TGInnocent
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 1,088
- 582
Tupe ushahidi.wadhamini wa hilo pambano ni kampuni ya kubet williamhill walishapanga matokeo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupe ushahidi.wadhamini wa hilo pambano ni kampuni ya kubet williamhill walishapanga matokeo
Round ya 5 na 11 ndizo babu alizolambishwa sakafu.Duuh huyu myukrane kaona cha moto raundi ya 5 naya12
Mapambano 19kuwa bondia mzuri ni pamoja na kuhimili vishindo vya makonde makali na uwezo wako wa kukepa makonde.....vitu ambavyo Joshua hana.! ....kinachombeba ni uzito wa makonde yake na uwezo wake wa kushambulia mfululizo..!...Klitscho atajilaumu sana kupoteza hili pambano alitakiwa alimalize raundi ile ya tano dogo alishasurrender
mkuu umeongea kishabiki sana ukionesha mahaba yako kwa wlad, ni vyema maana wewe ni mshabiki mkubwa wa wlad na ni kweli kabisa Joshua ana mapungufu mengi na watu huwa wana muita myanyua vyuma anaejua kurusha ngumi kwa kweli ana mapungufu mange na kama unaifuatilia heavy weight division vzr kuna watu wazuri sana ambao huyu wlad akikutana nao sijui kama atatoka salama kuna watoto wenye speed na uwezo mzuri kama Joseph parker japo watu hawa muongelei sana kuna mwenzie izu kuna king kong( Luiz Ortiz) kuna wilder na wengine wengi ambao naamini wana uwezo kuliko huyu Joshua lakini wlad nae ana mapungufu yake na aina ya guard yake anayoitumia akikutana na watu wenye upper cut nzuri hatoboi ila akijirekebisha anaweza kuwa vzr pia mwili wake ni wa asili hivyo ana kazi ya ziada kuhakikisha ana yafanyia mapungufu yake kazi kabla ya rematch kama itakuweo.Awali ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa watanzania wote mlioanza kulifuatilia pambano hili siku 3 zilizopita ama masaa machache kabla ya mpambano kuanza, hivyo kikubwa mlicho kiona kwenu ni kushabikia rangi ya mwili tu.
Niwashukuru pia kwa mayowe makali mliyopiga kutoka kila pande ya jiji la Dar na kuashiria kuwa bado mnamchukia Mzungu ati kisa tu aliwatawala.
Wengi wenu sio wapenzi wa mchezo wa Ndondi kwa sasa na miaka ya hivi karibuni. Wengi wenu hamumjui Wladimir Klitschko na wala hamumjui Antony Joshua...ila tu kwa kuwa mmekuta ndio jambo lililo na kick Duniani basi na nyie mkatumbukia na kushabikia kuliko hata wale mlio wakuta.
Nirudi kwenye pongezi kuu na za pekee ambazo zinakwenda kwa mwana Masumbwi Wladimir Klitschko ambae ndie bondia wa uzito wa juu kipenzi cha wengi Duniani kwa sasa. Bondia huyu mwenye rekodi ya kumiliki mkanda wa Uzito wa juu wa Dunia kwa miaka 9 mfululizo ni bondia bora kabisa ambae ameweza kuusimamisha uzito wa juu wa mchezo huu uwe na heshima. Pongezi hizi kwake ni kitendo chake cha kuomba haraka pambano la marudiano kati yake na bondia mchanga asie na jina wala mashabiki katika kila kona ya Dunia Antony Joshua.
Wladimir Klitschko Usiku wa kuamkia hii leo amepoteza pambano lake dhidi ya bondia huyo aliekuwa anapambana kwenye ardhi ya kwao, huku akishangiliwa na maelfu ya raia wenzie, lakini cha kuchosha zaidi ushindi huo amekwenda kuupata kwenye liuwanja la Mpira, mbaya zaidi ushindi huo wa bahati ameupata huku Wladimir Klitschko akiwa anaongoza kwa pointi nyingi tu.
Kwa kuonesha wazi kuwa yeye ni bora zaidi, bondia Wladimir Klitschko alimtwanga gumi moja takatifu na kufanikisha kumlambisha dogo ardhi ya nchi yake...kwa wanaojuwa masumbwi na kumjuwa Wladimir Klitschko basi ni wazi kabisa tunafahamu kuwa pambano liliishia pale. Ujasiri wa dogo kukomaa na pambano ni kutokana tu na makelele ya raia wenzake ambao waliuvaa uzalendo kabla hata mabondia hawa hawajapimwa uzito.
Katika mapambano machache aliopambana, Bondia huyu Antony Joshua alikuwa akiringa kuwa hajawahi kupigwa jeb mpaka kuanguka chini, lakini rekodi hio kwa sasa hana tena, na amebaki nayo kaka yake Wladimir Klitschko ambae katika kupigana kwake masumbwi kote mpaka alipo stahafu hakuwahi kuangushwa, huyu anajulikana kwa majina Vitali Klitschko ambae alikuwa bingwa wa Dunia wa Uzito wa Juu kwa mikanda yote, kabla ya kuja muachia mdogo wake Wladimir Klitschko.
Kwa watu wanaoujuwa mchezo huu wa masumbwi, sambamba na kumjuwa Wladimir Klitschko tunajuwa nini kitaenda mpata dogo Antony Joshua katika mechi ya marudiano. Mbaya zaidi kwa dogo huyu ni kwamba kama akijidanganya na kukubali kwenda kurudiana na Nguli huyu katika Ardhi ya Marekani ama iwe Madison Square Garden, ama iwe Trump Tower basi ni lazima apokee kipigo ambacho waingereza wenzie hawatakuja kukisahau. Kwenye ardhi ya marekani kuna watu wanaojuwa Ndondi na sio wapiga makelele ambao wengi wao walikuwa walevi na cha msingi kwao ni utaifa.
Namuonea huruma Joshua kama atakubali kusaini kupambana na Wladimir Klitschko katika ukumbi wa MGM Grand uliopo Las Vegas Nevada nchini Marekani, kwani umauti waweza mkuta humohumo.
Katika ukumbi huu wa kihistoria, dogo huyu Joshua atashangiliwa TU atakapo fanya shambulizi la maana mwilini mwa Wladimir Klitschko, kitu ambacho sioni kama kina nafasi siku hio. Dogo anatakiwa ajiulize kwanini bondia Muingereza mwenzie Tyson Furry alikuwa yupo tayari hata kufungwa jela ili tu asirudiane na Klitschko. Furry alijitetea na kukataa katakata kurudiana na bondia huyu na kusema kuwa yeye binafsi anatumia Madawa ya kulevya hivyo hawezi kupigana tena na Wladimir Klitschko .
Katika Ukumbi wa MGM ukumbi ambao Wladimir Klitschko hupendelea zaidi na zaidi kuvaa bukta yake nyekundu na Gloves nyekundu hakuna alietoka akiwa salama, kuna ambao walishindwa kuongea baada ya pambano, kuna walio ng'oka meno, kuna walio vunjwa taya, lakini hakuna ambae alitoka bila kuchanwa usoni na kutolewa damu...
Gang Chomba