Mkuu, huu uzi ni maalumu na wenye maudhui tofauti na ulichokiwasilisha, hapa tunaangalia ni namna gani kama jamii tunaweza kuunganisha nguvu kuwachangia vijana wetu/wenzetu wanaojiunga na elimu ya juu lakini wananshindwa kumudu gharama za masomo hayo. Tunatambua jitihada za serikali katika hili, lakini mahitaji ni makubwa mno kuliko uwezo wa bodi ya mikopo kwa sasa, kama wadau wa elimu na wana jamii huwa tunakutana kwenye uzi hii kuona nini tunaweza tukafanya ili ama kupunguza au kuondosha kadhia hii kwa wanafunzi wetu.
Jambo lako ni muhimu sana, bila shaka sote tunatambua kwamba MTU NI AFYA, bila afya njema kama jamii hatuwezi kujiletea maendeleo na hata kuyafurahia vizuri matunda ya maendeleo tuliyoyafikia, basi nakuomba ulipeleke hilo suala lako kwenye jukwaa la afya, jukwaa la matangazo madogomadogo au kwenye jukwaa la habari na hoja mchanganyiko. Tunathamini sana mchango wako, na pia kwa niaba ya wadau wengine wa elimu nikukaribishe kwa mchango wako (pale tutakapoanza) ili tuwasaidie vijana wetu/wenzetu walio masomoni.
Asante.