Anwani za makazi - maoni

Anwani za makazi - maoni

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Utaratibu wa kuwa na anwani za makazi ni jambo jema sana; Napongeza sana Serikali yangu
hata hivyo ninamapendekezo yafuatayo;

1. napendekeza kuwe na nyongeza ya kuelekezwa namna ya kuandika anwani baada ya kupata namba kwenye Nyumba;
Mf: utakuta nyumba imeandikwa #46 sinahakika nikisema Naishi Bugurini - Dar; nyumba #46 imetosha?
Namaanisha kila mtu ataandika kivyake na pengine kuchanganya; mwingine; Buguruni dar, karibu na Msikiti mkuu, nyumba namba #46 nk Nimeandika kwa kuwa kwenye maeneo kuna vitu maarufu pengine kuliko mitaa yenyewe; mf: Shule za zamani, Viwanda, Hospitali, Misikiti/makanisa nk. mfano; nakaa morogoro mjini karibu na geti la kiwanda cha Tumbaku # 46 NK

2. Nimeona Namba zina andikwa kwa kalam (nafikiri Marker pen) wananchi wasipokuwa makini muda sio mrefu nyingi zitafutika hasa Vijijini; sijui kutakuwa na utaratibu gani wa kuhakikisha zinadumu tusirudi huko baada ya miaka 5)
Pengina kila Halmashauri iweke utaratibu wa kuboresha na kwa kuanzia, kila kiongozi kuanzia ngazi ya chini kabisa awe na Kopi ya namba za Nyumba za eneo lake

nimawazo yangu!
 
Kule singida mjini namba zimeandikwa za kudumu badala ya kuandika kwa marker pen, hali kadhalika barabara zote zimeandikwa kwa vibao. Kuna barabara na mitaa imepewa majina kutokana na kuzoeleka kuitwa hivyo, kuna mpaka anna mughwira road. Zoezi hili linaendelea wiki ya tatu sasa mji mzima unajulikana mitaa na barabara zake
 
Utaratibu wa kuwa na anwani za makazi ni jambo jema sana; Napongeza sana Serikali yangu
hata hivyo ninamapendekezo yafuatayo;

1. napendekeza kuwe na nyongeza ya kuelekezwa namna ya kuandika anwani baada ya kupata namba kwenye Nyumba;
Mf: utakuta nyumba imeandikwa #46 sinahakika nikisema Naishi Bugurini - Dar; nyumba #46 imetosha?
Namaanisha kila mtu ataandika kivyake na pengine kuchanganya; mwingine; Buguruni dar, karibu na Msikiti mkuu, nyumba namba #46 nk Nimeandika kwa kuwa kwenye maeneo kuna vitu maarufu pengine kuliko mitaa yenyewe; mf: Shule za zamani, Viwanda, Hospitali, Misikiti/makanisa nk. mfano; nakaa morogoro mjini karibu na geti la kiwanda cha Tumbaku # 46 NK

2. Nimeona Namba zina andikwa kwa kalam (nafikiri Marker pen) wananchi wasipokuwa makini muda sio mrefu nyingi zitafutika hasa Vijijini; sijui kutakuwa na utaratibu gani wa kuhakikisha zinadumu tusirudi huko baada ya miaka 5)

Ni mawazo yangu!
Zoezi la anwani za makazi ni kichekesho na ushenzi mtupu kwa anayejua nini maana ya anwani za makazi.
 
Back
Top Bottom