Apata sifuri baada ya kutoa majibu sahihi

Apata sifuri baada ya kutoa majibu sahihi

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,252
MWANAFUNZI HUYU ALIPATA SIFURI LICHA YA KWAMBA MAJIBU YAKE YOTE YALIKUWA SAHIHI

SWALI: Mkwawa alikufa katika vita gani?
JIBU: Katika vita yake ya mwisho

SWALI: Mkataba wa Geneva ulisainiwa wapi?
JIBU: Mwisho wa karatasi

SWALI: Nini sababu kuu ya talaka?
JIBU: Ndoa

SWALI: Kitu gani ambacho huwezi kula wakati wa mlo wa asubuhi?
JIBU: Chakula cha mchana na cha usiku

SWALI: Kipi kinachofanana na kipande cha tunda?
JIBU: Kipande cha pili cha tunda hilo.

SWALI: Hitler alikufa vipi?
JIBU: Moyo wake uliposimama baada ya kufika malaika wa kifo.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom