Antony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na ya Nebukadneza Mfalme wa Babel

desmond3076

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
279
Reaction score
184
Jana nilifatilia kongamano la usalama la mkuu wa mkoa wa Dodoma maeneo ya s/m kisasa, mkutano huu ulikuwa mbashara TBC TAIFA, kilichoniskitisha ni kupigwa marufuku kwa mapambio ya kumsifu Mungu wakati wa mikesha usiku, nimeskitika Sana , niseme huo ni ushetani, Mungu wetu hana mipaka katika kuabudiwa .

Hii ni kwa wote hata kwa ndugu zetu waislamu, maana Kuna mida ya kuabudu mpaka swala tano na ZINAENDA Hadi usiku.

Nchii inayo Uhuru wa kuabudu pasipokuingiliwa na serikari naona ANGUKO LA MTAKA LITAKUWA KUBWA KAMA ANGUKO LA NEBUKADNEZA MFALME WA BABELI.

Niseme Mungu apingwi na Kuna mashekh na manabii wenye nguvu , wakimlilia Mungu wao sidhani Kama atabaki salama.

Mheshimiwa MTAKA ajue kabisa " yupo anayeweka wafalme na kuuzuru wafalme, na yeye humuweka na kumuondoa amtakae" kwa hio aache watu wamsifu MUNGU, Maana wakuabidiwa ni Mungu pekee.

Hivyo Mungu mwenyewe anasema " aliyevaa asijisifu Kama avuae," yasije yakampata Kama ya senekaribu , acha watu wamuimbie Mungu wao na ndicho kilichobaki.

Maisha YENYEWE mafupi haya

Mbarikiwe.
 
Mathayo 6:5-15

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.

Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
 
Mahusiano yako na Mungu wako yakigeuka kero kwa Binadamu wenzako, tayari unajichotea dhambi..

Ina maana M/Mungu ni kiziwi mpaka umwombe kwa Makelele?
Lakini biblia inasema sikio lake si kiziwi, but hua lazima kwenye maombi Ni mzuka , ndio maana yule bwana yeye akaamua kupiga hema zake pale kawe hataki shida .Sasa sisi huku mbeya jamani kila Kona makanisa mi naona Ni mzuka tu
 
Subiri watetezi wa Mtaka ndio mkuu wa mkoa bora waje wakupe makavu ila kuweka mipaka ya kumuabudu Mungu ni kumkosea Mungu.

Biblia inasema Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu watu wengi walikutanika kumlaki huku wakiimba HOSANA HOSANA mpaka makuhani wakakasirika wakamwambia awanyamazishe naye Yesu akasema "watu hawa wakinyamaza basi hata mawe yatazungumza", hii inaonesha ni namna gani utukufu wa Mungu ulivyo wa ajabu kwa wamsifuye na kumuabudu
 
Hayo maamuzi nadhani ni ya kukurupuka,angeangalia ni wapi kwa kukataza na wapi kuruhusiwe,akizungumzia general tu atakuwa anakosea sana kwani kuna makanisa mengine yako mbali na nyumba za watu sasa hilo katazo haoni kwamba linawagusa na wasio husika...
 
Hapa nimekukubali mkuu kabisa
 
Subiri watetezi wa Mtaka ndio mkuu wa mkoa bora waje wakupe makavu ila kuweka mipaka ya kumuabudu Mungu ni kumkosea Mungu...
Kabisa maana maandiko yanasema hata wakinyamaza Hawa mawe yatapiga kelele.

Hivi unadhani zilikuwa Ni kelele za Aina gani mpaka yerusalemu yote ikatkiska?
 
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi...
Ubarikiwe sana Mtumishi, hii ndiyo inatakiwa na siyo kuweka maspika makubwa makubwa
 
Ashukuru Mungu watu wanamtaja tofauti na wangeenda kwa waganga!
 
Hao

Hao mashekh na wachungaji wenye nguvu walikuwa wapi wakati Maghu anaua watu?mbona "hawakumlilia"Mungu aepushe majanga?
Lakini hatuwezi fahamu maana tunaona MUNGU mwenyewe aliamua kubadilisha utawala kwa kumchukua bwana yule
 
Subiri watetezi wa Mtaka ndio mkuu wa mkoa bora waje wakupe makavu ila kuweka mipaka ya kumuabudu Mungu ni kumkosea Mungu...
Tatizo mikelele ya mispika na lugha za ajabu ajabu usiku mzima bila kuzingatia wazee, wagonjwa, watoto, watu kuchoka kwa majukumu n.k. Tungekuwa tunaabudu kwa ustaarabu bila fujo usiku mzima kusingekuwa na tatizo.
 
Tatizo mikele usiku mzima. Spika kubwa, lugha za ajabu ajabu n.k.

Asiishie hapo tu, amulike mpaka kumbi za starehe na baa.Nazo ni full vurugu/kelele na uvunjifu wa maadili.
 
Kwa hiyo this is the beginning of the fall?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…