Antony Mtaka aambiwe kwamba sera ya elimu ni ya kitaifa na siyo mkoa kwa mkoa

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
762
Reaction score
1,236
Bila hata kujua kiwango cha elimu ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, mara moja naona makosa ya kiutendaji aliyonayo. Kwanza, yaonekana ni mtu asiyejua kuchagua maneno. Pili, hakujua mchakato upi uboreshe kiwango cha elimu mkoani kwake, siyo ufaulu anaotafuta. Elimu inaendeshwa kitaifa na siyo ki-mkoa.

Haiingii akilini kwamba mkuu wa mkoa anataka kuboresha ufaulu wa wanafunzi kwa kupambana na waziri wa elimu, kwa makambi ya elimu. Ili iweje?

Elimu ni mchakato wa miaka 7 kwa shule za msingi, miaka 4 sekondari, n.k. Kama kuna uzembe ktk miaka ya elimu, Mtaka anawezaje kuboresha uzembe huo kwa makambi ya miezi miwili? Yaani sasa hivi aanze, kufika septemba darasa la 7 wafaulu mtihani. Ni elimu gani hiyo?

Sera ya elimu ipo ili kudhibiti mawazo mfu kama haya ya akina Mtaka.
 
Ni la kitaifa wakati watoto wenu wanasoma Canada na International school, au unaongelea taifa gani.....
Hata watoto wake hawako shule za kata, kwa hiyo usimpe ubora na ushujaa mshenzi huo!
 
Bila hata kujua kiwango cha elimu ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, mara moja naona makosa ya kiutendaji aliyonayo. Kwanza, yaonekana ni mtu asiyejua kuchagua maneno. Pili, hakujua mchakato upi uboreshe kiwango cha elimu mkoani kwake, siyo ufaulu anaotafuta. Elimu inaendeshwa kitaifa na siyo ki-mkoa.

Haiingii akilini kwamba mkuu wa mkoa anataka kuboresha ufaulu wa wanafunzi kwa kupambana na waziri wa elimu, kwa makambi ya elimu. Ili iweje?

Elimu ni mchakato wa miaka 7 kwa shule za msingi, miaka 4 sekondari, n.k. Kama kuna uzembe ktk miaka ya elimu, Mtaka anawezaje kuboresha uzembe huo kwa makambi ya miezi miwili? Yaani sasa hivi aanze, kufika septemba darasa la 7 wafaulu mtihani. Ni elimu gani hiyo?

Sera ya elimu ipo ili kudhibiti mawazo mfu kama haya ya akina Mtaka.

Mkuu unafahamu maana ya SERA.
Unafahamu kuwa Usimamizi wa uendeshaji wa Shule za Msingi upo Chini ya TAMISEMI?
Unafahamu kuwa TAMISEMI kimkoa inaongozwa na Mkuu wa Mkoa

Unafahamu pia majukumu ya kuhakikisha Ufauku katika shule za msingi mkoa ni la Tamisemi?

Suala la ratiba ya kutoka limewekwa na wizara ya Elimu , Lakini suala extra time au makambi kwa madarasa ya mitihani si Suala la kisera mkuu, Ni suala la Mikakati ya Ufaulu ndani ya mkoa.Kama halileti shida Wizara ya elimu haipaswi kuintervine sababu linaihusu TAMISEMI.

Woengi tunasahau kuwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa ipo chini ya TAMISEMI kimkoa. Nilitegemea Ummy Mwalimu kuliingilia hili si Ndalichako sababu suala la uendeshaji wa Shule za Msingi ni ka TANISEMI

Tutafute maana ya SERA ya elimu kwanza ndo turudi
 
Umeongea vema sana mkuu, watu wengi akiwepo Mtaka suala la national curriculum hawalielewi wanaendeshwa kwa miemko na kukosa busara tu.
Waziri wa elimu yuko sahihi 100% na bado katumia busara kutokurupuka kumjibu mkuu wa mkoa.
Hawa watoto tunawatesa sana kwa overdose,hii ni brain masturbation kwa watoto na haikubaliki kitaaluma!
 
Hawa wapumbafu wanataka watu wakupakia kwenye malori na kwenda kukatika kwenye mikutano yao.
Kuna factors nyingi sana za kufeli na kufaulu,eg. Mtoto kama hana malezi bora nyumbani na afuatilii masomo tangu std 1,ata aongezewe muda hawezi kufaulu
 
Kosa la mtaka ni nn sasa? Maana sera ya elimu kitaifa ni kufaulu mitihani. Mtaka amekuja na mbinu ya kufaulu hio mitihan. Ww unakataa, kwa nn sasa?
Sera haiko ivyo mkuu,sera ni ya kitaifa sio juhudi za mkuu wa mkoa,RC anapaswa afanye kazi kwa kufuata sera za taifa, hakuna sera za kielimu kimkoa maana ikiwa ivyo basi kila mkoa uwe mamlaka kamili inayojitegemea aka serikali za majimbo
 
Yap, kwanza makambi ya kitaaluma ni mizigo tu kwa wazazi, wazazi wanatozwa pesa kubwa lkn ufanisi wake ni minor, wakuu wanapiga hela sana kupitia hayo makambi.
Ok sasa nimeelewa,kumbe ni suala la kimaslahi!
Sasa namuelewa RC,ovyo kabisa!
 
Mkuu unafahamu maana ya SERA.
Unafahamu kuwa Usimamizi wa uendeshaji wa Shule za Msingi upo Chini ya TAMISEMI?
Unafahamu kuwa TAMISEMI kimkoa inaongozwa na Mkuu wa Mkoa

Unafahamu pia majukumu ya kuhakikisha Ufauku katika shule za msingi mkoa ni la Tamisemi?

Suala la ratiba ya kutoka limewekwa na wizara ya Elimu , Lakini suala extra time au makambi kwa madarasa ya mitihani si Suala la kisera mkuu, Ni suala la Mikakati ya Ufaulu ndani ya mkoa.Kama halileti shida Wizara ya elimu haipaswi kuintervine sababu linaihusu TAMISEMI.

Woengi tunasahau kuwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa ipo chini ya TAMISEMI kimkoa. Nilitegemea Ummy Mwalimu kuliingilia hili si Ndalichako sababu suala la uendeshaji wa Shule za Msingi ni ka TANISEMI

Tutafute maana ya SERA ya elimu kwanza ndo turudi
Naona umefafanua mamlaka ya tawala za kimkoa tu haujaeleza kuhusu sera. UKIELEWA maana ya national curriculum itakusaidia sana kujua jinsi RC alivyoropoka kimakosa.
Kwa kifupi RCs wanatakiwa kutekeleza sera za wizara,juhudi za mkoa sio kuharibu ratiba ya wizara kisera,eg.km sera na taratibu ni kukaa darasani masaa 8, juhudi ya mkoa ni kufanikisha mtoto anakaa hayo masaa sio kumuongezea masaa ni kuharibu taratibu zilizowekwa na wizara.
 
Back
Top Bottom