Kwa hiyo ukishakamilisha hivyo vitu unaviloweka kwenye pipa kwa wiki moja kisha linatokea godoro.
Haahaa acha kujitoa ufahamu.
1. Baada ya kuwa na hayo mahitaji, kinachofuata ni uunganishaji au uundaji wa godoro. Utaamua saizi ya godoro ulitakalo.
2. Baada ya hapo. Utashepu godoro lako kwa kutumia makoa kwa kuunda fremu ya mfanano mawili au matatu au manne itategemeana unataka inchi ngapi?.
3. Utachukua wire wa kopa utaukata na kuushepu mfano wa zigizaga kwa saizi moja kwendana na futi size ya godoro utakalo. Utakata vipande vidogo vidogo 24 (Urefu 6 * Upana 4).
4. Unaichuwa steel-wire unaikata kwa mfanano ule ule wa inchi ya godoro.
5. Unachukua pamba yako safi tayari sasa kwa kutengeneza godoro.
6. Hatua hii ndio uundaji sasa wa godoro unapoanzia baada ya kuandaa kila kitu.
a) Unachukua vipande vya wire ya kopa unaviunganisha kwa kamba ya katani kuelekea urefu na upana wa godoro lako mfano 5*6 au 6*6.
b) Baada ya hapo. Unatandaza makoa yako ambayo uliyoyatengeneza kwa shepu ya fremu za godoro kwa kuunganisha huku yakipandiana kwa wire ya kopa aidha fremu 2 au 3 au 4.
c) Unaunganisha sasa na zigizaga ya wire wa kopa ulizoziunganisha awali. Unaweka steel-wire kwenye nafasi pembezoni mwa kila shimo la zigzaga. Baada ya hapo unaanza kufix au kuchomeka pamba yako sasa kwa ustadi mkuu.
Nitamalizia.