Anza kuwanyima watu taarifa zako hasa ndugu ,marafiki

Anza kuwanyima watu taarifa zako hasa ndugu ,marafiki

hapo hapo mnasema tusijitenge na watu ili tupate connection ya kibiashara,kazi au deals,mmhhh
kwa kifupi mnatuambia tutoke magetoni wakati huo huo tujitenge na watu ila hapo hapo tuwe karibu na watu,maisha yamekuwa magumu cha kushika ni kipi???
Watu? nenda bar nunua bia Moja au soda wakilewa wataropoka kila kitu wewe unaenda kukifanyia kazi
 
Kumbe? Sawa!!
 

Attachments

  • 20240702_160117.jpg
    20240702_160117.jpg
    161.6 KB · Views: 2
Fanya kama wafanyavyo majasusi, hukwambia unachotaka kusikia au hukwambia kitu au vitu vinavyoonekana vya maana sana kwako lakini kiuhalisia havimharibia mambo yake Kivyovyote, lazima ujue namna ya kuongea....inabidi uwe na akili nyingi sana kuweza hili.
 
Watu mnataka kuishi kama digidigi.

Watu wasijue ili iweje na wakikua wewe unaharibikiwa nini na wasipojua wewe utafaidika na nini.

Haya ni mawazo ya kijinga tu ya watu ambao hawana dira wala muelekeo wa maisha.

Usishangae haya ni maelekezo ya waganga ama wachungaji matapeli watafta sadaka.
 
Umenikumbusha tena tabia hii wanayo wasukuma kanda ya ziwa.
Kuna mzee alikuwa na pesa nyingi na biashara kubwa hata siku moja ajawai kumwambia mke wala watoto sababu ya kutowaamini akamwamini rafiki. Siku amefariki kwa ajali yule rafiki alijikausha kimya na ndio tajiri.
Familia ile imebaki ikilima na kuishi kwa shida
We umejuaje wakati alimwambia rafiki yake tuu
 
Hizi ni kanuni za waliojipata!
Wasijue niko wapi si wanajua niko home
Nafanya nini - naosha vyombo /nafua /napika
Wasijue kazi na biashara wakati kazi yenyewe sina na biashara yenyewe hali kadhalika!
Mipango natoa wapi na maisha yenyewe sina 🤣🤣🤣
Anyway ushauri wako poa sana mkuu
 
hapo hapo mnasema tusijitenge na watu ili tupate connection ya kibiashara,kazi au deals,mmhhh
kwa kifupi mnatuambia tutoke magetoni wakati huo huo tujitenge na watu ila hapo hapo tuwe karibu na watu,maisha yamekuwa magumu cha kushika ni kipi???
Mtoa mada yuko sawa.

Ila ni kwa waliojipata tu... au wale ambao taa ya kijani imeshawawakia kuelekea kujipata!

Watu uliowazidi mafanikio unatakiwa uishi nao kwa AKILI na TAHADHARI kubwa sana!
 
Hizi ni kanuni za waliojipata!
Wasijue niko wapi si wanajua niko home
Nafanya nini - naosha vyombo /nafua /napika
Wasijue kazi na biashara wakati kazi yenyewe sina na biashara yenyewe hali kadhalika!
Mipango natoa wapi na maisha yenyewe sina 🤣🤣🤣
Anyway ushauri wako poa sana mkuu


Ukiwa haujajipata ndo unabidi Ku-hide information ili uweze Ku-link na the right people only

Maana wakijua upo broke financially ujue ndo wanafurahia sana kusikia hivyo.

All you need is to Hide ur information na kuwapa taarifa zako watu sahihi and mostly successful people.
 
Tumia kanuni ya kuwanyima watu taarifa zako .

Wasijue upo wapi
Wasijue unafanya nini
Wasijue Kazi yako
Wasijue biashara zako wala kazi zako.
Wasijue mipango yako

Hii -ndo njia bora ya kuwa safe wewe dili na watu ambao mnafanya wote maisha .

Hakikisha unakuwa na sura mbili

Hakuna kitu kinaleta heshima Kama watu kutokujua habari zako.


Haya mambo ukiweza kujifunza mapema na kuyaishi kabla ya kufanikiwa ni jambo zuri sana.
Kwa bahati mbaya sana hayafundishwi shuleni na wazazi au walezi wengi hawatoi ufahamu huu kwa watoto wao.
Wengine wame hati iwa
Na ndugu na marafiki kwa kuto kujua haya.
Rafiki wa Leo ukiwa kawaida ni adui yako ugakapfanikiwa.
 
Back
Top Bottom