Antony Joshua Vs Andy Ruiz 2, tukutane hapa kwa updates

Hapa ndio nakumbuka maneno ya Tyson Fury akimzungumzia AJ, nanukuu, " AJ is not a boxer, he is just a body builder," AJ hana skills zozote za boxing zaidi ya kushinda kijanja janja
Kivipi yaani, zile KO 21 zote kashinda kijanjajanja?
 
Hakuna utamu wa ngumi inapendeza kupigana kwa ushindani siyo kurukaruka na kushika kila mara mpaka inachukiza mmexico kacheza vyema tena kwa kujiamini bila kurudi nyuma.
Ukute hujawahi pigana
 
Hawaelewi hawa vijana
Umeandika vizuri mkuu.
Wengi hasa vijana wa leo hawajui huu mchezo wa masumbwi.
Eti Joshua alikuwa akiruka ruka.
Yapo mambo mengi yanayoangaliwa na bondia kuhusu mshindani wake (opponent).
AJ alijua fika kuwa Ruiz ni boxer-puncher na ili upigane naye vzr ni kuweka gap ktkt na kusukuma mbele punches za masafa marefu.
Pia AJ ana advantage ya reach nzuri pia na urefu kidogo dhidi ya mshindani wake Ruiz.
Kwa wale walioangalia pambano la Lennox Lewis na Mike Tyson wanaweza kujua nini nimeandika.
 
Kumshinda Ruiz inakubidi uwe mvumilivu hadi mwisho ili uje uambukie ushindi wa Points tu. Hakuna short cut ya kumshinda Ruiz zaidi ya uvumilivu ili uvute points
AJ angekuwa anajiamini kuhusu pumzi zake zisikate, angeweza kufanya vizuri zaidi kwenye raundi tatu za mwisho kwa ku apply a constant pressures kila anapoona upenyo.
Tatizo ametumia staili ya slugger mwanzo mwisho. Zile KO's ktk game la kwanza labda zilikuwa bado ktk mind yake.
 
Angeweza kumKO sema alikuwa anajihadhari sana
 
 
Ulimsikia yule Mcrotia alivyosema alipoulizwa mbona umempiga mwenzako ngumi za kisogoni ,alijibu "This is war......" Kwa hiyo AJ kushinda kijanja ni mbinu za medani (field craft)
Ni kweli yule Mcrotia baada ya kuulizwa anajisikiaje mpinzani wake kulalamika kumchezea foul kwa kumpiga ngumi nyuma ya kichwa.Mcrotia alijibu hii ni vita mtu unatumia silaha zote ulizonazo.
 
sema AJ angepigwa angepoteza thamani yake yote, alikuwa makini sana
Na alilijua hilo ndio maana akawa anacheza KWA tahadhari sana naona huyo mmarekani-mMexico Ali interrupt interview ya AJ kuomba rematch for the third time,trust me asirudie TENA atapigwa VIBAYA mno,
 
Hii mbinu akitumia kwa Wilder haitafanya kazi.

Wote warefu kwa hiyo ni rahisi ngumi ya Wilder kufika , halafu kingine Wilder kukuvaa haoni hasara.
Wilder pambano la juzi alipoteza round zote hadi ile ngumi ya kichawi ilipoua mtu. Hizo round alizopoteza ingekuwa ni makonde ya Ruiz angepigwa KO.
 
Reactions: rr4
Dillian whyte mtoe huyu JAMAA mzito sana halafu pumzi kisoda
White alishapigwa KO na Joshua, ingawa wapambana vikali mpaka alipootewa round za mwishoni. Ingawa whyte nae alishamshinda Joshua when they were in amateur boxing!
 
White alishapigwa KO na Joshua, ingawa wapambana vikali mpaka alipootewa round za mwishoni. Ingawa whyte nae alishamshinda Joshua when they were in amateur boxing!
Whyte ana ngumi nzito Jana alimtandika sana yule mzungu japokuwa whyte naye pumzi tatizo alikuwa anahema sana
 
MCHEZO WA NGUMI HAUFANYIKI NDANI YA SHUKA tunauona live , hizi mambo mnatuambia kila siku hatujui eti kisa ngumi za kichwa

Tuliwezaje kuwashabikia akina MIKE IRON TYSON?

Ngumi za zamani kweli ndo ngumi halisi wanazotaka mashabiki
Ila kwa upande wa pili ndo ngumi zilizokuwa zinawauwa wapiganaji, mtu akifika miaka 60 au 57 anaanza kuwa zezeta, kutokana na mingumi aliyopigwa ya kutosha, ila kulingana na dunia ilivyobadilika lazima mambo yabadirike, wamegundua kikubwa ni kupata points tu
Antoni ana mikono mirefu, luiz ana mikono mifupi, ili Anton apate advantage ni inabidi kuwe na distance kwake na kwa luiz na ili Luiz apate advantage inabidi aipunguze hyo distance ili apate advantage, na Antoni kutokana na kuwa mikono mirefu hawez kupigana akiwa karibu sana, na ndo kilichokuwa kinafanyika in most of the game, lazima uone Antoni asitake kusogelewa sana na nyie lazima muone anakimbia
 
Ila Fury Ni Sugu Sana, Hata Wilda alichemka kumpiga kwa Knok Out. Linadondoka linaamka linaendelea





Katika ile raundi Wielder alikuwa kisha choka hivyo hakurusha lile konde kwa nguvu zake za siku zote.
 
Bab huwajui wabongo? kila kitu wanajua wao,ukiskia wanavyoongea na kuchambua mambo utasema Loh mbona wataalam ndo hawa sa tunakwama wapi kwenye medani za kimataifa?, kumbe babu nyerere katurishisha tantantalila nyingi kuliko akili alizokufa nazo peke yake....hahahaha
 
Na alilijua hilo ndio maana akawa anacheza KWA tahadhari sana naona huyo mmarekani-mMexico Ali interrupt interview ya AJ kuomba rematch for the third time,trust me asirudie TENA atapigwa VIBAYA mno,
nani atapigwa vibaya mno?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…