Anzisheni SACCOS za Kilimo kwa kila Jimbo

Anzisheni SACCOS za Kilimo kwa kila Jimbo

mwalimu Jr.

Member
Joined
Aug 20, 2008
Posts
51
Reaction score
4
HISIA za wananchi wengi ni kwamba 'wabunge' wanataka mfuko wa majimbo ili kulinda nafasi zao na wala sio kwa manufaa ya mkulima.

Mimi ninaishauri serikali kufikiria uwezekano wa kuanzisha SACCOS za kilimo za jimbo zitakazoendeshwa kwa kanuni maridhawa na safi za menejimenti na utawala chini ya uangalizi wa benki tarajiwa ya Wakulima.

Kwa hakika hili linategemea kama serikali yenyewe ina dhati ya kweli ya kuchochea mapinduzi ya kilimo nchini au inawasanii tu wakulima kwa kuwa uchaguzi mkuu wa 2010 unakaribia!!!

Kama nia ya serikali kweli ni kuwasaidia wakulima basi kinachohitajika ni kuacha utani na SACCOS na Benki za Kata na kuvijenga vitu hivyo vifikie hadhi ya Volksbank za Ujerumani eti.

Mwalimu kasema nani anabisha? Kama sio wanaotaarajia kupeleka ufisadi majimboni ?
 
Wazo zuri..

lakini nadhani hivi sasa ninavyoandika haya tayari kuna SACCOS za wananchi ktk sehemu nyingi maeneo ya vijijini. Siwezi kujua performance yao ipo ktk level gani au mtaji wao upo ktk level gani na wananchi wananufaikaje. Hivo suala hapa sio kuanzisha bali ni kuziimarisha hizi SACCOS zilizopo kwanza.

Ukweli mwingine ni kuwa sidhani kama kila wilaya inahitaji kuelekeza nguvu zake kwenye kilimo tu, nadhani kuna maeneo wanaweza kujikwamua kwa kasi kubwa zaidi kama wananchi wakiwezeshwa kwenye vipaumbele vinavyolipa zaidi kutegemea na mahali walipo, mathalan viwanda vidogovidogo, uvuvi, ufugaji, etc
 
Back
Top Bottom