Antony Joshua Vs. Joseph Parker 31/03/2018 [Special Thread]

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,551
Reaction score
1,777
Wakuu kumekucha , yule mbabe wa Dunia wa Ngumi za kulipwa uzani wa juu ( Heavywheight Champion) Bondia Antony Joshua a.ka. AJ amepata challenge kutoka kwa Bondia Joseph Parker (New Zealand) na leo hii wamefanya Press Conference kuthibitisha utayari wao wakutwangana masumbi. Pambano kufanyika tarehe 31/03/2018 huko Cardiff Uingereza.

Haya sasa huku Team [HASHTAG]#Ajboxing[/HASHTAG] kule [HASHTAG]#TeamParker[/HASHTAG]

Karibuni
Video_20180117142227510_by_1259312109.jpg
Video_20180117142227510_by_1038582310.jpg
Video_20180117142227510_by_597657405.jpg

Hivi unajua Lenox Lewis alipigwa na Oliver Mc Call na Rasim Rahman ambao hawakuwa maarufu kwenye ngumi?
Marudio na Oliver Mc Call unayakumbuka? Unajua nani aligeuka chizi baada ya vinu kumkolea?

Rahman alishinda pambano la kwanza Lewis alikua anajiamini mno hata Rahman kushinda ilikua confidence imemponza Lewis alikua anamfuata tu jamaa anamtegea ampe punch left jab.

Pambano la pili unalikumbuka?
 
Kwa Vitali aliponea chupuchupu huyu bondia wako alikuwa very defensive na mviziaji tu!
Hahahaha huo uviziaji na defensive ndiyo ulisababisha George Foreman aokoke siku alipokutana na Jimmy Young, na Foreman alikua very accomplished boxer ila usiku ule akaamua kuokoka.

Hapo unamzungumzia bondia ambaye Tyson akiwa kwenye kilele chake aliambiwa apigane naye akajibu kwa ukali "Nenda ukapigane naye wewe"
 
Nakataa hakuponea chupuchupu. Lile ni moja kati ya mapambano makali kuwahi kutokea kwa kipindi hiki. Kila mmoja alipigana vizuri na mshindi alistahili.
 
Marudio na Oliver Mc Call unayakumbuka? Unajua nani aligeuka chizi baada ya vinu kumkolea?

Rahman alishinda pambano la kwanza Lewis alikua anajiamini mno hata Rahman kushinda ilikua confidence imemponza Lewis alikua anamfuata tu jamaa anamtegea ampe punch left jab.

Pambano la pili unalikumbuka?

Your Lennox had a glass chin! Pamoja na kupoteza mapambano mawili tu bado anazidiwa umaarufu na mabondia waliopoteza 5+ kwa sababu ya style yake ya kupigana.
 
Nakataa hakuponea chupuchupu. Lile ni moja kati ya mapambano makali kuwahi kutokea kwa kipindi hiki. Kila mmoja alipigana vizuri na mshindi alistahili.
Kaangalie tena hilo pambano halafu uniambie kama Lewis alipigana comfortably!!!
 
Your Lennox had a glass chin! Pamoja na kupoteza mapambano mawili tu bado anazidiwa umaarufu na mabondia waliopoteza 5+ kwa sababu ya style yake ya kupigana.
Glass chin?

Evander chali

Tyson chali

Klitschko chali

Glass Chin? Upo serious?
 
Hahahaha huo uviziaji na defensive ndiyo ulisababisha George Foreman aokoke siku alipokutana na Jimmy Young, na Foreman alikua very accomplished boxer ila usiku ule akaamua kuokoka.

Hapo unamzungumzia bondia ambaye Tyson akiwa kwenye kilele chake aliambiwa apigane naye akajibu kwa ukali "Nenda ukapigane naye wewe"
Hata Mywether kila siku anashinda kwa staili yake hiyo hiyo ya kupaki basi
 
Back
Top Bottom