jeshi kutoka Iran hadi Lebanon kupitia Iraq na Syria.

Hivyo hadi hapa tunaona Assad anguko lake ni kamili. Na haya yote yanakuwa ni faida kwa Israeli ambayo leo imeshambulia ngome za Hezbollah huko kusini mwa Lebanon. Hivyo kama Assad akianguka basi Iran kamwe haitaweza kusambaza silaha, zana na jeshi kwa Hezbollah iliyodhoofishwa na Israeli. Hivyo anguko la Hezbollah litakuwa hakika huko Lebanoni.

Washirika wa Assad
Washirika muhimu wa Assad ambao ni Urusi, Iran na Hezbollah wamepishana mtazamo. Iran na Hezbollah wakiwa na nia ya dhati ya kumsaidia Assad wakionesha hatua hiyo kwa kupeleka majeshi yao, lakini Urusi ameishia kuondoa raia wake wote na kuondoa meli zake katika bandari ya Syria. Sahivi waziri wa mambo ya nje wa Urusi yupo Doha na waziri wa mambo ya nje wa Iran na Uturuki wakizungumza hatma ya Syria. Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi anasema Moscow itafanya kila kitu ili kutoruhusu magaidi kutawala lakini waasi wa Syria wakizidi kuendelea mbele kwa kasi. Ni kweli Moscow imejitahidi kufanya mashambulizi ya anga toka waasi wakiwa Allepo lakini mashambulizi hayo hayakuwazua waasi kuuchukua mji wa Allepo na kusonga mbele katika mji wa Hama na kuutwaa mnamo juzi. Na jana saa tano usiku wameutwaa mji wa Homs hali kadhalika wamekabiliwa na mashambulizi ya anga ya Mrusi. Sasa wanaelekea kuuchukua Damascus. Mashambulizi ya anga kamwe hayawezi teka nchi.

Wachezaji wa mchezo huu
Ingawa Marekani, Uturiki na Israeli wàlilitangaza kundi la HTS kuwa la kigaidi ingawa HTS wamejiosha sana kimataifa ili wakubalike kama chama cha mlengo wa kisiasa safi lakini bado msimamo wa mataifa hayo upo pale pale. Lakini ukizama chini sana utaona kuwa mchezo huu wote unachezwa na Uturuki, Marekani, na Israeli, na Saudia nk. Hivyo mashambulizi ya Israeli kwa Hezbollah na kuua uongozi wake wa juu ni moja ya ajenda ya mchezo huu. Mchezo huo wa Israeli ulifanikiwa kuisogeza karibu Iran, jambo ambalo walilitaka, hivyo Iran ikawa bize na Israeli na kuisahau Syria hivyo nafasi ikapatikana ya kuangua mayai ya waasi wa Siria walitoka kama nzige na kuuvamia utawala wa Assad. Assad pia aliwekwa bize na mashambulizi ya Israeli kwenye kambi zake pamoja na uvamizi wa Uturuki. Hivyo Assad amejikuta kambi zake za kijeshi zimevurugwa.

Iran nayo ikazubaishwa kwa majibizano na Israeli. Kwa kweli Iran iliondolewa meno kwa shambulizi la Israeli ingawa ilijaribu kuficha lakini vita vya Siria vimeiumbua. Iran imeshindwa kusambaza silaha kwa Assad na Hezbollah maana Israeli ililipua mitambo yake ya kuunda makombora. Kwa upande wa Urusi ambaye ndiye tegemeo kuu la Assad, ameshindwa kumsaidia ndugu yake sababu naye Ukraine imemweka bize. Inajulikana mwaka jana Urusi alipunguza 80% ya wanajeshi wake na zana huko Syria kwajili ya vita vya Ukraine, hivyo ni kama hana jeshi hapo Syria. Na sasa hana uwezo wa kipesa na silaha za kuendesha vita mbili kwa mpigo maana pia naye anasaidiwa wanajeshi na zana toka Korea kaskazini.

Hivyo naona anguko la Syria litafungua njia kwa anguko la tawala za kishia mashariki ya kati. Hivyo Iran yupo katika lengo la kuangushwa, na huyo ndio mlengwa mkuu. Na Trump ameahidi kula naye sahani moja.

Anyway zaidi tusubiri
 
UTAWALA WA FAMILIA YA ASSAD WA MIAKA 54 UMEANGUKA

Damascus mji mkuu wa Syria sasa upo mikononi mwa waasi.

Wapiganaji wa upinzani tayari wameshika miji mikubwa minne ya Syria ambayo ni Allepo, Hama, Homs na Damascus, hii miji ilikuwa chini ya ulinzi na uangalizi wa Urusi na Iran toka 2014. Assad kakimbilia urusi

Majeshi ya Iran yaliyokuja kumsaidia Assad yameshindwa vibaya mbele ya wanamgambo hawa. Na katika mazingira yasiyo elezeka Urusi aliye mshirika muhimu wa Assad naye alifungasha virago mapema na kutoa wanajeshi, meli zake na raia wake wote Syria. Ingawa ilijaribu kufanya mashambulizi ya anga lakini ndio hivyo tena, wameshindwa. Hezbollah sasa ipo matatani, Israeli wameanza kuishambulia tena.
 
Back
Top Bottom