Antony Joshua Vs Andy Ruiz 2, tukutane hapa kwa updates


Binafsi naamini AJ atatoka kidedea ingawa mhuni naye hatabiriki na ngumi zake za mfulilizo cha muhimu AJ ajue jinsi ya kumtoka haraka na asiruhusu kabisa kukaa karibu naye la sivyo mhuni atashinda tena
 
Mkuu hii si kweli.
Nilisoma kitambo nahisi ni boxing highlight au boxing guru ndiyo waliisema hii.

Kama unakumbuka kuna kipindi kulikua na joto la hawa kukutana kisha ghafla pakawa kimya.
 
Hali ya Instagram followers leo tar 5, ngoja tuone nani ataongeza followers wengi baada ya pambano lao tar 7
 
Hali ya Instagram followers leo tar 5, ngoja tuone nani ataongeza followers wengi baada ya pambano lao tar 7View attachment 1282371

floydmayweather
Verified



Floyd Mayweather

www.mayweatherpromotions.com


Mayweather anapigana kwa uzito wa chini ni vipi ana followers wengi kuliko hii miamba ya Heavy weight? halafu pia nimeshangaa kuona kuwa katika ma boxer tajiri duniani huyu bwana ni namba moja na AJ anashika namba 11 je hapo kuna science gani?
 
Size doesn't matter, huko chini kuna wapiganaji wengi wazuri kuliko heavyweight ambayo ina majina machache yenye ubora ndio maana kilasiku tunawasikia kina Wilder,AJ na Fury. Zamani ndio kulikuwa na mambo hayo kwamba mabondia waliokuwa wakitupiwa jicho ni wa uzito wa juu, ila baada ya kizazi cha kina Mike Tyson kupita ikaonekana kwenye uzito wa juu hakukuwa na mabondia wazuri/wenye ushawishi kwa kipindi kirefu, hivyo attention ya wadau na mashabiki ikahamia kwenye uzito wa chini, ndipo kina Mayweather ambao walionekana kuwa bora walipojivunia mashabiki. Ila hata AJ ana potential ya kupiga hela na kujivunia mashabiki kama Mayweather au kuzidi, coz hadi sasa kacheza mapambano 23 tu na umri bado unaruhusu, ila hilo litatokea kama atatengeneza rekodi nzuri, kashapata loss mapema, wakati Mayweather kamaliza career yake na 50-0
 
vipik2 Halafu kwa sasa bondia wa uzito wa kati 'Canelo' ndio ana mkataba wa pesa ndefu kuliko mwanamichezo yeyote, hapo inaonesha kwamba size doesn't matter, ni jinsi tu unavyoweza kutengeneza ushawishi ulingoni. Hata kule UFC (MMA) majina yanayotamba ni kama Khabib, Mc Gregor, Masvidal, Diaz, n.k ambapo wote hao ni uzito wa chini
 
vipik2 Halafu kwa sasa bondia wa uzito wa kati 'Canelo' ndio ana mkataba wa pesa ndefu kuliko mwanamichezo yeyote, hapo inaonesha kwamba size doesn't matter, ni jinsi tu unavyoweza kutengeneza ushawishi ulingoni

Asante mkuu, turudi kwenye jambo la muda wa mtanange ni saa ngapi kwani hata Azam wanatoa tu tangazo kuwa watatangaza kwa channel 126 lakini hawasemi ni kuanzia saa ngapi na haijulikani kama mapambano mengine/undercard kama wataonyesha halafu hiyo channel 126 sijui ipo kwenye bando lao la shillingi ngapi
 
Bando la 18,000. Muda ni kuanzia saa1 jioni kama sijakosea, channel no123
 
Swali la kijinga sana.

Nilipokuwa shule nilifundishwa kupinga hoja kwa hoja sio kupinga tu halafu huweki hoja yako hiyo inakuwa sawa na malaya akipewa pesa basi yeye chochote kwake ni ndiyo hajiulizi hata mengine yatokanayo. Lete werevu wako watu waelimike
 
Nilichojifunza kwenye boxing, ni kwamba sio kurusha rusha ngumi kama unacheza ngoma, unaweza rusha ngumi chache zenye point na ukashinda, bwana bonge ruiz kutoka mexico, ni mjanja sana nimecheki clip zake za mazoezi pamoja a interview zake jamaa anajijua aki fight kwa kukamia atawi kuchoka na kumpa nafasi AJ ushindi mrahisi, kwa upande wa bwamdogo AJ yeye kitakachomgharimu ni kuigia uwanjani na matokeo hilo tuu, kwa upande wangu natamani Ruiz ashinde hili pambano
 

Ni kweli ulivyosema na ukiangalia kwa namna fulani AJ anacheza akiwa ameweka akiba la kono la kulia ili kumaliza mchezo saa yoyote pale akipata mpenyo yaani sawa tu na Wilder anavyofanya, sasa mhuni Ruiz yeye hatari hiyo anaijua vyema na anachokifanya ni kumweka busy all the time kwa kuwa karibu yake ili ku destruct plan zake na pakitokea chance ndipo anampa za masikioni mpaka centre of gravity inapotea, napenda sana AJ ashinde ingawa ni kama Ngamia kupita kwenye tundu la sindano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…