APHFTA: Tumesikitishwa na Aga Khan kusitisha huduma ya NHIF, Taasisi nyingi za Afya zinaweza kusitisha pia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wiki iliyopita Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam inayomilikiwa na Taasisi ya Aga Khan ilitangaza kusitisha mkataba kati yake na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Vituo 11 kati ya 24 vinavyomilikiwa na Taasisi hiyo Nchini ikiwemo Hospitali ya Aga Khan Dar kwa sababu ya changamoto za kiuendeshaji.

Kutokana na maelezo na taarifa ya Aga Khan pamoja na ile ya NHIF ni kuwa leo Agosti 13, 2024 ndio itakuwa mwisho wa huduma hiyo kutolewa kwenye vituo hivyo.

Baada ya hali hiyo, JamiiForums imezungumza na Mwenyekiti wa Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (APHFTA), Dkt. Egina Makwabe ambaye anaelezea kuhusu suala hilo, anasema:

Aga Khan ni Wanachama waaminifu kabisa wa APHFTA, tumesikitishwa na kilichotokea kwa kuwa wao (Aga Khan) ni wawekezaji na wameweka mambo mengi ikiwemo teknolojia, kuajiri Wafanyakazi, walipa kodi wakubwa, hivyo tunapoona ustawi wao unapitia hali hiyo ni hali ya kusikitisha.

Sababu kubwa nadhani ni kutoelewana na NHIF kwenye masuala ya bei hasa katika Suala la Kitita.

Kile Kitita kinachotumiwa na NHIF hakina maslahi kwenye uendeshaji wa huduma za Aga Khan, kwani hichohicho ndicho kinachotumiwa na Taasisi za Afya za Serikali.

Taasisi za Serikali zinazotumia Kitita zinakuwa na usaidizi kutoka Serikalini tofauti na kwenye taasisi binafsi kama Aga Khan ambao wanalipa kodi, wamejenga majengo kwa gharama kubwa, wana mikopo mikubwa.

Sera ya Aga Khan ni kutoa huduma ya juu kwa gharama kutokana na ubora wa huduma zao, nadhani wameshindwa, wameona hauendani na gharama wanazotumia.

Nadhani hii ni “wake up call” kwa Wizara ya Afya, NHIF na APHFTA, tulizungumza lakini ni kama bei hazitaweza kuwa rafiki.

Kwa mazingira hayo, hospitali nyingi zitashindwa kujiendesha kutokana na Kitita kilichopo, mfano ni huo wa Aga Khan, nina uhakika baadhi ya hospitali nyingine zitafuata, japokuwa siyo jambo jema.

Duniani kote sekta binafsi ndio inaendesha Uchumi, lazima kuwe na mazingira mazuri ya kuiwezesha Sekta Binafsi ili iweze kukua.

Uwekezaji katika Sekta ya Afya ni gharama kubwa Dunini kote, Serikali inakusanya kodi ili ziende wapi? Ni ili iweze kujenga miundombinu ya afya, Elimu na Barabara.

Watanzania wamejitolea kuisaidia Serikali kuwekeza katika afya, hivyo ni vizuri kuweka mazingira wezeshi na rafiki.

Niwaombe NHIF, Wizara wakae ili ipatikane bei wezeshi ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa ubora wa hali ya juu.

Aga Khan ni hospitali inayotoa huduma kwa kiwango cha juu, ni hospitali peke yake inayotoa huduma ya kiwango cha juu peke yake, sasa bei ndio tatizo, hivyo wana haki na Serikali ingeweza kuwasikilia ili kuwe na bei stahiki ili kutengeneza mazingira ya bei wezeshi.

Lazima kuwepo na bei mbili ya Private na Serikali kwenye hicho kitita cha INHIF.

Ukiangalia uwekezaji wa Aga Khan mfano yale majengo ni mabilioni ya fedha ambayo mwingine wamepata kwa mikopo kutoka Benki ya Dunia, itarudije? Ni kupitia kwa huduma.

Mfano kwa nini Serikali isiseme itatoa mikopo kwa bei nafuu kama inavyofanya kwenye kilimo ili Taasisi ziweze kukopa.

Sasa hivi Watanzania wakiugua wakiwemo viongozi wa Tanzania kwa nini wanaenda India? Wakienda huko hawaendi Hospitali za Serikali, wanaenda Hospitali Binafsi ikiwemo ambazo zinashirikiana na Taasisi za Serikali za hapa nchini.

Hiyo haikuja hivihivi, India iliamua kwa makusudi, waliamua kuwezesha katika hospitali binafsi zikakopeshwa na Dunia nzima inaenda India kupata huduma.

Tukiweza kufanya hivyo, hata Nchi zinazotuzunguka zitakuja kupata huduma kwetu Tanzania.
 
Si mlisema ooh hospitali binafsi zinachaji gharama kubwa sana kuliko uhalisia? Leo mambo yanageuka....government hospitals zinapata subsidy kutoka seeikalini, unataka utoe package sawa na private hospitals, una wazimu?
 
Hodpitali ya selikali kuanzia majengo, vifaa tiba, madawa mpaka mishahara ya wafanyakazi inalipwa na serikali bila kujali hospitali hiyo ibaingiza mspato kiasi gani. Kwa kifupi wanatoa huduma kwa ruzuku ya serikali.

Hospitali binafsi nyingi kila kitu nilichokitaja hapo juu wanajilipia wenyewe.

Alafu NHIF wanatoa fedha hiyohiyo kwa hospital zote, wako serious kweli hawa?? Na waziri wao Ummy ambae hata sio mtaalamu wa afya.
 
Nimefurahishwa na hiyo hoja ya mwisho inayosema Kwa Nini viongozi kama rais waziri na wabunge wakiugua hukimbilia India?Kwa Nini wasitibiwe hapahapa?Kuna wengine hata tezi dume tu walienda kutibiwa marekani.Hii inaonesha hospitali zetu hazikidhi ubora.Serikali kaeni chini mmalize huu mgogoro wa aghakhani.Huduma zitoleeazo aghakhani ni Bora kuliko hizo hospitali zenu ndiyo Maana ninyi viongozi hamutaki kutibiwa huko
 
Kwa Private for Profit company its all about dollars and if it don't make dollars then it doesn't make sense...

Kwahio tuwaache na biashara zao sababu wanajua ni vipi wanapata faida ila kwa sisi wenyewe tuboreshe hospitali za UMMA sababu Afya ni Huduma sio kuwapangia watu wenye biashara zao jinsi ya kufanya biashara (hio sio charity)

Wiki iliyopita Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam inayomilikiwa na Taasisi ya Aga Khan ilitangaza kusitisha mkataba kati yake na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Vituo 11 kati ya 24 vinavyomilikiwa na Taasisi hiyo Nchini ikiwemo Hospitali ya Aga Khan Dar kwa sababu ya changamoto za kiuendeshaji.

Kutokana na maelezo na taarifa ya Aga Khan pamoja na ile ya NHIF ni kuwa leo Agosti 13, 2024 ndio itakuwa mwisho wa huduma hiyo kutolewa kwenye vituo hivyo.

Baada ya hali hiyo, JamiiForums imezungumza na Mwenyekiti wa Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (APHFTA), Dkt. Egina Makwabe ambaye anaelezea kuhusu suala hilo, anasema:

Aga Khan ni Wanachama waaminifu kabisa wa APHFTA, tumesikitishwa na kilichotokea kwa kuwa wao (Aga Khan) ni wawekezaji na wameweka mambo mengi ikiwemo teknolojia, kuajiri Wafanyakazi, walipa kodi wakubwa, hivyo tunapoona ustawi wao unapitia hali hiyo ni hali ya kusikitisha.

Sababu kubwa nadhani ni kutoelewana na NHIF kwenye masuala ya bei hasa katika Suala la Kitita.

Kile Kitita kinachotumiwa na NHIF hakina maslahi kwenye uendeshaji wa huduma za Aga Khan, kwani hichohicho ndicho kinachotumiwa na Taasisi za Afya za Serikali.

Taasisi za Serikali zinazotumia Kitita zinakuwa na usaidizi kutoka Serikalini tofauti na kwenye taasisi binafsi kama Aga Khan ambao wanalipa kodi, wamejenga majengo kwa gharama kubwa, wana mikopo mikubwa.

Sera ya Aga Khan ni kutoa huduma ya juu kwa gharama kutokana na ubora wa huduma zao, nadhani wameshindwa, wameona hauendani na gharama wanazotumia.

Nadhani hii ni “wake up call” kwa Wizara ya Afya, NHIF na APHFTA, tulizungumza lakini ni kama bei hazitaweza kuwa rafiki.

Kwa mazingira hayo, hospitali nyingi zitashindwa kujiendesha kutokana na Kitita kilichopo, mfano ni huo wa Aga Khan, nina uhakika baadhi ya hospitali nyingine zitafuata, japokuwa siyo jambo jema.

Duniani kote sekta binafsi ndio inaendesha Uchumi, lazima kuwe na mazingira mazuri ya kuiwezesha Sekta Binafsi ili iweze kukua.

Uwekezaji katika Sekta ya Afya ni gharama kubwa Dunini kote, Serikali inakusanya kodi ili ziende wapi? Ni ili iweze kujenga miundombinu ya afya, Elimu na Barabara.

Watanzania wamejitolea kuisaidia Serikali kuwekeza katika afya, hivyo ni vizuri kuweka mazingira wezeshi na rafiki.

Niwaombe NHIF, Wizara wakae ili ipatikane bei wezeshi ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa ubora wa hali ya juu.

Aga Khan ni hospitali inayotoa huduma kwa kiwango cha juu, ni hospitali peke yake inayotoa huduma ya kiwango cha juu peke yake, sasa bei ndio tatizo, hivyo wana haki na Serikali ingeweza kuwasikilia ili kuwe na bei stahiki ili kutengeneza mazingira ya bei wezeshi.

Lazima kuwepo na bei mbili ya Private na Serikali kwenye hicho kitita cha INHIF.

Ukiangalia uwekezaji wa Aga Khan mfano yale majengo ni mabilioni ya fedha ambayo mwingine wamepata kwa mikopo kutoka Benki ya Dunia, itarudije? Ni kupitia kwa huduma.

Mfano kwa nini Serikali isiseme itatoa mikopo kwa bei nafuu kama inavyofanya kwenye kilimo ili Taasisi ziweze kukopa.

Sasa hivi Watanzania wakiugua wakiwemo viongozi wa Tanzania kwa nini wanaenda India? Wakienda huko hawaendi Hospitali za Serikali, wanaenda Hospitali Binafsi ikiwemo ambazo zinashirikiana na Taasisi za Serikali za hapa nchini.

Hiyo haikuja hivihivi, India iliamua kwa makusudi, waliamua kuwezesha katika hospitali binafsi zikakopeshwa na Dunia nzima inaenda India kupata huduma.

Tukiweza kufanya hivyo, hata Nchi zinazotuzunguka zitakuja kupata huduma kwetu Tanzania.
NIMEGUNDUA UKIENDA GOVERNMENT HOS UNAPATA HUDUMA ZOTE BILA SHIDA!!!

SHIDA NI KWENYE PRIVATE HOS.
 
Back
Top Bottom