Anthony Lusekelo: Tuache nchi ipumue, watu waongee

Anthony Lusekelo: Tuache nchi ipumue, watu waongee

"Kwanini watu wanapotea potea mnaiibua jambo la mganga… Unajua kunakuhamisha upepo watu wachanganyikiwe… "

"Tuache nchi ipumue, watu waongee" amesema Mchungaji Anthony Lusekelo akizungumza tarehe 04 Septemba 2024 na wanahabari kuhusu masuala ya watu mbalimbali kupotea katika siku za hivi karibuni.

View attachment 3087472

- Anthony Lusekelo: Mtu amechana tu picha ya Rais, ametekwa
-
Inategemea unataka wananchi waongee nini .wengine hawajui wanaongea nini na wakati gani.hatuna mifumo ya kuwadhibiti waharifu .tukiwaachia uhuru wa kuropoka tu tutakuwa kama kenya,ukraine ,amerika na kwengineko ambako kama vile america anapigwa risari hadharani.unamchagua mjinga mmoja kama zelensky kuwa raisi.siyo kila kitu tuige kwa mataifa yanayojiita yamestarabika.eg USA ni nchi pekee duniani inasifika kwa kuua marais wakiwa madarakani .
 
Ulishawahi sikia kwenye mkutano kiongozi mkuu akisema mwaka huu tumeiba kura, zaidi ya wale wenye mihemko kama wa ngorongoro. wapinzani ndio wametujaza ujinga kuwa CCM ni wezi wa kura. Mkuu huo ni uongo ulioshikwa na wapinzani, uongo ukinenwa sana huonekana ni ukweli.Lete ushahidi kama ni kweli CCM ni wezi wa kura
Wewe chawa na Nape nani anaijua CCM?
 
Kifupi wanaopotezwa hawana madhara yeyote kwa Taifa, tunatumia nguvu kuubwa Kwa issue ndogo ndogo sana ambazo kudeal nazo unahitaji akili tu.

Hii tabia tukiizoe sana itakwenda mbali sana na kuleta madhara makubwa sana ambayo kuyaondoa itakuwa gharama kubwa sana.

Wahusika wa utekaji wanapaswa kujua wao ndio wanakwenda kuwa hatari kwenye usalama wa nchi, maana kupitia tabia hii tunaweza kuzusha mengine makubwa yanayoweza kuleta madhara makubwa sana.

Kuna siku watekwaji nao watachoka na kuamua kujilinda either kwa kuwalinda targets, au na wao kulipa kisasi.
Ukweli Hali hii ni Mbaya:
1:Wakosefu wapo ,Sheria zipo, taratibu zipo, vyombo vipo kwanini mtu atekwe apotezwe?
2:Akamatwe Kwa Taratibu na kanuni, Sheria ifuate Mkondo ashtakiwe ahukumiwe apate funzo, anauawa atajifunza nini Sasa?
3:Mtu huyu anawazazi, Watoto,ndugu,anategemewa, hao wategemezi hatima Yao nini Sasa?
4:Hivi makosa ya vijana Hawa yanastahili kuuawa kweli? Hakuna hukumu nyingine inawafaa?
5:Hivi Hawa vijana ni tishio kiasi Gani mpka adhabu Yao iwe kutekwa na kupotezwa? Wanataka kupindua nchi? Wanataka kuleta Magaidi? Mbona adhabu hii kubwa sana? Hata makaburi Yao yasionekane?
6:Nahofia siku watu Hawa wataota usugu, watasema liwalo na liwe,watajihami,watajenga visasi,chuki, hasira nk,itatokea nini?
Natamani kabisa turudi kwenye Tanzania yetu ya Amani
 
Back
Top Bottom