Anne Kilango Malecela: Kuna mkanganyiko kwenye suala la kodi ya majengo. Ieleweke anayelipa ni nani

Hii kitu naiona kama ina ugumu fulani hivi ktk utekelezaji wake...

Na shida kubwa ni kwa sababu zaidi ya 70% ya makazi (majengo) ya watu si rasmi, serikali haiyatambui...

Nadhani serikali ingeanza na kurasimisha makazi ya watu kwanza na ishu ya kulipisha kodi ya jengo kwa namna bora zaidi na ya haki ingeweza kuwa rahisi sana...

Lakini kwa hivi na kwa kutumia kigezo cha "mtu kumiliki LUKU ya umeme" tu, ni wazi kuna wenye nyumba wala hawatalipa kodi hii na italipwa na asiye mmiliki wa jengo...

By the way, huyu mwenye jengo kwa mantiki hii atakuwa analipa kodi aina mbili sasa, right?

MOSI, atalipa KODI YA ARDHI na sasa KODI YA JENGO, au siyo jamani...

Na hivi ni kwanini tusilipe kodi ya kichwa tu badala ya hii ambayo ni very complicated?

Mfano kama waTZ wenye haki yq kulipa kódi hii tukawa 35,000,000 na kila mmoja akalipa 10,000 kwa mwaka. Maana yake serikali itakusanya TZS 350,000,000,000..

Kama CCM wanataka hela, waturudishe tu huko. Wasisahau na ya ng'ombe, mbuzi, punda, Kuku, mbwa, baiskeli, pikipiki na Magari...!!
 
Wakupe Efd machine ukienda haja utoe risiti yaani.
 
Mbunge kasema "ieleweke kodi analipa nani" hivyo ni kazi ya tra kujua ni nani hasa analipa kwa huu utaratibu mpya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…