Anyimwa unyumba...... Kisa: mazoezi

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,282
Reaction score
248
Mpwa wangu (mtoto wa dada yangu) amenifuata asubuhi hii akilalamika ana miezi miwili hatafaidi ndoa yake. Kila aombapo mchezo mkewe humwambia amekatazwa na mwalimu wake wa mazoezi ya viungo, anadai kufanya mapenzi kutamsababishia kushindwa kupungua uzito. Mama huyo alishauriwa na daktari apunguze uzito.
Nimemwambia mpwa wangu apitie jioni ili tuongee vizuri.
Je nimshaurije huyu bwana mdogo?
 
Mambo ya mapenzi bwana, wakati mwingine ni vigumu sana kushauri maana waweza jikuta unavunja ndoa takatifu ya wapendanao.
 
Huyo Mwalimu wa mazowezi anataka kupewa yeye huo unyumba? mie nikifanya mazowezi kwenye sita kwa sita ndio mwili unakua poa, yy huyo analake jambo sio hilo,na huyu mpwa wako nae duh! anaipenda mpaka kakosa usingizi anarauka asubuhi yote hii, ukubwa kweli jalala sasa unayaanzaje mpaka umwambie huyo mke wa mpwa wako mpe mwenzio unyumba,mmh! kesi nyengine hasa mikasa.
 

kama ameshauriwa apunguze uzito kwa sababu ya ugonjwa ambao medically ni lazima apunguze uzito, then lazima amvumilie. Kama ni kutaka kuwa na shape nzuri wanavyodai wasichana wa siku hizi, hapo nina mawazo tofauti. Lipeleke kwa wazee, upate ushauri na ushahidi then chukua uamuzi, upi, wowote, bali usidhuru afya yake kwa namna yoyote.
 
Huyo mwalimu wake ni mwanaume, ndio maana, na hiyo dio mbinu yake ya kwanza kujichukulia kifaa kiulainiii bifu litakaposhindikana ndoa ikafa.
 
Tendo la ndoa haliongezi uzito wala kuzuia mtu kupunguza uzito...huyo mwalimu, pengine na mwanafunzi wake wana yao. Mimi naenda gym regularly kiasi walimu wengi wa mazoezi wamekuwa washkaji wangu sana. Niliwauliza siku moja kwa nini hawapendi kutrain wanaume, muda wote unakuta wako na wadada tu? Huyo mwalimu akatia mkono mfukoni akatoa manoti kibao ya elfu tano tano na kumi kumi, akaniambia unaona hii...nyie wanaume mkishalipa fees ya gym ndio basi...wadada wanatutoa na mishiko na 'penzi' wanatupa. Akaenda mbali zaidi kiasi cha kunionyesha wadada ambao ameshawala na walioliwa na matrainer wenzake pale gym, walikuwa wengi including wake za watu...Sijui kama alikuwa ananidanganya ili kujipa 'ujiko' lakini nilinote wale wadada alionionyesha kuwa kawala wako extremely close naye na wanamdekea dekea wakati akiwatrain, and the guy (the trainer) is in shape...I mean a goodlooking guy!

So jamaa awe makini sana, isije kuwa analipia kumegewa!
 
Huyo mwalimu wake ni mwanaume, ndio maana, na hiyo dio mbinu yake ya kwanza kujichukulia kifaa kiulainiii bifu litakaposhindikana ndoa ikafa.
Digna hakuna Mwanaume Mkware anayetaka Mwanamke aachane na Mumewe... Wanapenda kuwa~Marioooo tu.
 
huyo mwalimu wa mazoezi ndio mazoezi yenyewe!!!

Aisee.... inauma sana uchungu
 

Mmh!! walianzaje anzaje mazungumzo mpaka huyo mwalimu wa mazoezi akamshauri huyo mwanamama aache kufanya mapenzi? Mimi nilidhani mtu akifika gym kazi ni moja tu ya mazoezi anayoenda kufanya kumbe huwa kuna mazungumzo marefu yanaendelea mpaka na ya vyumbani? ASIDANGANYIKE huyo jamaa. Kuna uwezekano huyo mama akawa anapata huduma zaidi ya hiyo ya mazoezi.
 
huyo mwalimu wa mazoezi ndio mazoezi yenyewe!!!

Aisee.... inauma sana uchungu

Umeona ee Kamanda?! Visababu vingine jamani!! Pole Mpwa wa mwenzetu!
Afu kuna wanaomshangaa eti mwanaume anaipenda sana kiasi cha kukosa usingizi jamani haya mambo yaacheni tu kama yalivyo....
Zamani tulikuwa tunasimuliwa kuwa Bibi zeu walikuwa waki'nyimwa' wanaitisha kabisa kikao cha watu wazima, wanashtaki .'wazee wangu, mume wangu siku hizi anagoma kula chakula usiku' ujumbe unakuwa umefika sasa ole wako kuwepo na mtoto hakawii kukuumbua mbona kila siku tunakula pamoja na bebe mezani?

Hii ni haki bana na ukishaolewa kubali tu unless una sababu ya msingi kama kuumwa au umekatazwa kwa sababu za kidaktari .....sasa mwalimu wa mazoezi!! Mwe!
 
Waende wote kwenye hayo mazoezi kisha aone kama huyo mwalim atamuambia na yeye mwanaume alichomuambia mkewe!
 

Very true kamanda... this is contradictory, complication and confusing to me and probably many couples...

Hunyimwi hivihivi tu....
 
Waende wote kwenye hayo mazoezi kisha aone kama huyo mwalim atamuambia na yeye mwanaume alichomuambia mkewe!
safi sana

na nakuambia akienda pale utaona dada anakua moody na instructor anamuavoid yule dada au hatoi kabisa ushirikiano... he may even take a leave

It will take me some magic to believe otherwise
 
Huyo atakuwa amepata kidumu sehemu,ndoa gani ya kunyimana kwenye tendo halali kwa muda wote huo kwa sababu za hivyo?
 
Mmmh ndoa zina mambo jamani, mshauri aende nae kwa huyo trainer akamshauri hivyo mbele ya mumewe ili kuondoa mzizi wa fitna huku the owner wa hio gym akithibitisha lakini pia kiwango cha uelewa na elimu ya huyo trainer ni muhimu kufahamika otherwise ni mchezo wa maigizo tu ya ndoa, ena mkumbushe aende na sime kabisa na talaka mkononi akifika sivyo tu, habari yote iiishie hapo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…