Anuani za makazi zilibajetiwa kutumia Bilioni 740 zimeshushwa hadi Bilioni 28

Anuani za makazi zilibajetiwa kutumia Bilioni 740 zimeshushwa hadi Bilioni 28

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa Idara ya Habari maelezo amesema zoezi la Anuani za makazi zilipangwa kutumia Tsh. Bilioni 740 lakini Rais Samia aliishusha hadi Tsh. Bilioni 28.

Kutokana na bajeti wananchi wametakiwa kuchangia baadhi ya huduma ikiwemo huduma ya kuwekewa vibao ambapo tafiti zimeonesha wananchi wanalipia kuanzia Tsh. 1500 hadi 7000 kwa baadhi ya maeneo ili kuchangia bajeti iliyofemea.

Msigwa amesema utaratibu wa watu kulipia unatokana na sheria ya Mtaa kifungu cha 20 na 21.

Kwa hiyo wananchi acheni woga lipeni.
 
huku vijijini kuna anuani za ujenzi.

Mana hata sehemu ya biashara imehesabiwa kama makaz.


Wenda wameona mfali
 
Mkuu wa Idara ya Habari maelezo amesema zoezi la Anuani za makazi zilipangwa kutumia Tsh. Bilioni 740 lakini Rais Samia aliishusha hadi Tsh. Bilioni 28...
Hiyo bil 28 pia haikufika .nadhani ilikuwa bilion 2.8 tu. Kwa namna watu walivyolipwa au hizo bil 28 zilipigwa juu kwa juu

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Kama hivi, eneo moja ila majina mawili tofauti
20220526_131703.jpg
 
Kuna haja ya wananchi kuelimishwa kuhusu umuhimu wa hivyo vibao vya nyumba na mtaa kwa maana yeye ananufaika vipi na hivyo vibao lakini pia serikali ingesema bei ya vibao ni kiasi kwa nchi nzima au mkoa mzima wananchi wengi wanasita kulipia hivyo vibao kwa kuwa tu anasikia sehemu nyingine vibao ni nafuu kuliko sehemu alipo kwa mfano sehemu nayoishi kibao cha nyumba ni Tsh 8,000 na cha mtaa ni Tsh 150,000 ila kuna sehemu niliona kibao cha nyumba ni Tsh 4,000 na cha mtaa ni Tsh 140,000 hii inaleta ukakasi ikiwa vibao vyote materials ni sawa iweje vitofautiane bei!
 
Kwa nini wasitoe bei elekezi kwa nchi nzima ili kuondoa ukakasi usio wa lazima, na ni kwa nini wanatoa risiti ya mkono badala ya efd
 
Back
Top Bottom