Kumbe huyu Mbunge alikua mkamuaji! he got what he deserves..
Masatu na wengine wote msomao,
Wakuu ningewaomba msilisikilize jeshi la polisi kule Kenya maana wote wako-compromised na Kibaki.Kilichonifanya nijue kwamba hili jeshi is full of a criminal mind ni wakati alipouliwa Bw.Robert Ouko.Jamaa walisema eti he committed suicide in a very wierd fashion.Eti alijiwasha moto kisha akachukua bomba na kujipiga risasi.Huyu bwana pia kumbuka kua alipatwa na mguu uliovunjika...sasa nambie alijunja mguu,kisha akajiwasha moto,kisha akajipiga risasi????Duuuhh!... hii ishu ilileta kitimtim mpaka Moi akawaleta wale jamaa za Scotland yard.Kwa ufupi hadi leo aliyemuua Ouko hajulikani!Kisha tazama wanavyoua watu bila mpango na evidence zikionyeshwa wansema eti walopigwa risasi wana-act kama kwenye sinema za Rambo!Aliyesema ushuzi huu anaitwa Bw. Kiraithe ambaye ni kigogo wa jeshi la polisi la Kenya na kabila la Kibaki.
Sasa niambie kama unaweza kuamini maneno yatokayo kwenye vinywa vya watu kama hawa?
Sasa acha niwape nyuzi niliyobwagiwa hapa kutoka Nairobi.(my contact is up there in politics za Kenya kwa hivyo naamini updates zake kwa sana).Huyu mbunge wa Ainamoi aliyebwagwa jana
alipigwa tembe kumi na tisa mida ya
saa nne unusu asubuhi kadamnasi ya watu.Aliyefanya kitendo chenyewe alikula kona hadi mji uitwao
Turbo ambako alichukuliwa na helicopter nyeusi na
kupelekwa to an unknown destination.Tetesi ni kwamba helicopter yenyewe ni ya mtoto wa yule Rais wa zamani,Daniel Arap Moi.Kwa jina anaitwa
Gideon Moi.Hii yote imefanyika chini ya lisaa limoja na tayari polisi washaanza kusambaza hio story kwamba jamaa alikua mkamuaji wa wake za watu.Jamani!!!Hata iweje basi unafanya usinzi barabarani na unajua unajulikana wewe ni mbunge?Kumbuka pia marehemu wote wawili wana ukoo wa damu.A'fu pia hali ya Kenya ni mbaya na sidhani mtu mwenye akili timamu na anayewakilisha watu Bungeni anaweza kua barabarani,mchana kweupe, akinyemelea wake za watu.Mmmmmhhhhhhhhh!!!!
In this context it also imperative to note that wabunge kadhaa wa upinzani wamepata text mesasage zinazowaambia waachane na wake za watu.Hii ni kwamba wakibwagwa kwa sababu za kisiasa, polisi wataleta hizi story za kuwanyemelea wake za watu.Wabunge wa-ODM walikua wamefanya kikao awali wakilalamika eti masiha yao yanatishiwa na watu wasiowajua. Unadhani nani alikua namba moja kwenye hio listi yao?Huyo bwana aliyebwagwa!Sasa jaza mwenyewe.