Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Mkuu Artificial intelligence naomba ufafanuzi kuhusu hili suala
Nyayo hazigunduliwi kwenye mawe tu, bali sehemu nyingime za kawaida hata zilizo tambalale na zenye udongo wa kawaida. Tofauti ni kwamba nature of rocks inakuwa affected by different factors, kwahiyo kuna sehemu ukikanyaga unyayo unabakia either kwa mda mfupi au mrefu au pengine haubaki kabisa kutokana geological factors za hilo eneo. Mfano mzuri kwa wanyama, kuna sehemu wanyama wakubwa kama tembo/kiboko wakikanyaga nyayo zao zinabaki pale, kwahiyo ikiwa eneo hilo halitapata disturbance yeyote either ya kimazingira au kibinadamu, basi nyayo hizo zinaweza kukaa pale kwa muda mrefu. Kingine hata miamba ina muda wa ku disintegrate kutokana na physical, chemical na evironmental factors, kwahiyo nyayo kuendelea kuwepo inategemea na geological time scale pia.
 
Ndugu mimi nshazungumzia kuhusu giants sehemu ya 11, ipitie kwa umakini msitari kwa msitari.
Mkuu nilishaisoma hiyo namba 11 lakini bado sijaona sehemu imejibu haka kaswali kangu.

Maandiko yako ni mazuri mkuu yanafikirisha ila haina maana kwamba yatakuwa na majibu ya maswali yote ya wadau,hivyo tuvumilie na tujibu maswali kwa kadri ya muda ulionao ili tuzidi kupanua ufahamu.
 
Ndiyo ni Annunaki, Genesis na archeologists wamethibitisha hilo. Ukitaka kuamini kabisa kaangalie family tree yetu. Hata sisi wenyewe ni uzao wa Annunaki.
 
Hapana shaka ndugu, mimi kama kitu sikijuhi kabisa nasema.
 
kwahiyo ikiwa eneo hilo halitapata distabunce yeyote either ya kimazingira au kibinadamu
Mkuu kuhusu hii ishu inawezekana lakini kwa miaka hiyo mingi ambayo inadaiwa imepita ambayo ndio imetokea ni ishu ngumu sana kusema kwamba hizo nyayo ni za miaka na miaka.

Wakati huo kuna mvua,kuna matope,kuna upepo na vitu vingine.

Inawezekana vipi kwa hali hizo zote nyayo ibaki kwa mamilioni ya miaka ?
Nyayo hazigunduliwi kwenye mawe tu
Tuanze na Haya mawe mkuu, kuna utaalamu gani wa kisayansi ambao unaelezea kwamba jiwe linaweza kubonyea likikanyagwa alafu likatengeneza nyayo.

Mbona katika mazingira ya kawaida haiwezekani hii ishu ?
kuna sehemu wanyama wakubwa kama tembo/kiboko wakikanyaga nyayo zao zinabaki pale,
Ni sahihi mkuu lakini sio kwamba nyayo hizo ni za mamilioni ya miaka kama nyayo zetu za kale zinavyosemwa,hizo alama za wanyama utaziona za muda mfupi nyuma sio mamilioni ya miaka.


Kingine hata miamba ina muda wa ku disntagrate kutokana na physical, chemical na evironmental factors
Kivipi miamba ikidisintagrate inaweza kufanya mtu akikanyaga huo muamba ubonyee na kutengeneza nyayo mkuu au umemaanisha nini hapo mkuu ?
kwahiyo ikiwa eneo hilo halitapata distabunce yeyote either ya kimazingira au kibinadamu
Ni jambo ambalo kiakili linaleta shida kwamba hizo nyayo zipo katika sehemu ambazo tokea hao jamaa wapite basi sehemu hizo hazijawahi kupata mvua kubwa za kufanya matope,wala upepo mkali wa kuondosha mchanga n.k

wakati hiyk ni sehemu ya dunia pia inakosaje vikwazo hivyo kwa mamilioni ya miaka au malaki ya miaka mpaka hivi leo ?

Lakini pia wakati hao watu wanakanyaga maeneo hayo ni ushahidi kwamba hayo maeneo ya ardhi yalikuwa katika hali ya utopetope ndio maana ikaweza kutengeneza nyayo,hiyo inathibitisha kwamba maeneo hayo yanaweza kupatwa na maji na hali zingine za kidunia hivyo maeneo hayo yanaweza kukubwa na disturbance za aina hiyo.

Kwa maana hiyo kwa muda ambao inadaiwa hizo nyayo ndio jamaa wamepita mpaka hivi sasa kiakili haiwezekani kwamba hazikupata disturbance hizo zote za kimazingira.

Maana yake zilipata hizo disturbance za mimazingira,why mpaka leo zipo ?
 
Ndiyo ni Annunaki, Genesis na archeologists wamethibitisha hilo. Ukitaka kuamini kabisa kaangalie family tree yetu. Hata sisi wenyewe ni uzao wa Annunaki.
Mama ni hivyo mkuu huoni kwamba dini inaweza ikawa sahihi ikisema kwamba anunaki ni muendelezo wa uzao wa adamu.?

Kwa sababu hata adamu naye alikuwa ni pande la mtu kweli kweli,na uzao uliokuja baadae pia.

Hii ni kusema kwamba tukiunganisha doti tutaona kwamba hata adamu tunaweza kumuita anunaki kwa sababu alikuwa ni pande la mtu haswa ?

Je sio kwamba hayo mabaki yaliyogunduliwa sio anunaki waliomuumba mtu bali ni anunaki waliotokana na uzao wa adamu ambao wao walikuwa ni majitu makubwa sana ?
 
Annunaki hawatokani na Adam, ila Adam anatokana na Annunaki. Taarifa za Annunaki kumtengeneza mtu chanzo chake ni sumerian na mesopotamia, ambako ndiko chimbuko la civilization na dini, maandiko ya dini yametolewa huko. Hizo habari za mabaki ya giants zinatumika kama ushahidi wa kuthibitika ya kwamba ni kweli Annunaki walikuwepo duniani yapata miaka 450000 iliyopita.
 
Jiwe ni muamba mgumu hivyo kubonyea kisa mguu wa mtu siyo rahisi, isipokiwa udongo huo kubonyea ni rahisi (na mara nyingi mabaki ya nyayo yamepatikana sehemu zenye udongo wa tope ukilinganisha na sehemu yenye miamba migumu).

Niliposema rocks ku disintegrate, nilimaanisha inaweza kuwa factor moja wapo ya nyayo nyingi kuisha na kupotea mazima.

Kama unaamini kwamba haiwezekani kukosekane factors za kimazingira kama mvua n.k kupelekea kupotea kwa nyayo hizo, na mimi nikwambie kwamba huenda kutokana na factors hizo hizo nyayo nyingi zimepotea na kujikuta zikipatikana chache kwenye maeneo machache hapa duniani.

Kwahiyo kutokana na sababu hizo ulizozisema wewe ni rahisi kutembea dunia nzima, ila ukakutana nazo maeneo machache tu kama archeologists wanazokutana nazo.
 
Taarifa za Annunaki kumtengeneza mtu chanzo chake ni sumerian na mesopotamia,
Haya si ni maandiko mkuu ?
ambako ndiko chimbuko la civilization na dini, maandiko ya dini yametolewa huko.
Kama yametolewa huko kwa nini dini iende kinyume na hizo chimbuko wakati imetokea huko mkuu ?
Hizo habari za mabaki ya giants zinatumika kama ushahidi wa kuthibitika ya kwamba ni kweli Annunaki walikuwepo duniani yapata miaka 450000 iliyopita.
Kwa nini hizo mabaki za giant isiwe ndio uthibitisho wa kwqmba binadamu wakubwa wakubwa wa zamani ndio walikuwepo kama dini zinavyosimulia ?

Why unakataa kwwmba watu wa zamani walikuwa wakubwa sana pengine ndio hao giants mnaowasema ?
 
(na mara nyingi mabaki ya nyayo yamepatikana sehemu zenye udongo wa tope ukilinganisha na sehemu yenye miamba migumu).
Kwa maana mara chache mabaki ya nyayo yalipatikana kwenye mawe ama miamba migumu ?

Kama zilipatikana mara chache maana yake hizo nyayo zipo,na kama zipo swali langu liko vile vile mkuu kivipi unyayo uweze kutengenrza alama ya nyayo kwenye mwamba mgumu ?
Niliposema rocks ku disintegrate, nilimaanisha inaweza kuwa factor moja wapo ya nyayo nyingi kuisha na kupotea mazima.
Hapa nimekusoma mkuu
na mimi nikwambie kwamba huenda kutokana na factors hizo hizo nyayo nyingi zimepotea na kujikuta zikipatikana chache kwenye maeneo machache hapa duniani.
Hoja yangu mkuu ni kuwa miaka mingi iliyopita tokea madai ya anunaki na factor za kimazingira kama hizo kuwepo kwa miaka yote haiwezekani nyayo zikabaki kwa muda wote huo.

Kwa sababu hayo maeneo yenye nyayo ni dhaahir kwamba yikuwa yanapata mvua juu au yalikuwa yanachemchem ndio maana yakapatokana matope ambayo jamaa waliweza kupita na kuacha alama.

Sasa hata baada ya kupita hao jamaa haina maana kwamba hizo factor zimeondoka,bado pengine mvua ziliendelea kunyesha na matope yikuwepo.

Why kwa miaka yote hiyo zisipotee hizo nyayo zote ?

Tukumbuke kuwa factor za kimazingira hazina cha kupoteza kuondoa nyayo zote,labda tuseme ziliamua kubakisha baadhi ya nyayo ili ziwe kama ushahidi na hii ni ngumu kwa sababu mvua na matope yakinyesha inafukia kila kitu bila kubagua.
 
Kwanza jua yalikuwa mazito halafu marefuuu! sisi tulikuwa kma Panzi kwa.(rejea kitabu cha mambo ya nyakati) sasa linganisha panzi aone unyayo wako mmoja kariakoo....huo unyayo mwingine atauonea mbali sana,

mfano Kariakoo na ubungo!! sasa km kariakoo umekanyaga kwenye jiwe na ubungo umekanyaga kwenye vumbi ...ni unyayo wa kwenye jiwe tukariakoo utaonekana! Olduvai gorge drsa la tatu historia uliisoma kweli mkuu??!

sasa unganisha na kulinganisha hiyo historia na nyao km hizo!....utakuta kwamba kwingine walipata nyayo na kwingine walipata mifupa, mafuvu, na kwingine zana za vita, zana za kukamatia wanyama wakali nk!
 
Ndugu haya maswali yako yote yameshajibiwa humu ni yameshajadiliwa. Maandiko yalipindishwa na wao waleta hizo dini kwa maksudi yao wanayoyajua wenyewe ndiyo maana leo hii unashangaa na kuuliza maswali mengi unapo ambiwa umetengenezwa na Annunaki. Kwenye vitabu vya dini wameandika uwepo wa giants ambao ni hao Annunaki hata Genesis imeliweka wazi, na hapa wapo sahihi, shida inakuja hawakusema kama Annumaki ndiyo waliomuumba mwanadamu nadharia inayopingana na tablets from sumerian. Kwa mkutadha huo utaacheje kuyaamini yale yaliyoainishwa kutoka sumerian, ambako ndiko chimbuko la hayo maandiko ya dini unayoyaamini wewe?
 
Ndugu kwani hujawahi kukanyaga juu ya jiwe ukiwa na tope au umevaa buti na unyayo ukabaki? Sasa fikiria ukubwa wa hayo majitu, na unaambiwa mtu mrefu na mnene/mkubwa wa sasa angeweza kuishia kwenye goti tu kwa hayo magiants.

Bado ntaendelea kukujibu kwamba kama una amini uwepo wa factors hizo, ni factors hizo hizo zilizopelekea nyayo na mabaki mengi kupotea sehemu nyingi duniani, kwahiyo hizo zinazopatikana ni masalia machache sana na ni nadra kupatikana.
 
Hili nililiandika sehemu ya 11 kuhusu ukubwa wa hao giants. safuher yeye amekamatia kwenye nyayo tu, anataka kujua kuhusu unyayo hayo mafuvu, mifupa n.k ameviweka pembeni kwanza.
 
Na nikuulize kidogo, ukiachana na nyayo vipi kuhusu mabaki mengine kama mifupa, mafuvu, skeletons n.k unaamini kwamba yana athiriwa na evirommental factors unazozisema au uamini pia?
 
Aisee pole sana kwa kufungiwa account, mimi mwenyewe kuna vitu imenibidi nisiviandike kabisa kwenye huu uzi.
mkuu sehemu ya mwisho bado haijatoa mwanga. Baada ya binadamu kuumbwa kama kitendea kazi cha kina Annunaki, mtu wa leo ni nani? Kwa nini pawe na ukinzani kati ya mtu huyu na Annunsk hadi binadamu atake kuhamia sayari nyingine kupisha Annunak?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…