Apata 'ajali' angani akiwa kwenye ungo aangukia TANESCO

Hivi ni kwanini mara nyingi au mara zote wachawi wanaoanguka na ungo au kufumaniwa wakifanya mambo ya kichawi (Kuna mmoja aliwahi kukutwa uwanja wa ndege wa Dar es salaam akiwanga asubuhi ) huwa ni WANAWAKE?! Sijawahi sikia mwanaume kaanguka na ungo au kufumaniwa akifanya uchawi!.
Wanaume nasikia wako smart sana kwenye safari za anga za juu ndo maana hawapati ajali mara nyingi
ha haa!
 
Taharuki imetanda katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, baada ya mwanamke mmoja, ambaye jina lake halijafahamika, kukutwa akiwa uchi ndani ya ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akisafiri kwa ungo (ushirikina) kutoka Masasi, mkoani Mtwara, akielekea wilayani Nyasa, lakini alijikuta akianguka katika eneo la ofisi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya, tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa usiku kuamkia Machi 11, 2025.

TUKIO LINAVYOSIMULIWA

Kamanda Chilya ameeleza kuwa baada ya mwanamke huyo kukutwa katika eneo la jengo la TANESCO na umati wa watu kuanza kukusanyika, uongozi wa shirika hilo ulitoa taarifa kwa Kituo Kikuu cha Polisi Songea.

Askari polisi walifika haraka eneo la tukio na kumkuta mwanamke huyo akiwa uchi wa mnyama, huku akiwa amejificha kwenye moja ya vyoo vya ofisi hizo. Baada ya mahojiano ya awali, maafisa wa polisi waliamua kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Songea (HOMSO) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini hali yake ya kiafya, hasa ikiwa anatatizo la afya ya akili. Kwa sasa, amelazwa katika wodi namba nane akisubiri uchunguzi wa kitaalamu.

USHUHUDA WA WANANCHI

Tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa Songea, huku baadhi yao wakieleza kushangazwa na hali hiyo, ingawa serikali haitambui uwepo wa ushirikina.

Athumani Mohamed, mkazi wa Mtaa wa Ruvuma, amesema inadaiwa kuwa mwanamke huyo alipita karibu na Kanisa la Pentekoste REDMD (Walokole) ambapo alipoteza mwelekeo, na hatimaye akaanguka ndani ya uzio wa ofisi za TANESCO akiwa uchi huku usoni akiwa amepakaa unga.

Naye Asha Omari, mkazi wa Mtaa wa Mateka, ametoa wito kwa serikali na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli kuhusu tukio hilo. Alipendekeza kuwa mwanamke huyo anapaswa kuwataja watu aliokuwa nao kwenye safari hiyo ili hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya vitendo vya ushirikina ambavyo vinakwamisha maendeleo ya jamii.

TAMKO LA HOSPITALI

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk. Magafu Majura, amesema kwa sasa yuko nje ya mkoa kwa shughuli za kikazi, lakini alithibitisha kuwa uchunguzi juu ya hali ya mwanamke huyo unaendelea na taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
View attachment 3267564
Muda sii mrefu walokole watajitwalia utukufu kuwa maombi yao ndo yamemuangisha.Ukute ni kombola la mganga limemdungua ila sasa rangi za kila aina zitaanza kuonekana.
 
Daah, Kanisa la Pentekoste mmewasha moto 🔥 huko, wachawi wanaanguka kwa Jina la Yesu! Hii ni habari njema. Keep it up.

"Basi [Yesu] alipowaambia, 'Ni mimi', wakarudi nyuma, wakaanguka chini." (Yohana 18:6, SUV)
Huu ni mchongo wa hilo kanisa kurubuni waumini wake, na wwe umejaa!!
 
Taharuki imetanda katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, baada ya mwanamke mmoja, ambaye jina lake halijafahamika, kukutwa akiwa uchi ndani ya ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akisafiri kwa ungo (ushirikina) kutoka Masasi, mkoani Mtwara, akielekea wilayani Nyasa, lakini alijikuta akianguka katika eneo la ofisi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya, tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa usiku kuamkia Machi 11, 2025.

TUKIO LINAVYOSIMULIWA

Kamanda Chilya ameeleza kuwa baada ya mwanamke huyo kukutwa katika eneo la jengo la TANESCO na umati wa watu kuanza kukusanyika, uongozi wa shirika hilo ulitoa taarifa kwa Kituo Kikuu cha Polisi Songea.

Askari polisi walifika haraka eneo la tukio na kumkuta mwanamke huyo akiwa uchi wa mnyama, huku akiwa amejificha kwenye moja ya vyoo vya ofisi hizo. Baada ya mahojiano ya awali, maafisa wa polisi waliamua kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Songea (HOMSO) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini hali yake ya kiafya, hasa ikiwa anatatizo la afya ya akili. Kwa sasa, amelazwa katika wodi namba nane akisubiri uchunguzi wa kitaalamu.

USHUHUDA WA WANANCHI

Tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa Songea, huku baadhi yao wakieleza kushangazwa na hali hiyo, ingawa serikali haitambui uwepo wa ushirikina.

Athumani Mohamed, mkazi wa Mtaa wa Ruvuma, amesema inadaiwa kuwa mwanamke huyo alipita karibu na Kanisa la Pentekoste REDMD (Walokole) ambapo alipoteza mwelekeo, na hatimaye akaanguka ndani ya uzio wa ofisi za TANESCO akiwa uchi huku usoni akiwa amepakaa unga.

Naye Asha Omari, mkazi wa Mtaa wa Mateka, ametoa wito kwa serikali na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli kuhusu tukio hilo. Alipendekeza kuwa mwanamke huyo anapaswa kuwataja watu aliokuwa nao kwenye safari hiyo ili hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya vitendo vya ushirikina ambavyo vinakwamisha maendeleo ya jamii.

TAMKO LA HOSPITALI

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk. Magafu Majura, amesema kwa sasa yuko nje ya mkoa kwa shughuli za kikazi, lakini alithibitisha kuwa uchunguzi juu ya hali ya mwanamke huyo unaendelea na taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
View attachment 3267564
Afya ya akili jumlisha ulinzi duni wa ofisi husika.
 
Kuna mmoja miaka fulani hivi nyuma kipindi nasoma Pugu, kuna kanisa kama unaelekea kajiungeni aliangukaga kwenye hilo kanisa usku wa saa nane walokole wanafanya maombi yao. Tukanda kumshuhudia.
 
Taharuki imetanda katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, baada ya mwanamke mmoja, ambaye jina lake halijafahamika, kukutwa akiwa uchi ndani ya ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akisafiri kwa ungo (ushirikina) kutoka Masasi, mkoani Mtwara, akielekea wilayani Nyasa, lakini alijikuta akianguka katika eneo la ofisi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya, tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa usiku kuamkia Machi 11, 2025.

TUKIO LINAVYOSIMULIWA

Kamanda Chilya ameeleza kuwa baada ya mwanamke huyo kukutwa katika eneo la jengo la TANESCO na umati wa watu kuanza kukusanyika, uongozi wa shirika hilo ulitoa taarifa kwa Kituo Kikuu cha Polisi Songea.

Askari polisi walifika haraka eneo la tukio na kumkuta mwanamke huyo akiwa uchi wa mnyama, huku akiwa amejificha kwenye moja ya vyoo vya ofisi hizo. Baada ya mahojiano ya awali, maafisa wa polisi waliamua kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Songea (HOMSO) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini hali yake ya kiafya, hasa ikiwa anatatizo la afya ya akili. Kwa sasa, amelazwa katika wodi namba nane akisubiri uchunguzi wa kitaalamu.

USHUHUDA WA WANANCHI

Tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa Songea, huku baadhi yao wakieleza kushangazwa na hali hiyo, ingawa serikali haitambui uwepo wa ushirikina.

Athumani Mohamed, mkazi wa Mtaa wa Ruvuma, amesema inadaiwa kuwa mwanamke huyo alipita karibu na Kanisa la Pentekoste REDMD (Walokole) ambapo alipoteza mwelekeo, na hatimaye akaanguka ndani ya uzio wa ofisi za TANESCO akiwa uchi huku usoni akiwa amepakaa unga.

Naye Asha Omari, mkazi wa Mtaa wa Mateka, ametoa wito kwa serikali na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli kuhusu tukio hilo. Alipendekeza kuwa mwanamke huyo anapaswa kuwataja watu aliokuwa nao kwenye safari hiyo ili hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya vitendo vya ushirikina ambavyo vinakwamisha maendeleo ya jamii.

TAMKO LA HOSPITALI

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk. Magafu Majura, amesema kwa sasa yuko nje ya mkoa kwa shughuli za kikazi, lakini alithibitisha kuwa uchunguzi juu ya hali ya mwanamke huyo unaendelea na taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
View attachment 3267564
Huo usafiri urasimishwe ajali zinatokea kwa nadra sana
 
Hizo ndege kama kweli zipo ni wakati zisajiliwe sasa Ili ziruke mchana,maana zitasaidia kupunguza gharama na changamoto za usafiri,
Na Mimi nitasafiri kwazo Ili kusapoti sayansi ya Africa.
Raia wasafiri uchi? Sheria za kimataifa zinaruhusu?
 
Hii sayansi ya kufikirika haiwezi kudhibitishwa,
Huyo mtu atakuwa na matatizo ya akili.
 
Back
Top Bottom