Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Tuvumiliane kidogo, kukamilisha taratibu zote, inachukua muda kidogo kwa upande wetu.Asante

Mama, nimeanza kupata wasiwasi kidogo juu ya hili zoezi jema uliloliasisi, kwa vyovyote vile iwavyo ni lazima tutambue kwamba muda si rafiki yetu, tunapaswa kupewa utaratibu wa kuchangia mapema iwezekanavyo ili tuwe na muda mrefu wa kuikusanya hiyo michango na hivyo angalau tupate kiasi kikubwa cha fedha na kusaidia idadi kubwa zaidi ya wanafunzi.

Ninaendelea kusisitiza kwamba ninatambua umuhimu wa maandalizi mazuri kabla kuanza michango, lakini ni lazima tujue kwamba adui yetu ni muda, muda hautusubiri hata kama tunachofanya ni kitu muhimu (maandalizi).

Kwa mwaka huu wa masomo (2017/2018) ninategemea vilio kuongezeka zaidi, japokua mimi sio mtabiri ila hata kwa hisia tu.
Baada ya kuipitia hotuba ya bajeti ya wizara ya elimu kwa mwaka huu, imesisitizwa kwamba bodi ya mikopo itaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaostahili tu.
Hofu yangu inakuja hapo kwenye NANI ANASTAHILI ? Kwa mujibu wa bodi na uzoefu wa mwaka jana, ni wazi waombaji waliosoma shule binafsi, waliosoma masomo ya sanaa na watakaochaguliwa kozi zisizo za kipaumbele watamwaga machozi yao tena mwaka huu (kwa bahati nzuri) kama kiwango cha mwaka au (kwa bahati mbaya) zaidi ya mwaka jana.

Please mum, don't tell us to wait any longer.

Ni katika kukumbushana tu. Nakutakia muda mwema.
 
kuna wanafunz wengine wa elimu ya juu n wanafaika wa mikopo na walipostpone mwaka na taarifa ambayo tunapata et kwamba kwa huu mwaka ambao tumerud chuo hatuwwez kupewa mkopo naomba wahusika watuangalie katka hlo lina ukweli au#loanboard
 
Mh. Umeupokeaje uteuzi wa kuwa Mkuu wa Mkoa?
 
sasa kwa brain hii kwa nini Magu asipongezwe??
 
Hongera Mama Kwa Uteuzi, Sasa Ukafanyekazi Siasa Basi.. Mambo mengi yalisemwa na mengi yakaendelea kusemwa katika siasa za nchi yetu Mh. Rais akakuteua wewe. Nakuomba uache siasa ufanyekazi. Mh makonda anafanyakazi hana siasa siasa. Ufanye hivyo uache siasa
 
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako."
Leo Mama Kikwete AMEGEUKA nguzo ya chumvi. Hamtetei tena Mtotowa Kike. Anasema anayepata mimba shuleni ASISOME! Na wewe Mama Mghwira umeteuliwa katika nafasi ambayo, kwa mujibu wa katiba CCM, utahudhuria, KISHERIA, vikao vukuu vya Mkoa vya chama "kisichokuwa chako". Hawa wamama walioheshimika, mbona WANATUANGUSHA?
 
Cheo chenyewe ni cha kisiasa, sema akafanye siasa safi.
 
Mama umetuangusha, hiyo ilani ya CCM uliyopewa leo kipindi cha uchaguzi si ulikuwa unaipinga? Je yale matatizo uliyokuwa unayasema kwa ilani hiyo utayatatua? Some of us tulikuona kama kiongozi wa kipekee lakini ki ukweli umetuangusha
 
Mama umetuangusha, hiyo ilani ya CCM uliyopewa leo kipindi cha uchaguzi si ulikuwa unaipinga? Je yale matatizo uliyokuwa unayasema kwa ilani hiyo utayatatua? Some of us tulikuona kama kiongozi wa kipekee lakini ki ukweli umetuangusha
ukweli ni kwamba tatizo tumbo Singojr:
 
ukweli ni kwamba tatizo tumbo Singojr:
Yaani huwezi kuamini yule mama niliyemuona kichwa another hope kwa watanzania wanyonge leo kasmile akipewa ilani kandamizi. Ilani isiyo na hata mpango ya katiba mpya. Ataenda lakini hii itamuwinda i wish fahamu zimrudie mapema.
 
Jamani huu Uzi ni mahsusi kuhusu masuala ya mikopo (hata kama aliyeuanzisha ndiye mteuliwa), kama mna hoja, pongezi, malalamiko na madukuduku kuhusu uteuzi wake tafadhali nendeni kwenye nyuzi zingine (ziko nyingi sana zinazohusu uteuzi wake) mkazungumzie huko. Uzi huu si sahihi sana kwa jambo hilo, tusijaribu kupoteza maudhui ya huu Uzi.
 
Nakutakia utekelezaji mwema wa ilani ya CCM. Kumbe hukua mwenzetu kila la kheri katika majukumu yako mapya.
 
Kama haamini katika ilani ya aliyoitetea na kuzunguka nayo nchi zima. Tutamwamini vipi kwa thread ya JF
 
Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu


Anything can happen..

Mwacheni mama Anna akapige kazi..
 
Kama haamini katika ilani ya aliyoitetea na kuzunguka nayo nchi zima. Tutamwamini vipi kwa thread ya JF
Bora mmuunge mkono tuu akatende haki...sidhani kama atarudi nyuma

Ila lazima muelewe wanasiasa wana nia moja siku zote...

Watanzania tunapaswa kujifunza na kuelewa hili..

Mwisho wa siku ninyi msioelewa wanasiasa ndio mnakufa kwa presha.

If you can't fight them, join them- Ndicho alichokifanya Mama Anna.

All the Best to her..
 
Kama haamini katika ilani ya aliyoitetea na kuzunguka nayo nchi zima. Tutamwamini vipi kwa thread ya JF

Nilikua nazungumzia maudhui ya huu Uzi ukilinganisha na kinachojaribu kujadiliwa hapa, nimeshauri muende kwenye nyuzi kadhaa zinazozungumzia huo uteuzi (zipo, tena nyingi tu). Hapa panapaswa kuachwa pashughulike na namna ya kuwasaidia wahanga wa gharama za elimu ya juu. Kuhusu hayo masuala ya ilani, anachokiamini aliyeteuliwa na mengineyo mengi yanayokwenda pamoja na uteuzi wake yakajadiliwe kwenye nyuzi husika. Nilimaanisha hivyo tu mkuu.
 
Wazo zuri, na uwezo kupitia kwa wananchi wapenda maendeleo upo. Serikali kukwepa jukumu la kugharimia elimu ya juu ni ubinafsi wa viongozi wetu, na mgawanyo usio sawa wa raslimali zetu. Mafanikio ya elimu ya vijana wetu ndio mafanikio ya taifa. Elimu bure ya msingi mpaka f4 si mzigo mkubwa kwa familia. Uwezo kulipia chuo kikuu ni mgumu. Wingi wa mikopo inayotajwa kutolewa na sesikali ina mapambio, kuna wengi wamepata %ge ndogo sana. Wazo hili likijitangaza kwa wananchi, wengi watahamasika kuchangia. Mchango wa sh 1000 tu kwa mwezi, kwa watu 1m, kwa mwaka 1, mfuko wako utakuwa sh 12bn za kusomesha watoto elfu 6 kwa 2m.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…