TANZIA Anna Elisha Mghwira afariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Mount Meru

TANZIA Anna Elisha Mghwira afariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Mount Meru

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Aliyekuwa mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira amefariki dunia leo July 22, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha. Mama Mgwira alistaafu ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mei mwaka huu na alikabidhi ofisi kwa mrithi wake, Kigaigai Mei 27 mwaka huu wa 2021

Anna Mghwira ni mwanachama wa JamiForums tangu mwaka 2012

====

UPDATES:

====
Anna Mgwira.jpg

Anna Elisha Mghwira (alizaliwa 23 Januari 1959) ni mwanasiasa. Alikuwa Mwenyekiti wa Alliance for Change and Transparency (ACT) aliyegombea urais wa nchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, alihamia chama cha CCM mwaka 2017.

Maisha ya awali na elimu

Anna Elisha Mghwira alizaliwa tarehe 23 Januari 1959 katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, Kata ya Mungumaji - Kitongoji cha Irao katika Manispaa ya Singida-Mjini. Alikuwa mtoto wa nyumbani kwa sababu ya shida ya kiafya ambayo ilichelewesha uwezo wake wa kutembea.

Alijiunga na shule ya msingi ya Nyerere katika miaka ya 1968- 1974. Kisha akasoma shule ya Sekondari Ihanja kutoka 1975 hadi 1978 kabla ya kujiunga na Seminari ya Kilutheri kwa masomo ya A-level 1979 hadi 1981.

Alipata shahada yake ya kwanza katika theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipoongeza shahada ya sheria (LLB) mnamo 1986. Kwenye Chuo Kikuu cha Essex huko Uingereza aliendelea kusoma shahada ya uzamili ya sheria (LLM) mnamo 2000.

Mghwira alifanya kazi kwa mashirika ya kimataifa na ya Kitanzania yanayoshughulikia uwezeshaji wanawake, maendeleo ya jamii na wakimbizi.

Baba yake alikuwa diwani kupitia TANU. Anna alijiunga na umoja wa vijana wa chama cha TANU. Katika miaka ya 1970 alipunguza kazi yake ya kisiasa ili aweze kuzingatia masomo yake na familia.

Mnamo 2009 alirudi katika siasa alipojiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Bi Mghwira alishikilia nyadhifa tofauti kama katibu wa wilaya wa chama na baadaye mwenyekiti wa wilaya wa chama.

Mnamo mwaka wa 2012, alishindwa na Joshua Nassari katika uteuzi wa Chadema kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki. Alifanikiwa kugombea kiti cha Bunge la Afrika Mashariki mwaka huo huo, lakini bila kuchaguliwa.

1626948796806.png
Mnamo Machi 2015, alihama Chadema kwenda chama kipya cha ACT-Wazalendo, ambapo baadaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kitaifa wa chama wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa chama. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aligombea urais wa Tanzania.

Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akaacha ACT-Wazalendo akahamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
 
Sad news. Mama Anna Nghwira-EX RC KLM amefariki katika Hospitali ya Mount Meru leo majira ya saa 5asb alilazwa hapo akitibiwa kwa takribani wiki moja.
Real Sad!
 
BREAKING NEWS: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha, ndugu wa familia wamethibitisha.
 
So sad, kuna mtu naona kwenye whatsapp group alipost taarifa kama hizo pia

Poleni sana Fadhili kwa kumpoteza mama
 
😢😢😢
So Sad, Mungu akupe pumziko la milele.
Warumi 14:8-10
[8]Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
[9]Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
[10]Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
FB_IMG_16242121100003267.jpg
 
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospital ya maunt meru
 
Back
Top Bottom