Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Wazalendo wachache wasaliti na mafisadi wengi afu ndio watanzania wanawapenda UMASKINI ULAANIWE sababu ya watanzania kuwaangukia mafisadi ni UMASKINI ugonjwa mkubwa hata kuliko UKIMWI....Mama anna wewe ni mzalendo Mwenye kulenga point za jamii tungependa uteuliwe hata uwe mjumbe wa kamati ya ELIMU
 
Njia rahisi na ya haraka ni M-Pesa,TigoPesa, Airtel Money nk Maoni yangu lakini Kukiwa na uaminifu wa hali ya juu...
 
Ninaomba kuwajulisha kuwa kamati ya maandalizi ya mfuko imekaa na kupitia maeneo mbalimbali ya kuuwezesha mfuko kuanza kazi zake. Mtusamehe kuchukua muda mrefu kukamilisha lakini hatua nzuri zimeanza kujitokeza. Tutaendelea kutoa taarifa mpaka tukamilishe jambo hili. Asanteni kwa kvuta subira.
 
Tayari tuna mawasiliano na mitandao hii na taratibu zikikamilika tutajulishana. tutatakiwa pia kuwa na akaunti ya benki.
Njia rahisi na ya haraka ni M-Pesa,TigoPesa, Airtel Money nk Maoni yangu lakini Kukiwa na uaminifu wa hali ya juu...
 
Tayari tuna mawasiliano na mitandao hii na taratibu zikikamilika tutajulishana. tutatakiwa pia kuwa na akaunti ya benki.
Ahsante mama na tunasubiri pia tunawaombea huo utaratibu uwe na uwepesi kutoka taasisi husika...
 
AFYA YA KINYWA NA MENO
NAPOKEA MASWALI NA USHAURI

Mkuu, huu uzi ni maalumu na wenye maudhui tofauti na ulichokiwasilisha, hapa tunaangalia ni namna gani kama jamii tunaweza kuunganisha nguvu kuwachangia vijana wetu/wenzetu wanaojiunga na elimu ya juu lakini wananshindwa kumudu gharama za masomo hayo. Tunatambua jitihada za serikali katika hili, lakini mahitaji ni makubwa mno kuliko uwezo wa bodi ya mikopo kwa sasa, kama wadau wa elimu na wana jamii huwa tunakutana kwenye uzi hii kuona nini tunaweza tukafanya ili ama kupunguza au kuondosha kadhia hii kwa wanafunzi wetu.

Jambo lako ni muhimu sana, bila shaka sote tunatambua kwamba MTU NI AFYA, bila afya njema kama jamii hatuwezi kujiletea maendeleo na hata kuyafurahia vizuri matunda ya maendeleo tuliyoyafikia, basi nakuomba ulipeleke hilo suala lako kwenye jukwaa la afya, jukwaa la matangazo madogomadogo au kwenye jukwaa la habari na hoja mchanganyiko. Tunathamini sana mchango wako, na pia kwa niaba ya wadau wengine wa elimu nikukaribishe kwa mchango wako (pale tutakapoanza) ili tuwasaidie vijana wetu/wenzetu walio masomoni.

Asante.
 
Asante kwa maoni na mchango wako,

Mama naomba msichelewe sana kukamilisha hiyo mipango ili tujue tunaanzaje kuchangia, tazama bado miezi michache tu mnamo mwezi Oktoba tutapata kundi lingine la wahitaji ambao ndio watakua wanaanza masomo yao. Natambua umuhimu wa maandalizi mazuri, najua yanahitaji muda na umakini, lakini ni lazima muangalie muda wa maandalizi usiutumie muda mwingi wa kukusanya michango.

Kila la heri.
 
a
Asante Mboboyu kwa ufafanuzi. Uzi huu ubaki kwa suala la mfuko wa elimu ili kusaidia mjadala uendelee kwa ufanisi.
 
Asante sana, andiko tayari, bodi inakaa jumamosi hii..tayari tigo na voda wanasubiri tukamilishe watupe namba za kuchangia...wanafunzi wenye uhitaji pia wamejitokeza kwa wingi. Mamlaka husika kimsingi haina tatizo imetupa muda wa matazaamio tuone uchangiaji utakuwa wa namna gani. Ninaamini hatutachelewa zaidi kutoka wiki ijayo. Asanteni
 
Mwitikio wa wananfunzi juu ya hitaji hili ni mkubwa. Mpaka sasa tuna maombi kutoka wanafunzi wa SAUT, UDSM, TUMAINI, MZUMBE NA MUHIMBILI.
 
Analyst, hili ndilo lngo lake, ikiwezekana tuondokane kabisa na kuwana kadala raia wasio na elimu kwa sababu ya kukosa ada!
 
Tujit
Tujitahidi lisipotee!
 
Ni muhimu sana kuwa na mfumo wa elimu unaothamini utu, uzalendo na uadilifu. Kila mtu atafute sifa anayostahili kuipata.
 
Na sisi tunajitahidi kukamilisha taratibu za mfuko kuanza kazi wanafunzi wenye sifa na nia wapate msaada wanaohitaji.
 
Waheshimiwa wanajukwaa, natoa taarifa kuwa tumechukua muda mrefu kuanza lakini tunaendelea na mchakato kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa utaratibu unaokubalika wa nchi, taratibu za kisheria nk. Ninajua wanafunzi wengi wametegemea tutaanza mapema na sisi tungependa kufanya hivyo lakini kwa usalama na kufuata utaratibu tunachelewa, mtuwie radhi. Msikate tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…