Abunuwasi,
ni kawaida ya anna kilango kutoa matamshi ya vitisho, kwa wanaomfahamu wala hawashangazwi na kauli za hivi karibuni. kama anna kilango ametishiwa kuuwawa kama anavyodai, kwanini haendi kushtaki polisi, badala yake anakwenda kushitaki kwa yussufu makamba? anna kilango alitumia mbinu chafu katika uchaguzi wa 2005, kwa kuanza kampeni za ubunge tangu mwaka 2000, na pia kumwaga fedha wakati wa kura za maoni za maoni na uchaguzi mkuu.
kinachomtatiza anna kilango sasa hivi ni rekodi yake kama mbunge wa same mashariki. anna kilango ameshindwa kufuatilia ahadi ya raisi ya kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya mkomazi-ndungu-same. jimbo la same mashariki, na wilaya ya same, imeendelea kushika mkia mkoani kilimanjaro katika mitihani ya kitaifa na juhudi za mbunge katika suala la elimu hazionekani. kuna ufisadi wa kutisha katika uvunaji holela wa miti, na uharibifu wa vyanzo vya maji ktk jimbo la same mashariki, lakini mbunge haonyeshi kukerwa na ufisadi huo.
kazi aliyoifanya anna kilango ni ndogo na hairidhishi. ukweli huo ndiyo unaosababisha akabiliwe na upinzani jimboni kwake.tayari amejitokeza naghenjwa kaboyoka "mama maendeleo" na dr.michael kadeghe kumpinga katika kura za maoni za ccm.
soma jinsi hali ilivyokuwa tete mwaka 2005 baada ya anna kilango kumfanyia mchezo mchafu naghenjwa kaboyoka. wananchi walikuwa wanapeperusha bendera za ccm nusu mlingoti!!