Inasikitisha sana. Sasa hv kila anayejisikia anakiita chuo chake University na anapewa kibali hasa kwa miamvuli ya vyuo vikuu vishiriki. Naweza kusema, serikali sasa ipunguze siasa kwenye maswala ya msingi, wasilete siasa za Buzwagi kwenye masuala ya elimu, la sivyo tutaonekana tumekosa muelekeo hasa pale tutakapojiunga na shirikisho (tunaloshinikizwa na viongozi) la Afrika ya Mashariki. Wenzetu Kenya waliona si vyema kubadili colleges kuwa universities wakaleta wawekezaji kama wale walioanzisha Daystar University n.k. The same wawekezaji huwa wanatoa chance kadhaa kwa wazawa wenye vipaji kiasi cha wao kujiunga na hivyo vyuo ambavyo vingi ni vya kimataifa. Sasa hv Kenya hata mtoto wa masikini ana digrii. Sio kama hapa bongo watoto wa masikini wenye digrii ni wale wenye exceptional vipaji, as chuo tegemezi kwa masikini (UDSM) nacho kimegeuka private (practically) though theoretically na kiuongozi ni cha serikali.
Kuna mwana JF mmoja nimeona anatetea swala la hizo colleges kutokuwa na professors au doctors. But sidhani kama anaelewa kuwa Universities huwa zinakuwa assessed on annual basis na kuwa ranked internationally. Chuo kikuu cha DSM mwaka 2005 kilikuwa cha 64 ingawa kina professors wa kumwaga. Sasa sijui hivyo anavyovitetea vina professors wangapi na vitakuwa ranked wapi.
Pia atambue wawekezaji au hata mashirika na miradi ya serikali, wanaajiri based on sehemu mtu aliposoma yaani kama mtu anavyooa based on malezi ya mke mtarajiwa.
Siku hizi elimu imeoza, mfano, UDSM ina lecture rooms ambazo zina uwezo wa kubeba wanafunzi 500, but maprofesa ambao wameshachafuliwa akili na siasa, wana-admit wanafunzi 800 ili tu serikali ipate namna ya kujisifia kuongeza kiwango cha elimu. Huu ni upumbavu uliokomaa. Utakuta wanafunzi wamesimama milangoni, wengine wamekaa chini, ni aibu. Sasa sijui hz ni bora digrii au digrii bora zinazozalishwa hapo. Utakuta uongozi wa chuo unakazana kurekebisha mazingira kwa gharama kubwa wakati hakuna madarasa.
Siku hz, ukienda hivyo vyuo vingine kama Mzumbe, ni aibu, kuna digrii za ajabu. Watu wanapewa A za kumwaga ili tu washindane na vyuo vingine. Wakati ukikaa nao kwenye utendaji ni bora form six au form four. Ni wachache tu ambao wana akili binafsi. Bt these watu hawafundishwi kuelewa but kufaulu na kupata A nyingi ili wakienda kwenye soko waonekane wanafaulu sana. But ukichunguza, utakuta wanafunzi wanajua maswali before hata ya mitihani. Tunakwenda wapi..??
Mimi nafikiri serikali sasa iwekeze nguvu, na kualika wawekezaji kwenye sekta ya elimu rather than kualika wawekezaji wengi kwenye madini yasiyo na manufaa kwa wananchi wa chini. Waangalie mifano ya Kenya kisha wafikirie namna ya kuinua elimu na sio kuchafua elimu.