Apandishwa mahakamani kwa madai ya kuitukana Serikali juu ya deni la Taifa

Naona Serikali imeanza kupita mitaani kuwasikiliza wanaoisema vibaya, Jamal Mikome mkazi wa Chanika amefikishwa mahakama ya Kisutu kwa madai ya kuitukana Serikali wakati akitoa povu kuhusu Deni la Taifa na kuinyima kura Serikali mwaka 2025.

Kwani wasipite pia kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mkataba wa bandari kama wanayo 'manpower' ya kutusikiliza mitaani?

========

Mkazi wa Chanika, Jamal Mikome (48) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka moja la kutumia lugha ya matusi kuitukana Serikali iliyopoko madaraka.

Mikome, ambaye ni mfanyabiashara, alifikishwa mahakamani hapo, leo Jumatatu Juni 19, 2023 na kusomewa shtaka lake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Neema Moshi akishirikiana na Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio.

Wakili Mosha amedai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya jinai namba 104/2023.
Akisomewa shtaka hilo, Wakili Moshi amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 28, 2023 eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio na eneo hilo, alitumia lugha ya matusi kwa kuitukana Serikali iliyoko madaraka.

Mwananchi

Mbona hiyo lugha yenyewe ya matusi haitajwi
 
Yaani hawa itabidi siku moja tuwafurumishe ikulu watoke wote..wanatuzoea sana..kenya mbona mwananchi anaruhusiwa kuitikana nana kuikosoa serikali na kuandamana pia
 
Naona Serikali imeanza kupita mitaani kuwasikiliza wanaoisema vibaya, Jamal Mikome mkazi wa Chanika amefikishwa mahakama ya Kisutu kwa madai ya kuitukana Serikali wakati akitoa povu kuhusu Deni la Taifa na kuinyima kura Serikali mwaka 2025.

Kwani wasipite pia kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mkataba wa bandari kama wanayo 'manpower' ya kutusikiliza mitaani?

========

Mkazi wa Chanika, Jamal Mikome (48) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka moja la kutumia lugha ya matusi kuitukana Serikali iliyopoko madaraka.

Mikome, ambaye ni mfanyabiashara, alifikishwa mahakamani hapo, leo Jumatatu Juni 19, 2023 na kusomewa shtaka lake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Neema Moshi akishirikiana na Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio.

Wakili Mosha amedai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya jinai namba 104/2023.
Akisomewa shtaka hilo, Wakili Moshi amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 28, 2023 eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio na eneo hilo, alitumia lugha ya matusi kwa kuitukana Serikali iliyoko madaraka.

Mwananchi

Fuc.k the idiotic govt
 
Endeleeni Kutukana Serikali ,Sheria aliyotunga Mwendazake haijafutwa mkae mkijua.
---

Jamal Mikome (48) Mkazi wa Chanika, Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 28, mwaka huu mkoani humo.
 
hii nchi ukitaka kuifaidi, soma
Wanao watukana na kuwaibia wananchi hawakamatwi, why?

hii nchi ukitaka kuifaidi na kupiga pesa, soma upate kazi then chukua kadi ya CCM kuzugia. kuhusu ufisadi, wala usihofu Kuna mbululazzzz wafia chama…..watashinda JF na kwingineko kukutetea. Wewe kuwa mtiifu tuu kwa chama. kikubwa usijionyeshe kama wewe ni peoplezzzz….hata kama unawapigia kura.
 
ipo day
FxHB4UfWAAYYeg7.jpg
 
Inawezekana kabisa, Kwa haya yanayoendelea, Samia atalazamika kufunga watu wasokua na Hatia.

Ni Hatari sana kua na Rais mbovu, alozungukwa na wajaza matumbo.
Hapana mtu huwezi mtukana rais matusi ya nguoni afu ukasema upo huru. uhuru usio na mipaka ni hatari. ipo siku utampa uhuru uloopitiliza mwanao atakushika pumbu mbele za watu
 
Back
Top Bottom