Dah wajameni me kama wiki hivi nakidogo imepita nilikuwa najihisi kichwa kuuma naviungo kuuma nikaenda kwa hsptl kwabahat mbaya nikakuta mtandao wabima unasumbua hivyo sikuweza kupata Huduma ila kutokana namaelezo niliyompatia dokta akanishauri ninunue azuma dozi pamoja napanadol nitumie, nikafanya hivyo nakweli nafuu ikapatikana kidogo ila nilipomaliza dozi nikaanza kuharisha tena kama masihara vile siku yakwanza nikaharisha mara mbili asubuhi nausiku tena choo kingi kile chakupiga kelele nakupumua juu hata mpaka aliyepo njee anasikia siku yapili nikaharisha mara nne uzalendo ukanishinda nikaenda duka ladawa nikawaelezea wakanipatia dawa inaitwa erythromycin nikaanza kuitumia hiyo dawa ila mpaka sasa mabadiliko bado naharisha nikarudi tena pharmacy wakaniambia itakuwa maleria hiyo wakanipa mseto hiyo nijuzi nikaanza kutumia mseto ila chaajabu mpaka hivi sasa nafuu yatumbo bado nambaya zaidi limeanza kuwa linauma nakuuma nawakati mwanzo lilikuwa haliumi ila tu nilikuwa naharisha wajuvi wamambo mnaweza kunisaidia japo kwauzoefu wenu