Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Musa Solela Ngasa (40), mkazi wa Kijiji cha Nhobola, Kata ya Talaga, Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga, amenusurika kifo baada ya kupigwa ubavuni na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa mshale.
Akizungumza na vyombo vya habari, mhanga huyo amesema tukio hilo limetokea Januari 2025, majira ya saa kumi na mbili jioni, alipokuwa akitoka shambani kwake baada ya shughuli za kilimo.
Ngasa amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa miaka mitano.
Aidha, ameeleza kuwa amewahi kukumbwa na matukio mengine ya aina hiyo, na mara kadhaa amepatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.