ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Hayo ndio yamejiri huko Mererani Wakati Waziri wa Madini bwana Antony Mavunde akizindua Mnada wa mauzo ya Madini ya Vito kwenye Jengo jipya lilojengwa na Serikali maarufu kama Magufuli House.
Bwana Mavunde bila kueleza sababu za serikali kunyachukua Madini kutoka kwa wafanyabiashara mwaka 2017, amesema Serikali itayarejesha Madini Yao na kwamba yamehifadhiwa BoT.
==
Waziri wa Madini Anthony Mavunde amewaondoa hofu wafanyabiasha wa madini kuwa serikali haina mpango wa kuchukua madini yao yatakayobaki katika minada.
Mavunde amesema kumekuwa na dhana potofu kuwa serikali ilichukua madini ya wafanyabiasha katika minada iliyofanyika mwaka 2017 na kutoa ufafanuzi kuwa madini hayo yamehifadhiwa Benki Mkuu na wakati wowote wenye madini hayo wataitwa na kukabidhiwa.
Akizindua minada ya ndani ya madini ya vito Disemba 14 Mirerani, Manyara, Mavunde amesema minada hiyo inaendeshwa na Tume ya Madini kwa kushirikiana na TMX kupitia mfumo wa kielektroniki ili kuweka uwazi.
Ameeleza kuwa sekta ya madini imekua, ikiongeza mapato ya serikali kutoka shilingi bilioni 161 (2015/16) hadi bilioni 753, na inalenga kufikia trilioni moja ifikapo 2024/25, akisisitiza udhibiti mzuri wa serikali katika sekta hiyo.
"Pia niwahakikishie kuwa hakuna madini ya mtu yatakayobaki baada ya minada kumalizika yatachukuliwa na serikali, na hata yale madini yaliyobaki mwenye mnada wa mwaka 2017 yapo BoT na wakati wowote wahusika wataitwa kukabidhiwa madini yao"
Swali: Kwa nini Serikali ilinyakua Madini ya wafanyabiashara mwaka 2017?