Aomba talaka kisa kapata kazi

Asipompa atapewa yeye baada ya kufanyiwa vitimbi vyote. Mwanamke akishasema hataki kuwa na wewe usipoteze muda kumshauri kwani tayari ameshaamua ndani ni suala la muda ataenda zake.
Wanaume tafuteni amani na furaha ya mioyo yenu kwanza vingine viwe vya ziada. Mwanaume hakikisha haya:
1. Unakula vizuri
2. Unavaa vizuri
3. Unafanya mazoezi
4. Unapata muda wa kushiriki burudani na starehe nyingine za afya
5. Unakuwa na akiba benki,simu na vitega uchumi vingine kibao
Mengine ONGEZA wewe
NB
MWANAMKE AKIKUPENDA HAWEZI KUTAMKA TALAKA AU KUACHANA KWASABABU YOYOTE ILE
 
Mpe talaka tu akafanye kazi
 
Huyo ni wewe mkuu! Pole maamuz ni yako na mke ni wako
 
Mwanamke anaruhusiwa kufanya kazi, aachiwe kufanya kazi.
 
MKuu, biashara ni kazi sawa na kazi zingine ila unavyooneka unataka kuheshimiwa si kwa social responsibility as a husband ila kwa economical power.
Una taka utoe approval kila kitu cha mkeo, hiyo ni micromanagement

Mtu mzima hachungwi, tabia ya mtu ni sawa na ngozi yake, kamwe haibadiliki, utafanya cosmetics tu but uhalisia utabaki km ulivyo.

Ndiyo maana wanaume tunakufa mapema kwa kujilimbikiza matatizo na majukumu yanayoepukika.

Acha mke afanye kazi bana, iwe biashara au kuajiriwa, yaani mtu mna miaka 9, huyo hata wivu ushaisha mshabaki kuwa life partners, interest kubwa si mapenzi yenu tu bali ustawi wa kizazi chenu.
 
Hivi mtu ahangaike kusoma miaka 17+ halafu umkateze kufanya kazi? Ukimkuta mwanamke amesoma kubalianeni kuhusu mambo ya ajira mapema kabla ya kuoana. Vinginevyo hata mimi ningechagua kazi over hiyo ndoa +utakuwa ulikuwa unamnyanyasa.

Kama hutaki mke atakayeajiriwa chagua ambao hawajasoma
 
Uhakika
 
Umenena vyema sana mkuu infact sio mimi mhusika
 
Kaka asante kwa mawazo mazuri nimezingatia ila mimi sio mhusika, hii hata yeye anaisoma
 
Ni ukweli halisi dada
 
Kama alikua anamsimanga kwa pesa na kumfanyia ubahili imekula kwake. Talaka ataitoa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…