MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
Ukijengewa jungu na wewe pika lako it is the survival of the jungle.
Wanajamii, kama kuna mtu anamfahamu Anne Kilango au watu wake wa karibu, basi wamshauri asome (kama hajawahi kusoma) the damned book "Lo Prince" by Machiavelli ili ajuwe siri ya politik! That book gave the politcian an advice about what he/she should do to persevere and to promote in his/her position badala ya kulialia. Alitakiwa kujua by now kwamba politiks is a dirty game. There is no definite rules. Siasa ni kama ile PRO-WRESTLING ya zamani (late 80s); you can use everything near you: kick, punch, slap, na ukiweza ua kabisa.
Laiti kama hayawezi haya, basi jibu lake ni rahisi; leave the dirty game to the dirty players and stop crying!:A S 20:
Wananchi wa Same wasipomchagua(kama ni kweli hajawafanyia chochote)basi wananchi hao hawana haki ya uduma ya uongozi wa mama huyo and vice versa.
Bubu;Tuko all the way pamoja....Isipokuwa tuliwaambia toka nyakati zile especially mama alipodai "Hapatakalika" "Patachimbika" nk...Tulisema ondokeni humo nyie mnaojiita wapiganaji,naona bado wanabisha,sasa kama hoja zao dhidi ya ufisadi ni kwenda kinyume na matakwa ya chama watamlaumu nani zaidi yao wenyewe?Tunasikia ccj hivi wapiganaji vile lakini hakuna action.Mkuu Mafisadi bado wameshika hatamu ndani ya CCM na Serikalini hivyo watafanya kila wawezalo na kwa kutumia mabilioni yao ya kifisadi kupambana na wabaya wao na kuhakikisha hawarudi tena Bungeni baada ya uchaguzi. Bongo bila ufisadi inawezekana, mimi nakataa kauli hii umefisadi umeota mizizi kila pembe na vigumu mno kuushinda.
Hivi kwa nini baadhi ya wana JF wanajifanya wanademokrasia lakini hapo hapo itokeapo mgombea pendwa anapata mpinzani tayari huyo mpinzani atahusishwa na ufisadi??? acheni kudharau wapiga kura kwani wao ndiyo wanaejuwa nani anafaa katika mazingira yao [It up to the voters to decide] Kabla ya mama huyu kulikuwa na mbunge mbona alivyobwagwa hakupiga kelele kama hizo?????kweli nguvu ya mafisadi imeonekana jimbo Same mashariki, na ukiona Mama Ana kilango analalamika kiasi kile bungeni basi AMINI ni masikitiko kutoka moyoni kwake....hali yake jimboni ni mbaya sana na hata watu wake wa karibu wamemshauri hali ni ngumu sana, fitina zilizopandwa ndani ya jimbo na pesa zilizomwaga basi zimefanya hata wale wananchi waliokuwa wakimpenda kujenga chuki nae.....
Utafiti uliofanywa unaonyesha Mama Ana kilango huenda asirudi tena bungeni kwani upinzani ni mkubwa ssana, na kutokana na muda muwa mfupi kazi itakuwa kubwa kubadilisha matokeo....
Wanaomhujumu mgombea ubunge wa CCM Same waonywa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya same, Bw. August Kessy amesema kuanzia sasa viongozi wa ngazi zote wanaomhujumu mgombea Ubunge wa Jimbo la same Mashariki kupitia Chama hicho, Bi. Anne Kilango, wataondolewa.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Kambene Kata ya Miamba Bw. Kessy alisema kuna viongozi ambao wamekuwa mwiba mkali kwa kampeni hizo, kutokana na kuchochea uasi.
Bw. Kessy alisema kutokana na hali ya kampeni kudorora katika Kata nyingi, ameamua kupeleka taarifa mkoani, kuelezea tatizo hilo.
Nimeshapeleka taarifa mkoani wameniruhusu kumuondoa kiongozi yoyote, ambaye ataleta vurugu na mgawanyiko wa kichama wakati wa kampeni, hata kama kiogozi huyo anaondolewa na vikao kwa mujibu wa katiba, lakini mimi nitamuondoa kwa muda hadi kampeni zimalizike, ndipo vikao vikae, sasa hivi hatuna muda,alisema Mwenyekiti huyo.
Alisisitiza kwamba viongozi hao, ni wale ambao hawakufarahishwa na mgombea ubunge aliyeteuliwa na CCM.
Alisema viongozi hao pamoja na wananchi, wamekuwa wakisusia mikutano ya kampeni ya mgombea huyo wa CCM.
Jamani kura za maoni sasa hivi ni historia, lakini kwa Jimbo la Same Mashariki, bado kura za maoni ni tatizo. Matokeo yake yamesababisha kudorora kampeni zetu bila sababu za msingi,alisema Bw. Kessy.
Mwenyekiti huyo, alitoa karipio hilo, baada ya kupita kwa maandamano na kukuta bendera za CCM zinapeperushwa nusu mlingoni, kama ishara ya maombolezo.
Alisema kwa vyovyote hatua hiyo, ina mkono wa viongozi, jambo ambalo lilipingwa vikali kwa kiapo na Mweneykiti wa Kata hiyo Bw. Pagu Mkulu.
Tangu kuanza kwa kampeni za mgombea huyo, wananchi wamekuwa wakisusia mikutano yake, kuzomea na kurusha mawe kwa sababu zinazoelezwa kwamba chanzo chake ni kura za maoni, ambapo mgombea anayekubalika na wananchi wengi Bi. Naggy Kaboyoka alitemwa.
Hata hivyo, Bw. Kessy alisema hata kama wananchi hawampendi Bi. Kilango ni vema wakaja kumsikiliza, badala ya kususia mikutano yake.
Pale Mjema na Bombo Kata nzima walikuja watu saba kwenye mkutano, hapa kuna tatizo, pia kuna kukosa uungwana kwa viongozi na wanachama wa CCM,alisema.