ANUNNAKI: Nadharia za Mungu, miungu, fumbo la sciencenscience na Teknolojia kubwa katika Dunia ya kale, kuanguka Kwa civilization na kuinuka Tena

Anunnak walipokuja duniani kulikuwa hakuna binadamu/watu kabisa katika uso wa dunia au kulikuwa na watu ila wakaja kuumba binadamu.

Maana kuna nadharia inasema watu na binadamu ni tofauti mpaka Leo hii miongoni mwetu kuna watu ambao ni originals wa dunia hii na kuna binadamu ambao ni cloned human beings.

Na kama walikuta hakuna watu/binadamu walikuta kuna viumbe vingine tuvijuavyo yaani kama samaki,nyoka,wanyama wa porini na wakufugwa na mimea yote hii tuionayo(re:biology:zoology and botany)
Au wao hawakukuta chochote walianza kazi ya uumbaji wa vyote hivyo mpaka ku clone huyo binaadamu?

Au la ndio kusema hao anunnak ndio Mungu sasa?
Mbona confusion ni nyingi sana.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Swali zuri Mkuu,Katika Epic of Girgamesh Annunak walimkuta kiumbe Primitive aitwaye Enkidu,
Maandiko ya Sumeria yanaweka wazi kuwa huyo kiumbe Alikua na manyoya mwilini mwake akiwa na mfanano na mtu ila si timifu,alikula majani kama hayawani wengine,Hana ufahamu wowote na hucheza Katika bustani ya kumwagilia akiwalinda wenzake wasishambuliwe na Alliens,
Hapa tunaona Annunaki waliwakuta primitive na waliwaongozea uwezo Ili wawe genre ya Homo sapiens!
 
Dumas the terrible:kwa hiyo wewe binafsi unajua au unaamini nini na baada ya Kifo chako nini kitafuata?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app

Mkuu usijidanganye kwamba ukifa kuna sehem utaenda. UKIFA UMEISHA!!! MWISHO WA BINADAMU NI KIFO.

Hata huyo Adam na Eva mnaoaminishwa ni binadam wa kwanza kuumbwa BADO WAPO KABURINI.

Kama wadudu,wanyama na ndege wanavyokufa na kuisha ndivyo na mwanadamu akifa anaisha.

Ukijaaliwa kuiishi miaka 100 ukiwa hai utaenda kuwa kwenye udongo infinity namba of years there
 
Ufinyu wa uelewa wetu juu ya Annunaki unasababishwa na kwa kiwango kikubwa nyie wachungaji ama makuhani wa Annunaki kutokuwa na uelewa wa kutosha wa jinsi ya kutuhubiria juu ya Annunaki! Pengine ndiyo maana unasema Annunaki alikuwepo kabla ya Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo! Swali langu kilichomtoa kwenye ramani ni nini?

Umezungumza juu ya ukongwe wa Annunaki, nadhani ni mkongwe kwenu nyie mnayemjua!!! Binafsi nimeanza kumjua Mungu wa Ibrahim toka miaka ya themanini na nimekuja kumjua Annunaki hivi sasa kupitia JF!! Kwangu mimi mkongwe ni Mungu Ibrahim!! Huyu wa kwako kwa kweli simjui na maelezo yake yananichanganya! Kwa kifupi simuelewi, sidhani kama nitamuelewa!

Haya, kilichopelekea kina Ibrahim kumkataa Annunaki na kuungana na YAHWE ni nini? Waligundua nini juu ya Annunaki?

Nadhani, makuhani wa Annunaki mkasome mbinu za kumhubiri Annunaki!!
 
hao annunaki waliwatuma wapelelezi wazunguke kwenye sayari mbalimbali"

naimani hizo sayari na hata hayo madini(dhahabu) kuna nguvu iliyozitengeneza kabla na iyo nguvu ndo mungu mwenyewe sasa.
 
Upo na Low IQ Broo believe me,wapi nilipodai Annunaki walikua Mungu na Wana makuhani?

Habari za Annunaki ziligeuka za kiimani Katika Sumeria ya kale sababu watu waliwahusudu kama miungu ila kiuhalisia walikua ni Viumbe kutoka angani au mbinguni walioshuka duniani wakitoka space,

Kutokana na teknolojia Yao kubwa Sana Katika science and technology waliweza fanya mambo mengi makubwa Katika Dunia ya kale ikiwepo kuwaumba binadamu Kwa mfano wao Ili awe kijakazi wa kuchimba dhahabu,

Pia unapodai Mungu wa Ibrahimu,Isaka na Yakobo unamzungumzia
Elohim/Elojim/ YHW
Huyo Alikua ni Mkuu wa Annunaki anayetawala Nibiru au 12th Planet,
Pia mtawala wa Mwanzo wa 12th Planet aliitwa ANU na mkewe KI ambaye ndie baba wa waanak wote huyo Alikua ndie MTANGULIZI mwenye nguvu aliyeibadirisha sayari Yao iliyoharibiwa na vita vya Mbinguni au Galactic civilizations Kwa kuwatuma wanae wafuate dhahabu duniani itakayotumika kurecover atmosphere ya sayari Yao Nibiru,

Kitu kingine ambacho Naona unafanya makosa ni kumtaja Mungu ambaye hata humjui ila umekaririshwa tu,
Narudia Tena
Hapa kwa msisitizo
"Nadharia za Mungu/Miungu ilianzishwa na ANUNNAKI Kwa mara ya kwanza Duniani Katika Pantheons ya Sumeria huko Mesopotamia,
Na Hii ndio maana ya Mungu ambaye Hilo jina linawakilisha cheo Cha mtawala wa Nibiru au 12th Planet (mbinguni)

MUNGU - Master of High Chamber
Katika accient tablets master of high chamber Alikua anaitwa
'ANU'
Alikua na mke anaitwa
'KI'
ANU NA KI walikua na watoto kama ENKI, ENLIL, INNANA, UTU,NIKURASAGI,ISHTAR nk

Kumbuka Nibiru ni Intelligence planet Yenye jamii za viumbe High Advanced Katika science and technology kiasi kwamba haielezski Katika Hali ya kawaida wao huendesha mawazo ya juu na chini ya hisabati,Biolojia na Physikia Katika kiwango kikubwa Toka Hapo kale sana Katika historia ya Ulimwengu,

Mwanzo wao kuja Duniani walishuka na Spaceship/UFO's kubwa Sana na waliweza Jenga majengo makubwa yenye Uhandisi wenye Physics kubwa
Mfano wa hayo majengo yapo Mpaka Leo
Hizo ndizo Pyramids tatu kubwa za Giza,Grand Ziggurat of Uru,
Pyramids za Mexico kama Cholula,Inca,machupichu, temple of condor,great stone of Costa Rica, Stonehenge,Rama setu bridge Tamil Nadu India, Angkor wat kambodia,
Pia Annunaki waliacha magofu ya machimbo ya kale ya Dhahabu kule South Africa,Maputo msumbiji,Kush,Grand Canyon Marekani vile vile waliacha secret Accient Mining nyingi Sana Moja wapo ambazo zimefichika na hamtakaa mjue
Hapa Tanzania ipo
GAMBOSH
Najua mtastaajabu
Ila ni kitu Cha kushangaza Sana pia Kuna Underground tunnels nyingi Sana chini ya bahari pamojaa na miji iliyozama kipindi Cha Deluge!
 
hao annunaki waliwatuma wapelelezi wazunguke kwenye sayari mbalimbali"

naimani hizo sayari na hata hayo madini(dhahabu) kuna nguvu iliyozitengeneza kabla na iyo nguvu ndo mungu mwenyewe sasa.
usipende kulazimisha maswali magumu yajibiwe Kwa majibu mepesi
Una ushahidi juu ya huyo Mungu?
 
Huu uzi umeshawahi kuletwa humu.
Tumewajadili Sana Annunak na kumuumba Mtu Katika Uzi wa Artificial intelligence hapa huu Uzi ni mwendelezo tu juu ya Annunaki sababu nimeona watu wengi hawana ufahamu kuwahusu,lengo ni kuwafundisha binadamu wa Leo juu ya historia ya Dunia iliyofichwa Kwa muda mrefu Sana Kwa sababu mbali mbali either ajenda za Siri au ujinga na ukosefu wa exposure na maarifa juu mambo mengi,Pia kulingana na ukuaji wa science and technology watafiti wengi wa mambo kale wanazidi gundua maajabu ya Accient civilization na kujibu maswali magumu

Mfano zamani kwenye mawe na majengo ya kale kulikua na michoro ya UFO, Spaceships na viumbe vyenye mabawa mawili mapaka miaka ya 1800's binadamu hakujua kile ni Nini baada ya ugunduzi wa spacecraft ndio binadamu wa Leo tukajua kumbe Ile michoro ikiwaonesha Annunaki wakiwa na wings pamoja na vyombo vyao UFO Spaceships ndio tunagundua kumbe Hapo zamani za kale palikua na ustaarabu mkubwa kushinda wa kwetu!

Watafiti wanabaki na mshangao vile vile majengo kama Pyramids za Giza walidai ni Makaburi ya Pharaohs baada ya ugunduzi wa New World kule mexico,Peru,Costa Rica na Mesoamerica kiujumla wakazikuta kubwa na nyingi Sana Ndipo wakajiuliza je na haya ni Makaburi ya Pharao Gani?

Hapo Ndipo utafiti ukaanza fanyika Inakuaje utamaduni wa kale Katika Dunia nzima ufanane?
Na hapo tunaambiwa watu wa kale walikua duni Katika science and technology maajabu tunaona Kazi ambazo zinaacha utata mkubwa yaani majengo Yana miaka zaidi ya 15000 BCE hayana hata ufa na nimakubwa yaliyojengwa Kwa mawe ya miamba iliyochongwa Kwa kukatwa Kwa shape wakati Leo hatuna teknolojia hiyo hujiulizi tu nani kafanya?
 
Kwahyo Anunaki sio Mungu ila wanaumba binadamu kwa Advanced tech waliyonayo right?


Ila same advanced tech haiwez kuumba dhahabu wakatengeneza hkohko Nibiru? Hiyo advanced tech inashindwa tengeneza machine za kuchimba dhahabu Ila wanaingia gharama za kuumba mwanadam?


Hawa viumbe wenye advanced tech ambao wanajali Sana mazingira ya Nibiru walishindwa kuwa na proper exit strategy baada ya kuchimba dhahabu mpaka wagombane wao kwa wao na kususa kuamua kumwacha mwanadam?


Unajaribu kuonesha Mungu hayupo ila Imani na dhana ya kiwepo na kiumbe au cheo cha Uungu ilianza enz za hao Anunaki,

Swali, Nan aliyetengeneza sayari? Nan aliyetengeneza Nibiru na dhahabu? Tujuze kwanini watu tunakufa? Nadharia ya shetan ilianzia wapi na lini?


Mkuu una uhakika umesoma vyema hii habari? Na una uhakika umeyasoma haya tuliyokaririshwa vyema kiasi cha kuweza kuyachallenge ukilinganisha na hao Anunaki?
 
Enlil ndiye Mungu wa anga aliyekuja na slogan ya heaven aand earth ambayo baadaye Quran ikaja kuiandika upya halafu kongole imeenda kwa allah
 
kuhusu ANNUNAKI kumuumba Binadamu ni Moja ya advanced science waliyokuwanayo Annunaki,
Wewe kinachokushangaza ni kuumba Mtu badala ya kuumba mashine Hivi hujui Kutokana na wao kua advanced Mtu nae ni mashine ya Kazi Katika migodi Yao na ni Moja ya taknolojia kubwa sana kwao?

Pia swali lako la pili linanishangaza unashangaa Anunnaki kumuumba Mtu na kushindwa umba dhahabu
Please naomba nitajie element zinazounda dhahabu,Mimi nikupe element zinazounda Mtu/binadamu halafu twende field tuone nani ataibuka bingwa
Pia nakukumbusha utajaribu kama Kuna dhahabu ya maabara itatokea na Mimi nitakuonesha jinsi Gani human manipulation na cloning project inaweza ibua kiumbe chochote maabara na ukastaajabu,
Elimu! Elimu! Elimu!
 
Inawezekana kweli nina low IQ, pengine ndiyo maana toka awali nikasema kwa kweli hili somo la Annunaki limenishinda!

Kwa uelewa wangu mdogo nimeaminishwa mwanadamu ameumbwa na Mungu. Inawezekana hakuna popote umetamka Annunaki ni Mungu lakini kwa kusema tu, Annunaki alimuumba mwanadamu tayari unahubiri kuwa Annunaki ni Mungu sijui unanielewa? Umetamka mwenyewe INDIRECTLY, pengine PASIPOKUJITAMBUA kwamba Annunaki ni Mungu lakini tena wewe wewe unakanusha!!!

Ninaposema juu ya makuhani, ninamaanisha nyie mnaomhubiri Annunaki!!! Nyie mnao mtafutia Annunaki kajinafasi ndani ya mioyo yetu ndiyo makuhani wenyewe!! Na ninawaomba mkamsome upya huyo Annunaki maana maelezo yenu kwa kweli ni lugha gongana! Hamueleweki na mnajikanyagakanyaga bila hata kujua!
 
Enlil ndiye Mungu wa anga aliyekuja na slogan ya heaven aand earth ambayo baadaye Quran ikaja kuiandika upya halafu kongole imeenda kwa allah
hahahahah hua nikisoma maandiko ya hizi Abrahamic religion hua nacheka Sana,laiti wafuasi wao wangejua waanzinzilishi wa hizi dhana ni Viumbe tu Tena intelligent wa kale wasingejisumbua kutaabisha miili Yao na nguvu zao kuwaabudu!
 
Sikia nikuambie kitu kimoja ankori unajua bible verses ilikopy maandiko ya kale ya Sumerian ila yenyewe iliweka nadharia tu za kuumbwa Kwa udongo na blabla ila amini kwamba maandiko ya kale kuliko bible yaani Sumerian tablets imeelezea binadamu na watu jinsi walivyofanywa na intelligent being ANNUNAK wakitumia human manipulation na cloning project ,
Ile science Leo ndio inatumika kuclone viumbe mbali mbali,pamoja na mimea ndio mbegu za GMO za kisasa zinazotumika Leo ,hiyo ni tech ya kale imerudiwa tu
Nitakupa SoMo!
 
Hivi vitabu ebu viorodheshe hapa tena(put the list of the annunaki books)
Ili tuchimbe tuelewe hizo hekaya za kale za huko Mesopotamia.

Kuna huyu jamaa Elon Musk,katika moja ya interviews zake akiwa anahojiwa kuhusu namna anavyomudu kazi mbalimbali za science and technology alijibu Kuwa yeye kama yeye amekuwa na utamaduni wa kusoma vitabu vingi sana tangu akiwa kinda kabisa wa miaka 5 hadi 6 hivi na alishawahi kusoma vitabu akiwa teenager vinavyohusu sayari za anga za mbali na kuhusu viumbe waliowahi kuitembelea dunia(Alliens) kuanzia hapo akastaajabu na ndipo alipopata msukumo wa kutaka kujua zaidi kuhusu universe as the whole na mpaka Leo anashangaa anadai the universe is infinitely,na pengine hii universe hii tuliyopo ambayo ina sayari lukuki na mabilioni ya nyota inaweza kuwa moja tu lakini kuna fununu kuwa kuna mabilioni ya universe kwa ukubwa na upana usio kifani.
Je hayo inaweza kuwa yapo kweli based on rejea zako kutoka hadithi/habari za Anunnak.
Je ni kweli au inawezekana Elon musk alisoma habari za hawa Anunnak?


Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Ankori labda wewe ndie brain washed juu ya neno 'Mungu'
Hebu Soma Tena nimetolea ufafanuzi kwanini nawaita Annunaki miungu

Unajua maana ya neno 'MUNGU'
lakini Ankori?
 
Ankori labda wewe ndie brain washed juu ya neno 'Mungu'
Hebu Soma Tena nimetolea ufafanuzi kwanini nawaita Annunaki miungu

Unajua maana ya neno 'MUNGU'
lakini Ankori?
Nieleweshe tafadhali! Nipo tayari kujifunza japo unajichanganya sana rafiki! Stori yako haina mtiririko unaoleweka! Unaongea, unajipinga, unajikubali! Naomba jikite kwenye kweli!
 
Ankori labda wewe ndie brain washed juu ya neno 'Mungu'
Hebu Soma Tena nimetolea ufafanuzi kwanini nawaita Annunaki miungu

Unajua maana ya neno 'MUNGU'
lakini Ankori?
Hapa unawaita miungu siyo Mungu!
Enlil ndiye Mungu wa anga aliyekuja na slogan ya heaven aand earth ambayo baadaye Quran ikaja kuiandika upya halafu kongole imeenda kwa allah
hahahahah hua nikisoma maandiko ya hizi Abrahamic religion hua nacheka Sana,laiti wafuasi wao wangejua waanzinzilishi wa hizi dhana ni Viumbe tu Tena intelligent wa kale wasingejisumbua kutaabisha miili Yao na nguvu zao kuwaabudu!
Hapo, ume"support" tena Enril ndiyo Mungu siyo miungu.

Kuna mahali hapo kabla umesema Mungu wa Ibrahimu ni mkuu kuliko Annunaki. Lakini hapa unasema unawacheka wanaoamini Mungu wa Ibrahim! Now which is which please?
 
Hivi unaelewa utofauti wa creation na cloning?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…