Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

QUOTE="kerubi afunikaye, post: 20021372, member: 144421"]Mama wazo lako zuri,tunashukuru maana sie wengine tunaosomesha hadi wadogo zetu kwa kweli awamu hii imekuwa mzigo mzito.
Mtu una vijana wawili wote wako chuo,no mkopo,yaani hadi kichwa kinauma.
Kuna jambo moja nimekutana nalo wakati nahangaika na mdogo wangu mmoja,hebu tusaidie kulifikisha huko ngazi za juu walifikirie upya.
Nakumbuka wakati akiweka jiwe la msingi la hosteli mpya UDSM,mh,Rais Magufuli alisema ni wakati wa vyuo vya serikali kuchukua idadi ya wanafunzi sawa na capacity yake,kwa kuwa vimekuwa vinachukua wanafunzi wachache tofauti na uwezo wake,matokeo yake wanafunzi wengi huenda vyuo binafsi ambavyo vimekuwa vingi bila sababu za msingi.
Katika masuala aliyowahi kuyasema Magufuli,hili lilinigusa sana.
Naomba ukipata nafasi uende kwa Rais ukamkumbushe kuhusu hilo,vyuo vya serikali viongeze udahili wa wanafunzi,ili watoto wengi wasome huko hata kama ni kwa kujilipia,walau ada za vyuo vya serikali ni nafuu.
Hili litazamwe hasa kwenye zile kozi vipaumbele vya taifa,vyuo vya govt vichukue watu wengi.Kozi kama za tiba,it's better wengi wakasoma huko maana ni expensive sana,ni nyeti sana,na wanahitajika sana wataalamu hao.
Mama unahamasisha vijana wa mitaani wajiendeleze vyuoni,uko sahihi,ila katika kuwapa moyo,tungepunguza masharti magumu kwao.Na wao wapewe mikopo,na wadahiliwe na vyuo vya serikali,maana sasa hivi vyuo hivyo havichukui vijana wanaojiendeleza ambao walimaliza zamani.Vinachukua from 2015 kuja mbele nadhani.Sasa mtu anajisomesha mwenyewe,hapewi mkopo,halafu analazimishwa akasome vyuo binafsi vyenye ada kubwa ilhali vyuo vya govt bado vina nafasi?ni bora angeruhusiwa kusoma govt institutions lakini kwa kujilipia,au hata na kozi fulani nyeti iwe hivyo ili kuwahamasisha vijana kusoma huko.[/QUOTE]

Kwelikabisa, hata mimi nilifanyahivyo zamani. lakni mtoto aliyefika miaka 18 ni vizuri apate mkopo unaomfaa na kumpa fursa ya kujifunza kujitegemea. La sivyo inaharibu tabia za watoto wategemezi kuwanyonya wazazi bila sababu ya msingi. Kwa hiyo mkopo una faida nyingi na elimu pana ya maisha. Tuchange sisi, tuwape fursa viajana kujifunza kuitegemea licha ya ada na mahitaji mengine.
 
I'm speechless!!

Mama Mghwira umeshamaliza kila kitu.Hongera sana,Uko very active.
 

Kididimo, hiyo ndiyo roho ya nia hii...hakuna zaidi wala pungufu.!
 
Mama anzisha harambee hapa hapa JF tunatosha kufanikisha hili jambo.
Kweli kabisa, tuanze wakati kamati inajipanga kuandaa uzinduzi rasmi...ili angalau waliotufikia wakati huu wapate nafsi kuendelea na masomo. waliorudishwa juzi nao warudi na kunedelea. Itakuwa amani sana!
 

Asante Gamba, mashrti yatazingatiwa.
 
Huyu Mama Anna Mghwira ni hadhina kubwa sana ndani ya taifa Mama naamini kama jambo hili litatendewa haki na kulifanyia kazi utakuwa umesaidia sana watoto wengi wa masikini wenzetu katika nchi hii
 
Anna Mghwira. Kwa, Rais tuliye nae hashauriki tena kwa wanawake ndio kujisumbua huyu Mkuu wetu amekuzwa ktk mfumo dume
Cha mhimu tujipange 2020 hakuna vinginevyo tumeshaumia
Daaah.... Kweli kuwa ukawa ni zaidi ya uchizi. Sasa ujipange 2020 ili umuweke nani? Namuunga mkono mama asilimia zote! Mabadiliko yanaanzia kwako hapo ulipo, na pia serikali ina ukomo wa bajeti, kama tukiweza kulifuata au kuliboresha wazo la mama ni hatua nzuri na pia ni wakati muafaka.
 
Mama upon
 
Natamani vijana wa mwaka wa kwanza walio appeal wangejibiwa kabla vyuo kufunguliwa kwenda semista ya pili
 
Wazo zuri bimkubwa ila lazima utambue mwanzo ni mgumu pia usiogope vikwazo tutafanikiwa
 
Mama wewe ni Kiongozi Bora. Mungu akubariki sana. Natamani wewe ndio ungekuwa hata makamo wa rais labda ungesaidia kufikisha ushauri vizuri kwa mtukufu Rais asiyejaribiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…