Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, amesema Watanzania wamezidi maneno badala ya vitendo, akiwataka kubadili mtazamo huo kwa kuiga mfano wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu na mbunge wa Ismani, marehemu William Lukuvi kwa kutanguliza kazi.
Akizungumza leo Jumanne, Machi 31, 2026 wakati wa mazishi ya kiongozi huyo (Lukuvi), ambapo amemuelezea Lukuvi kama mtu wa vitendo zaidi na si wa maneno, jambo lililomtofautisha na wengi.
“Lukuvi hakuwa mtu wa maneno bali vitendo zaidi. Tukiwa Umoja wa Vijana tulikuwa timu ya mwisho pamoja na kina Jakaya Kikwete na Abdulrahman Kinana, na baadaye ndipo kikaingia kikosi cha akina Lukuvi,” amesema.
Soma Pia: Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia
Ameongeza kuwa Lukuvi aliwafundisha wananchi wa Ismani kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii bila kulalamika.
“Watanzania tumezidi maneno, lakini maneno pekee hayaijengi nchi, tunapaswa kufanya kazi,” amesema