PreGE2025 Anthony Mavunde agawa “smartphones” kwa wenyeviti wa mitaa 222

PreGE2025 Anthony Mavunde agawa “smartphones” kwa wenyeviti wa mitaa 222

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Nikiwa nimebakiza siku moja kabla ya kukoma kuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini leo saa 2:30 asubuhi kwenye ukumbi wa Jiji la Dodoma, nitazindua rasmi mfumo wa kidigitali wa kusikiliza kero za wananchi kwa uharaka kwa kupitia serikali ya mtaa.

Hivyo nitauzindua huo mfumo rasmi na kukabidhi simu janja(𝙨𝙢𝙖𝙧𝙩 𝙥𝙝𝙤𝙣𝙚𝙨) kwa wenyeviti 222 wa mitaa yote ya Jimbo la Dodoma Mjini ambapo panapotokea jambo la haraka la kutaka linifikie kwa wakati, mfumo huu utatumika ambapo taarifa kwa haraka ofisini kwa Mkuu wa Wilaya, kwa wasaidizi wangu ofisini kwa Mbunge na kwangu mwenyewe bila hitaji la kupiga simu.

Simu hizi zinatoka kwenye kiwanda cha kutengeneza simu cha Raddy Electronics Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kinachomilikiwa na mtanzania mwenzetu Bw. Ramadhan Mlanzi @raddytanzania

WhatsApp Image 2025-06-26 at 07.17.37.jpeg
 
Alikuwa wap kipindi chote hicho wakati akiwa mbunge kusikiliza kero za wananchi? ndo aje leo kusikiliza kero wakati bado muda mchache ubunge wake ufikie tamati
 
Alikuwa wap kipindi chote hicho wakati akiwa mbunge kusikiliza kero za wananchi? ndo aje leo kusikiliza kero wakati bado muda mchache ubunge wake ufikie tamati
Kipindi chote cha ubunge kuhudum8a wananchi ruksa hata kama imebaki robo saa bunge kuvunjwa
 
Alikuwa wap kipindi chote hicho wakati akiwa mbunge kusikiliza kero za wananchi? ndo aje leo kusikiliza kero wakati bado muda mchache ubunge wake ufikie tamati
Sijui hata jinsi wabunge wanavyofikiri, sema watampa tena
 
Nikiwa nimebakiza siku moja kabla ya kukoma kuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini leo saa 2:30 asubuhi kwenye ukumbi wa Jiji la Dodoma,nitazindua rasmi mfumo wa kidigitali wa kusikiliza kero za wananchi kwa uharaka kwa kupitia serikali ya mtaa.

Hivyo nitauzindua huo mfumo rasmi na kukabidhi simu janja(𝙨𝙢𝙖𝙧𝙩 𝙥𝙝𝙤𝙣𝙚𝙨) kwa wenyeviti 222 wa mitaa yote ya Jimbo la Dodoma Mjini ambapo panapotokea jambo la haraka la kutaka linifikie kwa wakati,mfumo huu utatumika ambapo taarifa kwa haraka ofisini kwa Mkuu wa Wilaya,Kwa wasaidizi wangu ofisini kwa Mbunge na kwangu mwenyewe bila hitaji la kupiga simu.

Simu hizi zinatoka kwenye kiwanda cha kutengeneza simu cha Raddy Electronics Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kinachomilikiwa na mtanzania mwenzetu Bw. Ramadhan Mlanzi @raddytanzania

Kusikiliza ni jambo moja kuzifanyia ni jambo lingine!!
 
Back
Top Bottom