Kifupi wanaopotezwa hawana madhara yeyote kwa Taifa, tunatumia nguvu kuubwa Kwa issue ndogo ndogo sana ambazo kudeal nazo unahitaji akili tu.
Hii tabia tukiizoe sana itakwenda mbali sana na kuleta madhara makubwa sana ambayo kuyaondoa itakuwa gharama kubwa sana.
Wahusika wa utekaji wanapaswa kujua wao ndio wanakwenda kuwa hatari kwenye usalama wa nchi, maana kupitia tabia hii tunaweza kuzusha mengine makubwa yanayoweza kuleta madhara makubwa sana.
Kuna siku watekwaji nao watachoka na kuamua kujilinda either kwa kuwalinda targets, au na wao kulipa kisasi.
Ukweli Hali hii ni Mbaya:
1:Wakosefu wapo ,Sheria zipo, taratibu zipo, vyombo vipo kwanini mtu atekwe apotezwe?
2:Akamatwe Kwa Taratibu na kanuni, Sheria ifuate Mkondo ashtakiwe ahukumiwe apate funzo, anauawa atajifunza nini Sasa?
3:Mtu huyu anawazazi, Watoto,ndugu,anategemewa, hao wategemezi hatima Yao nini Sasa?
4:Hivi makosa ya vijana Hawa yanastahili kuuawa kweli? Hakuna hukumu nyingine inawafaa?
5:Hivi Hawa vijana ni tishio kiasi Gani mpka adhabu Yao iwe kutekwa na kupotezwa? Wanataka kupindua nchi? Wanataka kuleta Magaidi? Mbona adhabu hii kubwa sana? Hata makaburi Yao yasionekane?
6:Nahofia siku watu Hawa wataota usugu, watasema liwalo na liwe,watajihami,watajenga visasi,chuki, hasira nk,itatokea nini?
Natamani kabisa turudi kwenye Tanzania yetu ya Amani