Aomba namba za msichana, apewa namba nusu

Aomba namba za msichana, apewa namba nusu

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,329
Reaction score
2,644
Jana nilienda kwenye moja ya saluni kupunguza nywele..

Nikafika nikamkuta kinyozi yuko pekeyake anakula mziki akisubiri wateja..bila kuchelewa nikakaa kwenye kiti ili nipate huduma..wakati huduma inaendelea alikuja dada mmoja ambaye alipeleka simu yake ichajiwe na alikuwa ameifuata..kinyozi alimpa simu na wakaendelea na maongezi..

Sikutaka kufuatilia maongezi yao lakini nililazimika kufanya hivo baada ya kusikia kinyozi anaomba namba za simu za yule mchuchu..bi dada bila hiyana akamwambia aandike 0*****mwisho 94 ..kinyozi akauliza mbona ziko nane yule demu akamwambia kama anaona ana shida sana kuongea na yeye hizo namba mbili za mwisho afanye makisio akibahatisha basi akishindwa ndo hivo tena..kisha akaenda zake...

Jamaa aliduwaa mno lakini ndo hivyo hakuwa na jinsi..akaendelea kunipunguza nywele huku povu likimtokaa...

Dada zetu kama hamjisikii kutupa namba zenu semeni sitaki lakini siyo haya mnayotufanyia...sijui kinyozi alitaka kumwambia nini yule dada....[emoji25]
 
alimuweza ndo wakome tongoza tongoza
 
bahati gani mkikubal mnatuita TAKE AWAY tukiwakatalia TUNARINGA tutapoteza bahati mmmhhhh poleni
hiyo avatar inanishawishi nikuombe namba lakini ngoja niache maana nilishapewaga namba ya mama mtu..[emoji125]
 
hiyo avatar inanishawishi nikuombe namba lakini ngoja niache maana nilishapewaga namba ya mama mtu..[emoji125]
namba yangu ni 07645323_ _ hizo mbili utamalizia ni yangu kabisaaa usihofu Mkuu, piga muda wowote
 
Na wewe povu limekutoka[emoji1] [emoji1]
 
namba yangu ni 07645323_ _ hizo mbili utamalizia ni yangu kabisaaa usihofu Mkuu, piga muda wowote
[emoji3] [emoji3] [emoji3] ungemalizia tu mkuu maana naweza buni nkajikuta imetuma kwa mama j*sca [emoji125]
 
ukipatia u
[emoji3] [emoji3] [emoji3] ungemalizia tu mkuu maana naweza buni nkajikuta imetuma kwa mama j*sca [emoji125]
ukiipatia utanipata pia ukipatia namba ya mama jesca sio mbaya
 
Mmmmmmmhhhhhj[emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji35]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
namba yangu ni 07645323_ _ hizo mbili utamalizia ni yangu kabisaaa usihofu Mkuu, piga muda wowote
hihihihihi... wew kweli ni Ke, kwa izo namba naona watu wataokota dodo kwenye mpela
 
Back
Top Bottom