Pre GE2025 Apewe maua yake kabla hajafa, Mbowe ni Mkufunzi, CHADEMA ni chuo cha wanasiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Ukweli ni lazima usemwe Mbowe ni jabali la siasa pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu,
Dhahiri CHADEMA chini ya ukufunzi wa Mbowe amekuwa ni mpishi muhimu kwa wanasiasa wa Tanzania, na wanafunzi wa Mbowe wengi wao wamekuwa wakishahitimu CHADEMA huchukuliwa na CCM moja kwa moja na kupewa nyadhifa mbali mbali serikalini.

Hiyo ni picha tosha kuwa wamepikwa na wakapikika na hujawahi kusikia Mbowe akiwajibu kwa lolote, japo kila mmoja anaehitimu CHADEMA huondoka kwa matusi na kejeli!

Tusiache mpaka mkufunzi Mbowe afe ndio tusifie kuwa aliandaa vijana wengi wanasiasa kwenye nchi hii.

Ushauri chadema ifungue chuo ianze kutoza ada!

Tumpe maua yake ingali bado yupo hai!

Viva Mkufunzi wa siasa Aboubakari Mbowe malipo yako utayakuta kwa Mungu
 
Lakini ni wakati sasa Mangi amuachie Lissu.
 
Nakubaliana na wewe kwa jambo moja, mbowe aachie ngazi.

Sikubaliani na wazo la kuachiwa lisu. Lisu hawezi kuongoza chama, yeye aendelee kuwa mropokaji tu kwenye chama. Uenyekiti wa chama unahitaji mtu mwenye hekima, lisu hana hiyo.
 
Naungana hoja moja kwa moja

Anastahiki pongezi nying kwa ukomavu wa hali ya juu.

Chama kimeishi miaka mingi japo kmepitia meng sana.

Vimekuja ving na kudondoka ila kupitia ukomavu wake na akili nyingne chama kinazid kuimarika na kuleta chachu kwa chama tawala.

Uongozi wake madhubuti nathubutu kusema angekuwa mwepesi chadema kingekuwa mfu kitambooo

Analeta chachu kwenye siasa za tanzania. PONGEZI KWAKO MBOWE. Kama siasa unaijua

Mapungufu mengne ni sehemu ya maisha na uongozi.
 
Nakubaliana na wewe kwa jambo moja, mbowe aachie ngazi.
Sikubaliani na wazo la kuachiwa lisu. Lisu hawezi kuongoza chama, yeye aendelee kuwa mropokaji tu kwenye chama. Uenyekiti wa chama unahitaji mtu mwenye hekima, lisu hana hiyo.
Mbowe ye ni kimya na vitendo tuu
 
Ukweli ni lazima usemwe Mbowe ni jabali la siasa pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu,
Dhahiri CHADEMA chini ya ukufunzi wa Mbowe amekuwa ni mpishi muhimu kwa wanasiasa wa Tanzania, na wanafunzi wa Mbowe wengi wao wamekuwa wakishahitimu CHADEMA huchukuliwa na CCM moja kwa moja na kupewa nyadhifa mbali mbali serikalini.

Hiyo ni picha tosha kuwa wamepikwa na wakapikika na hujawahi kusikia Mbowe akiwajibu kwa lolote, japo kila mmoja anaehitimu CHADEMA huondoka kwa matusi na kejeli!

Tusiache mpaka mkufunzi Mbowe afe ndio tusifie kuwa aliandaa vijana wengi wanasiasa kwenye nchi hii.

Ushauri chadema ifungue chuo ianze kutoza ada!

Tumpe maua yake ingali bado yupo hai!

Viva Mkufunzi wa siasa Aboubakari Mbowe malipo yako utayakuta kwa Mungu
Tuliyasema kitambo wao wanarudia tu!
 
Back
Top Bottom