Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Unaweza kumtaja Seymour Hersh kuwa ndo mwandishi bora wa habari za uchunguzi duniani, jina la Hersh ndo lilibeba habari ya kufichua yaliyojili huko Vietnam kwenye My Lai Massacre, lakini wapo wengine watasema majina ya Bob Woodward pamoja na Carl Bernstein ambao ndo waliibua habari kuhusu kashfa iliyomtoa madarakani Rais Richard Nixon, kashfa ya Watergate.
Kuna Anabel Hernandez kutoka Mexico ambaye ndo alifichua uchafu ambao wanasiasa wanaufanya kwa ushirikiano na makundi ya uhalifu haswa katika usafirishaji na uuzaji wa madawa ya kulevya. Lakini leo natamani nije na jina moja la kipekee sana, jina ambalo limeandika vitabu vitano bora sana haswa katika kueleza uhalisia na ukweli wa serikali ya Marekani.
Yale yote ambayo yapo chini ya carpet basi kalamu yake ilikuwa tayari kuyaonesha wazi kwa watu, yeye ni nembo ya ujasiri na uchambuzi wa kina wa masuala ya siri za serikali ya Marekani. Sio mwingine bali ni Annie Jacobsen, moja ya vichwa haswa kwenye uandishi wa vitabu vinavyobeba siri nzito katika mtindo wa maandishi.
Jacobsen alianza kujulikana sana baada ya kuchapisha kitabu chake maarufu “Area 51: An Uncensored History of America's Top Secret Military Base” mwaka 2011. Kitabu hiki kilitoboa undani wa eneo la siri la kijeshi la Area 51, mahali ambapo kwa miongo mingi kumekuwa na tetesi kuhusu majaribio ya ndege zisizoonekana kwa rada, teknolojia za hali ya juu, na hata viumbe wa angani maarufu kama Alien.
Ingawa wengi walikiona kama nadharia za ki-majabu, utafiti wake ulitokana na mahojiano ya watu waliowahi kufanya kazi katika eneo hilo. Watu kadhaa waliowahi kupata kufanya kazi kwa ukaribu ndani ya eneo la Area 51 walipata kuelezea kazi, majukumu pamoja na mambo baadhi ambayo umma walikuwa hawajui hata kidogo.
Lakini Jacobsen hakusimama hapo. Alizidi kupenya kwenye maeneo yenye giza la kiintelijensia kupitia vitabu vingine kama:
“Operation Paperclip” cha mwaka 2014: Kitabu hiki kinachunguza jinsi Marekani ilivyowachukua wanasayansi wa Kijerumani waliokuwa wa Nazi baada ya Vita ya Pili ya Dunia na kuwapa nafasi ya kufanya kazi katika miradi ya siri ya kijeshi.
“The Pentagon's Brain” cha mwaka 2015: Hiki ni kitabu kinachoeleza historia ya DARPA – shirika la utafiti la jeshi la Marekani ambalo limehusika katika uundaji wa teknolojia hatari mbalimbali kama drones, silaha za akili bandia, na hata utafiti wa udhibiti wa akili.
“Surprise, Kill, Vanish” cha mwaka 2019: Kinahusu vikosi vya siri vya CIA na jinsi wanavyotekeleza mauaji ya kimataifa kwa siri kubwa, vikishika nafasi ya vitengo vya kijasusi wa enzi za Vita Baridi.
“Nuclear War: A Scenario” cha mwaka 2024: Kitabu hiki kipya kinaeleza kwa undani uwezekano wa vita ya nyuklia, kikielezea mpangilio wa nchi ambazo zimepata kuanza kuonesha hatari ya matumizi ya teknolojia hizi, kitabu hiki kinakwenda kuonesha mtiririko wa sekunde kwa sekunde na dakika kwa dakika ya mashambulizi ya nyuklia kama yangetokea leo.
Annie Jacobsen ameweza kuibua mijadala mikubwa juu ya maadili ya serikali, udhibiti wa taarifa, na usalama wa dunia. Uandishi wake haumaanishi kuwa yeye ni mtu ujasiri, bali ni inatoa nafasi ya waandishi kufikiri upya juu ya imani yao kwa serikali na mustakabali wa teknolojia za kijeshi. Kwa Jacobsen, ukweli unaogopesha zaidi ya nadharia. Na kwa wasomaji wake, kila ukurasa ni mlango wa kuelekea katika dunia ya siri nzito za nguvu na udhibiti.