1. Kama mbunge alipaswa aseme na kupendekeza nini kifanyike. Kusema tu waende wakaangalie kwa sababu mitaani halieleweki. Sijui anataka wakaangalie nini sasa maana wao ndiyo wameshaliangalia na kuja na utaratibu huo...
2. Ukweli ni kuwa kwa namna lilivyoletwa na litakavyotekelezwa (kama halitafanyiwa mabadiliko), hii haiwezi kuwa KODI YA MAJENGO bali ni bora iitwe KODI YA LUKU yaani kila mwenye LUKU ya umeme...
3. Ni kwa sababu, siyo kila LUKU YA UMEME imewekwa kwenye Jengo. Kuna watu wana LUKU na wameziweka kwenye miti Mf. Mafundi seremala, mashine za kupasua mbao nk nk
4. Aidha huko vijijini kuna LUKU zimewekwa kwenye nyumba za nyasi na matembe (zilizoezekwa kwa miti na udongo). Hawa kuwalipisha kodi ya Jengo siyo sawa hata kidogo tena kwa kiwango sawa na mwenyewe nyumba ya thamani ya Tshs. 300,000,000...!!